CUF wilayani Kwimba wawaponda viongozi Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wilayani Kwimba wawaponda viongozi Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145


  Monday, 21 March 2011
  CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani Kwimba, kimewaponda viongozi wa Chadema kwa uchochezi na kumpongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuongoza nchi kwa amani.Pongezi hizo zilitolewa juzi na Katibu wa CUF wilayani hapa, Julius Samamba, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ngudu wa kupinga maandamano ya uchochezi yaliyofanywa na Chadema.Katika maandamano hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Christopher Kangoye, Samamba, ambaye ni Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wilayani hapa, alisema Watanzania wasikubali kutumiwa kwa maslahi ya wachache, hivyo kuzua vurugu na machafuko ya kisiasa.


  Alisema Rais Kikwete ana nia na ameonyesha jitihada za kudumisha amani nchini, lakini viongozi wa Chadema wanataka kuivuruga kwa uchochezi na maandamano yasiyo na tija.Aliongeza kuwa kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi maana yake siyo kuzusha machafuko kwani, chama kikishika dola kinachofuata ni kutekeleza amani, kujenga uchumi ili nchi iendelee na wananchi wafaidi matunda ya Uhuru.“Mamlaka ya serikali yoyote yanatoka kwa Mungu hivyo bila kukubali kushindwa hakuna amani, Kikwete ni rais makini, anastahili pongezi ndiyo maana nasema wazi, uchaguzi ulishakwisha na sasa tunataka amani siyo machafuko,” alisema Samamba na kuongeza.“Mnaonisikiliza hapa msikubali kutumiwa kwa matatizo yenu kuzua tatizo la machafuko, CCM ndiyo iliyo madarakani lazima tuiheshimu.”Alisema rais Kikwete aliahidi kutatua mgogoro wa Zanzibar akatimiza sasa ameahidi Katiba mpya itaandikwa kuondoa manung’uniko, lakini Chadema wanataka kuzusha vurugu.Pamoja na kuwapongeza wananchi wakiwemo Sungusungu zaidi ya 2,000 waliohudhuria mkutano huo wa kupinga uchochezi wa Chadema, alidai wana - Kwimba siyo sawa na tembo ambaye pamoja na maguvu yake hunyeshewa mvua porini, wawaogope viongozi wachochezi.Naye Mbunge wa Kwimba Shanif Mnsoor akiwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao, alisema waachane na watu wanaoitukana serikali waliyoichagua.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mtumbwi ni chombo muhimu huko zenji ila ni gogo la kuachwa shambani litafunwe na mchwa huku tabora (bara)
  so siasa za CUF wengi tunaziona ni gogo
   
 3. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao CCM-B ungetarajia waseme nini? madam baadhi ya hoja walizowasilisha kwa njia ya mandamano serikali inafanyia kazi. Hapo uchochezi uko wapi? CUF wameishafungwa bao la kisigino huko Zanzibar na Bara. Hawana jipya.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  huu ndio mwendelezo wa yale yanayotokea Kuanzia Dodoma- Kisiwa ndui- Buguruni hadi kwa Bw. Samamba Kwimba. Wanachosahau kusema ni kuwa MAANDAMANO ya CDM ni halali kisheria ni ya AMANI na ndiyo maana yanaruhusiwa na yanafanyika. Kama yangekuwa ni ya uvunjifu wa amani nadhani wangeyazuia na kukifuta CDM so hizo ni kelele za chura. CUF na CCM ni chanda na pete siyo wapinzani hao
   
 5. Salathiel m.

  Salathiel m. JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CUF Zenj huku ni kapu tu!!
   
Loading...