CUF yaandaa mgomo Zanzibara!

Mbona mnakimbia mada iliyo mbele na kuanza stori nyingine?
Huyo mwakilishi wanataka wam -ZITO.
Waangalie, manake kufungia kuna matokeo wasiyoyatarajia!
Kuandamana ni haki yao kama wanaona wana hitaji hilo! Polisi wawapeni ulinzi!
 
kama imethibitishwa kuwa mchele ni mbovu, basi mgomo huo ni lazima kutokea kwa manufaa yao wenyewe wananchi, na sio kwa manufaa ya chama.
 
CUF yaandaa mgomo dhidi ya bidhaa za BOPAR




Na Ali Suleiman, Zanzibar

CHAMA cha CUF kimesema kitaitisha mgomo Unguja na Pemba kuwataka wananchi kususia mchele unaoagizwa na kampuni ya BOPAR Enterprises baada ya kubainika kwamba ni mbovu.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Salim Bimani, alisema jana kwamba mchele unaoagizwa na kampuni hiyo ni mbovu na haufai kwa matumizi ya binadamu, na kudai kuwa Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo.


"Saratani kwa asilimia kubwa inatokana na watu kula vyakula vibovu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu, sasa sisi tunataka kulishughulikia tatizo hili kwa kulikomesha moja kwa moja," alisema Bw. Bimani.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) juzi ilitoa taarifa kuhusu mchele mbovu uliozusha malalamiko kwa wajumbe wengi wa Baraza hilo, ambapo ripoti yake haielezi hali halisi ya mchele huo unaolalamikiwa.

Lakini taarifa hiyo ilisema inakusudia kuwachukulia hatua kali baadhi ya watendaji wa taasisi zinazojishughulisha na vyakula kikiwamo kitengo cha kumlinda mlaji kwa kutokuwa makini katika kushughulikia tatizo hilo.

Akichangia taarifa hiyo, Mwakilishi wa CUF, Bw. Haji Faki Shaali, alisema Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo, ambaye amekuwa akifadhili CCM.

BOPAR Enterprises kwa muda mrefu wamekuwa wakiingiza vyakula vilivyo chini ya viwango. Kuna wakati aliingiza unga wa ngano mbovu, na wananchi walipofahamu walisusa kununua unga huo au boflo zilizo okwa kwa unga huo.
Kitendo cha kuendelea kuleta vyakula vibovu vinapaswa kusimamishwa mara moja. Kwa hili naungana na mjumbe wa Baraza Uwakilishi aliyetoa hoja hiyo.

Nafikili kuna tatizo kubwa katika kitengo cha kulinda haki za mlaji kama ilivyo ainishwa na SMZ. Hivyo ni bora kwa SMZ hiyo kuhakikisha kuwa kitengo hicho kinawajibika kwa kuwalisha wananchi chakula kibovu.

Ziadi Mhe.Shaali amechemka sana na kauli yake, na anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni na sheria za Baraza la Wawakilishi
 
mzee kibunango

sheria ina kazi si mchezo.

ukweli chakula ni kibovu na ni muda mrefu sana wazanzibar wanalishwa mlo mbovu, ila utashi na jazba bila ya kuangalia unaweza kusema maneno yakakueka hatiani.

sasa kuthibitish kauli yake ni kazi.

madai ya kuwa bopar anaingiza mlo mbovu ni kweli ila kuthibitisha kuwa ccm wanamlinda kwa kuwa ni mfadhili wake.
 
Wafanyakazi wa SMZ na hasa wa kitengo cha kulinda Haki za Mlaji ndio wanaomlinda Bopar. Hili linajulikana na ni wakati sasa kulipatia utatuzi wa kudumu. Sasa huyo mwakilishi akisema kuwa ni ccm atakuwa tu anaongea kwa jazba zake juu ya ccm, kwani hicho chama sio ambacho kimeajiliwa na SMZ kwenye Kitengo cha Kulinda Haki ya Mlaji.

Kauli zingine badala ya kunenepesha hoja huwa zinaikondesha, hoja kama ya huyo mwakilishi. Ndani ya wafanyakazi wa SMZ kuna CCM na CUF vile vile, sasa kukurupuka na kusema kuwa CCM inamlinda Bopar si sahihi kabisa, na anapaswa kuadhibiwa tu...
 
CUF pia ilisema kuna vifo vingi vinavyosababishwa na matumizi ya dawa zisizofaa na vyakula vilivyomaliza muda wake.

Chama hicho kimelaani hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kuthubutu kuficha ukweli juu ya kashfa ya kuingizwa nchini mchele mbovu.

Alisema ni jukumu la SMZ kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika ili kulinda afya za wananchi.
Sijui ni ukweli gani ambao SMZ wamejalibu kuuficha!..

Zaidi Soma hapa
 
Back
Top Bottom