CUF waishambulia CHADEMA

Nakubakiana nawe mkuu, lakini chanzo kikuu ni hicho, you wait and see hali iko hivyo time will tell na wewe utashuhudia hayo. Hatuna haja ya kubishana let us hope for the best.
 
jamani naona kuna watu huenda hawajafahamu au kwa makusudi hawataki kufahamu kilichozungumzwa

mm nimeona vitu viwili

kwanza chadema wao wako tayari kushirikiana na CUF na wala hawaonyeshi kua na wasi wasi na kuunda upinzani na CUF

la Pili chama cha CUF kinaona sio busara kuunda umoja wa upinzani wa Vyama viwili tu, wao wanaona vyama vyote vyenye wabunge vya upinzani vishirikishwe na wanaamini kuwafata CUF tu wawe kwenye kambi hio sio sawa na CUF wanahesabu ni mtego na Chadema kukosa msimamo

la tatu alizungumzia kuhusu gharama ya kutomtambua Rais


na la mwisho ambalo hata na mm ningependa kujua kua Chadema imewakwaza viongozi wakuu wa NCCR na CUF kivipi ?
 








Mimi naona kwa hili kuwa kama Zanzibar vyama viwili ndio vimeungana serikari ya Kitaifa kwa nini wasihusishe na vyama vingine huko zenji?
 
Jamani, mi nafikiri CUF sio chama cha Upinzani, na CHADEMA hawana sababu ya kuwashirikisha CUF kuunda kambi ya upinzani maana wataidhoofisha sana.
Sababu:
Ikiwa CUF na CCM wameunda serikali Zanzibar na Katibu wao (CUF) Mkuu ndiye makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na wabunge wake 7 wameshika wizara. Si rahisi kwao kuja Bara (Serikali ya Muungano) na kugeuka kuwa Wapinzani wakiwa chini ya Katibu Mkuu wao ambaye pia ni Serikali.

Hapa panahitaji fikra za dhati na uelewa mkubwa!!!!!!! Naamini CHADEMA ndio wapinzani wa kweli wanaoweza kuleta changamoto kwa Selikali kwa manufaa ya Taifa.
 
Hapa tukubali tukatae kuna element za udini, japo kuna deeper issues than this. Nilitegemea kusikia maneno ya busara yangetoka kwa Hamad Rashid, matokeo yake katoa pumba tupu. Totaly immatured!
 
Mimi naona kwa hili kuwa kama Zanzibar vyama viwili ndio vimeungana serikari ya Kitaifa kwa nini wasihusishe na vyama vingine huko zenji?


katiba ya zanzibar inaelekeza vipi serikali hio itaundwa


vyama vyenye uwakilishi barazani kwa sasa ni viwilitu ila fursa iko kwa kila chama chenye wawakilishi kushirikishwa kwa mujibu wa uakilishi wake
 
Hapa tukubali tukatae kuna element za udini, japo kuna deeper issues than this. Nilitegemea kusikia maneno ya busara yangetoka kwa Hamad Rashid, matokeo yake katoa pumba tupu. Totaly immatured!


kama yepi ?

kukubali vyama viwili kuunda umoja na kuviona vyengine kwa kua na uwakilishi mdogo si wapinzani ?


chadema mtulie muache makeke


ngoma yataka matao
 
CUF yenyewe ilipata muafaka baada ya kutomtambua Karume eti leo ndio wamekuwa watu wa kumshauri Chadema iendelee kumtambua mchakachuaji??? This is a joke!
CHADEMA inatakiwa iendelee na msimamo huo huo hakuna haja ya kuwasikiliza walionunuliwa kwa muafaka sasa wanakubali hata uchakachuaji!
Lazima hili suala la uchakachuaji liwatese sana CCM mpaka washike adabu. Chadema inafanya hivi kwa manufaa ya Demokrasia ya Tanzania ya sasa na vizazi vijavyo. Lazima uchakachuaji uwatese kila walalapo na kuamka ndio dawa pekee ya kuukomesha.

Safi sana CHADEMA.
 

Pamoja na hao wabunge 7 wa CUF wameshika wizara hiyo ni kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ujuwe Nchi yetu inaendeshwa na Serikali mbili Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa hao Wabunge 7 wa chama cha CUF waliochaguliwa kwa upande wa Serikali ya Zanzibar tu si kwa ajili ya Serikali ya Muungano. Usichanganye suala la Seriakali ya Mapinduzi Zanzibar na ukatia na masuala ya Serikali ya Mungano wa Tanzania ni vitu viwili tofauti hapo mkuu.
 

Safi sana, I think you are right..
 

Hamna lolote wanaiogopa CCM tuu ambayo imeshawaoa.
 
Chadema kimedhihirisha kuwa ni chama chenye nguvu na ambacho kimekubalika kwa wananchi.
Wajitahidi wafanye kazi kwa umakini mkubwa katika kutetea maslahi ya wananchi bungeni.Haina haja ya kubishana na hao CUF,wawaache tu kwani wameshajitundika kitanzi na kifo chao kinawanyemelea.
Cha msingi kwa chadema ni kufunga mjadala huu wa kambi ya upinzani bungeni na kujipanga dhidi ya hila yoyote ya kukivuruga chama.
Kuna mpango wa kuchafua taswira ya Chadema kwa wananchi,lakini ukweli utabaki palepale wananchi hatudanganyiki.Fanyeni wajibu wenu sisi tutatoa hukumu.
 

CUF ni moja,hakuna CUF ya bara na ya visiwani.Sana sana inanguvu visiwani ambapo iko ndani ya serikali,kwa hiyo usitegemee hata siku moja wakaipinga serikali.Haya yote ni matunda ya muafaka wa ccm na cuf.
 

liwalo na liwe historia itasema kwa hivyi sasa vyama vyingi ni machaka ambayo yanatunza makenge nyoka ng'e mitulanongo.....dawa kufeka chaka uzuri wananchi upofu umepungua nb ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA!
 

cuf waweke mambo yao sawa kwanza kwa kuwa cuf zina mapande manne 1cuf mageuzi 2cuf upemba 3cuf udini 4cuf uccm tushirikiane na cuf ipi ili cuf ipi isichonge?maana kila cuf ina malengo yake....
 
Chadema will be better off if they go alone as the leader of the oppsition in parliament; any attempt to co-opt other parties will make their task unnecessarily harder as these so called parties will just be MOLES of the ruling party!!
 
Makubaliano ya kuunda kambi ya upinzani yanahusisha uongozi wa chama ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kisera, msimamo na mitazamo mbali mbali inayogusa maswala ya jamii.

Ni rahisi kuunda kambi ya upinzani yenye vyama vichache kwa kuwa ni rahisi kukubaliana misimamo na sera na kwamba wapinzani kwa umoja wao watasimamia nini.

Bunge la 9, Kambi ya Upinzani chini ya Hamad ilimtimua Cheyo kwa kuwa alienda Bungeni kusema kitu ambacho hawakukubaliana kwenye vikao vyao vya kambi ya upinzani. Cheyo alienda kulalamika kwa Spika, Spika akamtoa baruti kwamba alienda kinyume na msimamo wa kambi, na maamuzi ya Kambi ya Upinzani hayawezi kuingiliwa na Spika.

Leo Hamad anataka kuongeza matatizo kwamba Mrema na Cheyo waingizwe kwenye kambi ya upinzani. Mrema alikuwa anampigia kampeni JK na ilihali ana mgombea Urais wa chama chake, huyo ndio unaweza kumwita mpinzani? Cheyo alishaonyesha kwamba yuko against upinzani tangu Bunge lililopita, lini amebadilisha msimamo wake?

Kafulila juzi amepingana na Mnyaa kwamba alichokifanya hayakuwa makubaliano ya kambi ndogo ya upinzani, lakini yalikuwa ni maamuzi yake binafsi. Huo ni mfano mdogo tu wa jinsi ambavyo umakini unahitajika mnapoamua kuungana na kuunda kambi kubwa ya upinzani.

Uongozi wa CHADEMA na NCCR wana tofauti kubwa sana ambazo zinahitaji mjadala mkubwa ili kuweza kuzimaliza na si za kuongelea kwa siku moja na kuzimaliza. Kafulila na Mkosamali wote wametokea CHADEMA na walitofautiana viongozi walio madarakani. Marando ametoka NCCR nae ana tofauti zake na Mbatia, sasa ukiunganisha hayo lazima kuwe na muda wa kutosha ku-reconcile.

Kwa ujumla Hamad naona anatafuta excuse ya kwanini waliamua kuunda kambi ndogo ya upinzani. Lakini sioni future ya hiyo kambi ndogo kwa kuwa tayari CUF wameishaonyesha wazi kwamba wako tayari ku-give in kwa CCM na si kwa upinzani. Ndio maana Hamad hakusema kitu siku Mnyaa alipojitoa, Kafulila kilimuuma kwa kuwa aliona wazi kwamba NCCR nao wataonekana wanawaunga mkono chama tawala na ili hali msmamo wao hauko hivyo.

Huo ndio upinzani wa Tanzania, sometimes it is much better kila chama kikaendelea kivyake badala ya kuunda kambi za kinafiki na ilihali kila chama kina agenda zake za siri.
 
A bit politically apologetic. Nadhani ni CUF ndiyo inayoona hatari ya hata mbunge wake mmoja kuteuliwa kuwa waziri kivuli bungeni zaidi kuliko chadema kutomtambua rahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…