Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
Chama cha Wananchi CUF kimesema kiko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya muafaka na Chama cha Mapinduzi endapo mazungumzo hayo sasa yataongozwa na Rais Kikwete mwenyewe kama Mwenyekiti. Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema leo kuwa kwa vile kamati zilizoundwa kushiriki mazungumzo hayo zimemaliza kazi zake, na kutokana utata uliotokea baada ya maamuzi ya Butiama basi ipo haja ya mazungumzo hayo kufanywa na viongozi wa juu.
Uamuzi wa CUF amesema umezingatia kuwa ni yeye Rais Kikwete aliyeahidi kutafutia ufumbuzi mpasuko wa kisiasa uliodumu visiwani Zanzibar kwa muda mrefu sasa.
Hadi sasa hivi haijajulikana kama Rais Kikwete atakuwa tayari kusimamia mazungumzo hayo yeye mwenyewe hasa baada ya wale waliotakiwa kufanya hivyo kuonekana kushindwa au kutokuwa na nguvu ya kufikia muafaka wa kweli.
Hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM inatarajia kufanya kikao chake maalum kusimamia ile "agenda ya siri". Rais Kikwete amemaliza ziara yake ya siku sita mkoani Singida muda mfupi uliopita.