CUF wakanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif

CUF wakanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
128
Reaction score
93
Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif ambazo zilianza kusambaa tangu jana jioni kwamba kiongozi huo amefariki dunia

Jussa Ismail Jussa, amesema taarifa hizo sio za kweli. Pia amezungumzia hali ya kisiasa mjini Zanzibar kwamba kwa sasa hali si shwari.

JUSSA: Niwaambie kwamba ni mzima na kwa hakika tuko Dar es Salaam asubuhi na mimi nimefatana nae, asubuhi tumekuja tumekuwa na miadi ya kuonana na balozi wa jamhuri ya watu wa China katika Tanzania. Tumetoka katika mazungumzo hayo, yuko mzima. Jana alikuwa ameendelea na mazungumzo ya vikao ambavyo vinafanyika katika ikulu ya Zanzibar kuhusu suala la mgogoro wa Zanzibar. Hivyo niwatolee wasiwasi, Maalim yuko fiti kabisa. Wapuuze uvumi huu na wawapuuze wenye nia hizi mbaya.

Bahati mbaya kwenye nchi yetu sasa yamekuwa ni mazoea haya, watu wanatumia vibaya mitandao ya kijamii lakini kumekuwa na hii tabia ya kuombeana mabaya tu kila wakatilakini niwaambie njama zao hazitafanikiwa, Maalim Seif anaendelea kufanya kazi zake.

Hali ya kisiasa Zanzibar bado ni ya wasiwasi, mimi nilikuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Malindi na nina cheti changu cha kuthibitisha nimechaguliwa kihalali, watu wengi wanafatilia kwa kina iwapo maamuzi ya ya tarehe 25 Oktoba kama yataheshimiwa.

Hali ya amani itategemea sana kufanikiwa kwa jitihada hizi na nichukue fursa hii kuomba sana viongozi wa Tanzania hasa Rais John Magufuli ambae ameanza kwa kasi nzuri sana asiruhusu suala la Zanzibar kuvuruga kazi nzuri alioifanya na sote kwa pamoja tuchukue jitihada kuona haki inatendeka.


 
Last edited by a moderator:
Hii taarifa ni ya kutia wasi wasi zaidi.
 
Baada ya kuona mkakati wao wa kurudia uchaguzi kule Zanzibar umebuma, hao jamaa wanekuja na 'mkakati' huu mwingine wa kuvumisha kuwa mshindi huyo wa kiti cha Urais huko Zanzibar hatunaye tena hapa duniani.
Itabidi TCRA wawatie nguvuni haraka iwezakanavyo hao waliovumisha uvumi huo, wasiishiage tu kuwakamata akina Yericko..........
 
Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif ambazo zilianza kusambaa tangu jana jioni kwamba kiongozi huo amefariki dunia

Jussa Ismail Jussa, amesema taarifa hizo sio za kweli. Pia amezungumzia hali ya kisiasa mjini Zanzibar kwamba kwa sasa hali ni shwari.

Amesema wanasimamia misingi ya amani lakini wataendelea na majukumu yao ya kutafuta haki kwa watu wote na pia wanampongeza Rais John P. Magufuli kwa kuchaguliwa kwake.

Kwa hiyo CUF inatambua ushindi wa Magufuli?
 
Lisemwalo lipo kama halipo basi laja
 
Si afe tu,kwani atakua wa kwanza kufa,mbona kipenzi chetu nyerere kafa na watu tuko kimya?
 
Kwanza tu imenistuka sana! Hawa watu hawana aibu tusishangae lakn kwa kweli utakuwa mwisho wa amani Tz.
 
Ukawa. Ndo. Mabingwaa. Wa kusambaza. Izo. Taarifa. Mfano. Mkuu wa majeshi. Kafa. Mkapa. Amekufa.
 
Ccm kwenye cc hakukuwa na agenda ya znz. Tanganyika inatazama tu kik0l0ni chake kikiteketea
 
Back
Top Bottom