Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 676
CUF yaandaa mgomo dhidi ya bidhaa za BOPAR
Na Ali Suleiman, Zanzibar
CHAMA cha CUF kimesema kitaitisha mgomo Unguja na Pemba kuwataka wananchi kususia mchele unaoagizwa na kampuni ya BOPAR Enterprises baada ya kubainika kwamba ni mbovu.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Salim Bimani, alisema jana kwamba mchele unaoagizwa na kampuni hiyo ni mbovu na haufai kwa matumizi ya binadamu, na kudai kuwa Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo.
"Tunaunga mkono juhudi za Mwakilishi wetu Shaali, kufichua uoza na kusema ukweli kuhusu mchele...ingawa ukweli huo Serikali haiutaki...tunakusudia kuitisha mgomo kuwataka wananchi wasinunue mchele wa BOPA," alisema Bw. Bimani.
Alisema wananchi wa Zanzibar wamechoka kulishwa vyakula vibovu ambayo vinahatarisha afya zao, kwani baadhi ya wagonjwa kutoka Zanzibar wanaotibiwa katika hospitali ya saratani Ocean Road, Dar es Salaam, wanakabiliwa na matatizo hayo.
"Saratani kwa asilimia kubwa inatokana na watu kula vyakula vibovu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu, sasa sisi tunataka kulishughulikia tatizo hili kwa kulikomesha moja kwa moja," alisema Bw. Bimani.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) juzi ilitoa taarifa kuhusu mchele mbovu uliozusha malalamiko kwa wajumbe wengi wa Baraza hilo, ambapo ripoti yake haielezi hali halisi ya mchele huo unaolalamikiwa.
Lakini taarifa hiyo ilisema inakusudia kuwachukulia hatua kali baadhi ya watendaji wa taasisi zinazojishughulisha na vyakula kikiwamo kitengo cha kumlinda mlaji kwa kutokuwa makini katika kushughulikia tatizo hilo.
Akichangia taarifa hiyo, Mwakilishi wa CUF, Bw. Haji Faki Shaali, alisema Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo, ambaye amekuwa akifadhili CCM.
Madai hayo yalipingwa na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kutakiwa Mwakilishi huyo, kutoa ushahidi wake au kuomba radhi, ambapo yeye alisema hatafanya hivyo.
Sakata la Mwakilishi wa CUF kwa sasa limepelekwa kwa Kamati ya Maadili na Kinga ya Baraza la Wawakilishi, ambayo itafanya uchunguzi wa suala hilo pamoja na mwakilishi kuwasilisha ushahidi wake.
Hatima ya Mwakilishi Shaali itajulikana mwakani, ambapo Mkutano wa Baraza la Wawakilishi utapokea ripoti na taarifa ya Kamati hiyo.
source majira