CUF wazidi kuiandama CHADEMA

Ha ha ha, Hivi Chadema alau ina Tawi lilo hai ndani ya Zanzibar? CUF ina vitu vya Ubuge mpaka Tanganyika na ina madiwani, sasa kipi kinapaswa kufungiwa na Tendwa?

Usianze kuropokwa kama hujamsikia Juma Duni alicho zungumza. Subiri Juma tano kipidi kitarushwa tena kwa marudio. Mulidhani Juma Duni, Maalim Seif na watu wa CUF wote watakuwa mabubu na kutafuna maneno kisa wamo serikalini? Hapana kabisa kabisa! Tumekubaliana kuwa na maridhiano kwasababu zote ni ndugu hakuna haja ya kuuwana tena. Zaidi tumeipunguzia mzigo serikali ya Tanganyika ya kuleta vifaa vya kijeshi kama vile Zanzibar kuna vita. Sasa hamuoni hiyo faida moja kwa serikali ya Tanganyika? Au raha zenu muje mtupige ikisha musingiziye mambo ya 1953-1964?

Duni kashasema na Maalim Seif kashanguruma Zanzibar. Kauli ni moja, Zanzibar kwanza, tusdhalilike kwa sababu tuna fadhiliwa ardhi huko Taganyika. Utu wako ndio muhimu kwa hiyo na sisi utu wetu ndio kwanza ikisha ndio ufahari wa mali.
 
Sio kweli, nimekuwa nikifuatilia kauli yingi za Chadema. Wanapo jaribu kutaka kujinadi basi jambo la mwanzo, nchi hii WMalimu nyerere hivi hivi, kitu si kitu mwalimu Nyerere hivi hivi, huyu Mwalimu nani haswaa hata ikawa ndio nukuu kubwa kwa wanasiasa wa tanganyika?

Sisi Wa-Zanzibari hatuukubali kwamba Muungano huu kwanza ni halali. Kilichopo ni ubabe tu uliotumika na ulaghai. Kama wazee wetu walikuwa woga basi sisi vijana tunasema basi. Kwa hiyo ni sawa kwenu kumuona Mh Juma Duni hana maana, lakini kwetu sisi ni lulu na fahari kuwa na kiongozi kama yeye ndani ya CUF na SMZ. Wekeni kongamano, na mutowe Chadema kumi kwa Juma Duni mmoja kama mutaweza kujibu hoja moja kutoka kwake....
 
Hatusemi hatutaki Muungano. Tunacho sema Muungano ni mzuri lakini si huu wa sasa. kama ni huu bra tusiwe na Muungano. Sera ya CUF ni kuwa na Muungano wa serikali tatu, na kama hilo haliwezekani basi Muungano basi.

Lakini haki kama hiyo na nyinyi Watanganyika munayo yakuamua kama munakubaliana na masharti yetu. Hamulazishwi lazima lazima muwe na sisi Zanzibar. Hatukuja kuomba Muungano, aliye kuja na shauri hili ni huyo Saint wenu Nyerere. Kwa lazima mufahamu hilo, si kuporoja tu. CUF tupo wazi kabisa kwenye kauli zetu na tupo makini, upooo wewe?
 
Wazanzibar wanampango wa kututengenezea katiba mbaya halafu wao wanruka kiunzi na kutukimbia na kutuacha tukuhangaika
 
Nyakati zao cuf walikuwa wakiupinga muungano huu sana.... leo wamepata wapi nguvu za kuukubali? nini kimebadilika??? yaani wao wanaolingana na mkoa mmoja wa kwetu Tanganyika tuwe sawa wawakilishi??
Nyerere alikosea kwa hili kama alivyokosea na mambo mengine na hatuwezi kukubali kuburuzwa na kupoteza taifa letu Tanganyika.

Kweli,
Kama nyerere alifanya blanda,tusiogope kumkosoa kisa ndo muasisi wa taifa,swala la muungano na zenji alikurupuka tu,au alikua na maslahi yake binafsi,kwani tanganyika tunawategemea zenji kwa lipi?
Kama vipi turudishiwe tanganyika yetu manake tanzania ni ya kifisadi,labda nayo ijivue gamba nahis changes zitaonekana. !
 
shame on them KAF mwisho wao waja 2015 hakuna anae wataka tena hawa wadin walio olewa na magamba b.
 
Back
Top Bottom