CUF wakanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif

mkuu hivi kumbe yule kijana mzushi aitwaye yericko yupo ndani? afadhali maana sasa hivi angalau hapa JF pamekuwa mahali salama pa kupatia habari badala ya uzushi.

Baada ya kuona mkakati wao wa kurudia uchaguzi kule Zanzibar umebuma, hao jamaa wanekuja na 'mkakati' huu mwingine wa kuvumisha kuwa mshindi huyo wa kiti cha Urais huko Zanzibar hatunaye tena hapa duniani.
Itabidi TCRA wawatie nguvuni haraka iwezakanavyo hao waliovumisha uvumi huo, wasiishiage tu kuwakamata akina Yericko..........
 
Yanayoingiliwa huko si la uchaguzi wa mwaka huu pekee.

Unafahamu asili ya muungano wenyewe?

Unafahamu yaliyotokea katika matokeo ya chaguzi zote tangia vyama vingi vianze?

Yalikuwa yapi? Na ilikuwaje?

Kwa taarifa yako tu ni kuwa kuna watu 'wana-influance', haikutokea mara moja, si mara mbili wala tatu.

Nakuomba usinitie majaribu niende 'in deep', -Nikasughulikiwa na sheria ya mtandao.

Sitaki kuamini kuwa hujui.

-NIMEFUNGA MJADALA-
Usiufunge, nionyeshe kwanza ni wapi Magufuli anahusika kwenye mambo ya ZEC tuendelee na mambo mengine. Hiyo sheria ya mtandao wala usiwe na wasiwasi nayo kama una uhakika na unachokiandika.
 
Kuna tofauti kati ya ujinga na upumbavu, huyu au hawa waliotoa taarifa hii ni wapumbavu kwasababu wanaujua ukweli, lakin wangekuwa wajinga ingewezekana pengine kufanya makusudi au bahati mbaya, kama lengo lao maalim Seif afe kwanza watatangulia wao maana haya mengine ni ya Mungu sio ya mafatani.


Tunza akiba ya maneno, usisukumwe na hisia zako tu. Waweza yakana uliyoyaandika.
 
Nyie mbuzi,malofa na mapumbavu sio nyie mliokuwa mnapinga sheria ya mitandao? Sasa mnazungumza utumbo gani humu, tatizo la nyumbu hakumbuki tukio la dakika iliyopita mwenzie kuliwa na mamba,dakika ileile anarudi palepale. Hata huyo aliiponda sheria ya mitandao halafu sasa analalamika mitandao kutumiwa vibaya ........fankuuuuuuro
 
Hakuna mtu anayeweza kukurupuka tu na kusambaza uzushi wa namna hii.Hata kama CUF wamekanusha,lakini kuna kitu kinachoendelea hasa ukizingatia hali ya kisiasa Zanzibar.Upo upande utakaofaidika na kifo cha Maalim Seif kwa kiwango kikubwa.

Tusubiri,ukweli utadhihirika,mbona njia ya mwongo ni fupi.
Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif ambazo zilianza kusambaa tangu jana jioni kwamba kiongozi huo amefariki dunia

Jussa Ismail Jussa, amesema taarifa hizo sio za kweli. Pia amezungumzia hali ya kisiasa mjini Zanzibar kwamba kwa sasa hali si shwari.




 
Last edited by a moderator:
Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif ambazo zilianza kusambaa tangu jana jioni kwamba kiongozi huo amefariki dunia

Jussa Ismail Jussa, amesema taarifa hizo sio za kweli. Pia amezungumzia hali ya kisiasa mjini Zanzibar kwamba kwa sasa hali si shwari.






I must admit, Jussa ana akili sana huyu jamaa. Katika kujibu hili suala, hakuacha mwanya kwa wajanja kuweza kumu edit kama alivyowacha mwanya Vuai (naibu katibu wa CCM Zanzibar). Nilishangaa sana style anayotumia Vuai kujibu suala ama kutoa statement akiwa kama kiongozi mmoja mkuu wa CCM bila ya kujuwa athari ya style anayotumia katika maendeleo ya teknolojia ya kisasa. Welldone Jussa.
 
Last edited by a moderator:
Usiufunge, nionyeshe kwanza ni wapi Magufuli anahusika kwenye mambo ya ZEC tuendelee na mambo mengine. Hiyo sheria ya mtandao wala usiwe na wasiwasi nayo kama una uhakika na unachokiandika.

Wewe unajiwehusha.
Wapi nimemtajq Magufuli Mimi?
 
Masuala ya uchaguzi Zanzibar yapo chini ya ZEC, chombo ambacho hakipo chini ya muungano na Magufuli hana mamlaka nacho. Narudia tena, ni mambo yao na wayamalize wenyewe. Sisi kwetu tumetimiza wajibu wa kulikata fisadi na kazi inaendelea.

Jaribu kutumia kilicho kichwani mwako efficiently hata kama ni kamasi.
Mkuu vipi bana?
Kwa nini unatoa rai ambayo haimbatani pia haiendani na uhalisia?
Tanzania ni nini? Je Zanzibar ni Tanzania? Je ni nchi jirani ya Tanzania? Je Zanzibar ni mbia wa Tanzania?

Linalohusu hapa ni hili.
Nani alipeleka Jeshi ? Nani ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi Tanzania? Kama una majibu ya maswali hayo ,ishirikishe akili yako katika kufikiri kwa upana. Je Muungano unahusika?Je Magufuli anahusika?

Link1. https://twitter.com/thomasamter/status/658965881284857856

Zanzibar electoral commission lockdown

On the semi-autonomous archipelago of Zanzibar, the announcement of the election was temporarily suspended after soldiers stormed the collation centre, eventually evicting journalists and observers.

Link2. Tanzania election: Government ministers suffer shock defeat - BBC News

Kama umetimiza wajibu wa kulikataa fisadi, kwa nini tunaruhusu ufisadi uendelee huko Zanzibar?

Lubuva alichukua kura za Zanzibar katika kufanikisha hili la kulikataa fisadi, kwa nini tunataka kulea fisadi aliyevaa mavazi ya kijani na manjano huko Zanzibar?

Najua utarudi kurusha madongo, lakini Magufuli anasema msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Tuseme ukweli na tuepuke unafiki.
 
Kumbe Cuf wanamtambua magufuli,na wameitambua kasi yake kuwa ni nzuri,asante Jussa

Zanzibar ni nchi kama mnavyoimba kila siku. Yamalizeni wenyewe ya nchi yenu.

Ukawa inabomoka.
Cuf ni mdau mkubwa wa Ukawa.
Ukawa inadai haimtambui JPM kama rais halali, lakini Cuf wanamtambua vema.
Na ule ulongo wa Zanzibar inamlaka kamili umefika mwisho kwani kilivyobuma tu Maalim kakimbilia kwa Kikwete na sasa wote wamemgeukia JPM.
Ukawa ilikuwa gia ya kutafutia tu kura za uchaguzi.
Ndo maana humsikii Mbowe au yule jamaa wa 'Mama Tanzania' wakivalia njuga ishu ya Zanzibar.
 
Baada ya kuona mkakati wao wa kurudia uchaguzi kule Zanzibar umebuma, hao jamaa wanekuja na 'mkakati' huu mwingine wa kuvumisha kuwa mshindi huyo wa kiti cha Urais huko Zanzibar hatunaye tena hapa duniani.
Itabidi TCRA wawatie nguvuni haraka iwezakanavyo hao waliovumisha uvumi huo, wasiishiage tu kuwakamata akina Yericko..........

Ulisikia wapi tcra ikakamata watu wanaokebehi na kutukana upinzani, we upo nchi gani, ingekuwa ni chama tawala na serikali yake tayari alishakamatwa na tukamjua ni nani, lakini kwa hili ndugu sahau
 
Back
Top Bottom