Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF bwana Juma Duni Haji ametetea vikali mswada wa katiba mpya uliopitishwa na bunge na kusema hata mwalimu Nyerere wakati wa uandaaji katiba ya mwaka 1977 aliteua wajumbe nusu kwa nusu kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Waziri huyo ameilaani Chadema na kumfananisha Tundu Lissu na mtu asiye na akili. Bwana Juma Duni Haji ameyasema hayo katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kimerekodiwa na kitarushwa siku ya Jumatatu.