CUF sasa yakosa sura ya kimuungano

CUF sasa yakosa sura ya kimuungano

Huna ukweli kwenye hoja yako ungemfundisha mwanao hesabu sio kutuletea mapovu hapa shika adabu yako
Tatizo ninyi wenye vichwa vyepesi hamuwezi kufikiri kwa ku-extrapolate matukio.
Mbowe aliambiwa ajichunge sana asigombane na dola akabisha, aasema yeye na UKUTA na UKUTA ni yeye.
Sasa kakumbushwa deni lake la nyumba na kufungishwa virago.
Amekuwa mpole na mdogo kama piritoni.

Maalim siku zake zinahesabiwa , hata mkono hatoi kwa wanaombeba, CUF ni yeye na yeye ni CUF.
Lazima kuna jambo atakumbushwa muda si mrefu.
 
Ukiangalia kwa juu juu una weza kukubaliana na watoa mada. Maalim ame wasaidia sana wafanya siasa wa bara akitaka kukuza chama ila bara wengi ni wasaliti hawana msimamo. Kuna kipindi kulikuwa na uchaguzi Maalim aka wapatia wa milioni 6 kila mmoja kwa ajili ya kampeni. Watu hawakupiga kampeni wakala pesa baada ya uchaguzi waka kimbilia ccm. Mapalala alikula dili na watu flani flani kutoka kwa Komandoo ili CuF ifutwe kisheria....alitengeneza nembo na bendera mpya ili kutengeneza mazingira ya kufutwa baadhi ya watumishi wa watawala waka mhabarisha Maalim na kuita mkutano wa dharura akiwa na Bendera na nembo mpya. Siasa ukiwa na njaa ina hitaji moyo sana na ndo maana ccm wana mwona Mbowe ni tishio kwa kuwa hawategemei kifedha.
Miaka ya mwishoni mwa 1990 wapinzani walitaka kutengeneza umoja wao wakauita UDETA..enzi hizo mwenyekiti wa Chadema alikuwa Mtei. Mtei aliitwa na msajili wa vyama wa enzi hizo marehemu mzee Liundi na kumweleza kuwa UDETA ni umoja unao sukumwa na watawala na wanataka kuangamiza upinzani nchi kwa ushauri wake akamwambia aitoe chadema kwenye UDETA...Rejea mahojiano ta Liundi na gazeti la Rai ya wakati huo.
Ni kazi sana kufanya siasa wakati kuna wasaliti wengi tu wamepandikizwa na watawala
 
Ni kwamba CUF ilikuwa na sura ya muungano baada ya kujishikiza kwa Chama cha Wananchi cha mzee Mapalala. Historia inaonyesha kwamba wale wanasiasa waliofukuzwa CCM wakati huo wakiwa akina Hamad Rashid, Seiff Shariff Hamad, Mloo, nk walianzisha KAMAHURU huko Zanzibar wakati wa vuguvugu la uanzishwaji wa vyama vingi. Baaada ya vyama vingi kuruhusiwa, KAMAHURU ilikosa sifa ya kuandikishwa kwa kuwa haikuwa na sura ya Muungano. Hivyo basi maalim na wenzake wakamfuata Mzee Mapalala akiwa na chama chake kikiitwa Chama cha Wananchi, wakaungana na kuanzisha CUF na hivyo kuwa na sura ya muuungano na kupata usajili. Baadaye wakamtupia virago Mzee Mapalala.

Hali ilivyo sasa ni kwamba CCW na KAMAHURU ndio vinajitenga na kujionyesha sura zao halisi na kwa hakika CUF itafutwa kwa kuwa itakosa sifa ya kisheria ya kuendelea kuwemo kwenye daftari l msajili wa vyama.
Pumba tupu, cuf ina sifa kuliko vyama vyote vya kisiasa, sifa kubwa na kuwa kila upande wa jamuhuri ya muungano kina wabunge, hichi chama toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kinaitesa ccm.

Hichi chama hakina mmiliki, zaidi ni viongozi, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
 
Tatizo ninyi wenye vichwa vyepesi hamuwezi kufikiri kwa ku-extrapolate matukio.
Mbowe aliambiwa ajichunge sana asigombane na dola akabisha, aasema yeye na UKUTA na UKUTA ni yeye.
Sasa kakumbushwa deni lake la nyumba na kufungishwa virago.
Amekuwa mpole na mdogo kama piritoni.

Maalim siku zake zinahesabiwa , hata mkono hatoi kwa wanaombeba, CUF ni yeye na yeye ni CUF.
Lazima kuna jambo atakumbushwa muda si mrefu.
Kuiba ushindi wa Seif mara tano kunahitaji vichwa vinavyoweza kufikiri kwa matukio?

Kwa nini CCM iibe ushindi wa CUF? Kwa nini CCM ilazimishe kung'ang'ania madaraka?
Wewe Jidu na CCM yenu mnajifanya mbuni lakini kila mtoto, kijana, mzee, Afrika na dunia inajua CCM ilishindwa uchaguzi wa 25 oktoba,2015.
Hizi kitu mnafanya ni kujaribu kumrubuni ili akubali kushindwa. This time amewagomea na kwa kweli inaeleweka kwa nini mmekuwa mbogo. Mna hasira kweli, mnapanga mengi.

Link Moyo: Nilitumwa kumshawishi Seif akubali matokeo 2010

Link CUF: Maalim Seif akishinda urais hatakubali matokeo Zanzibar
 
Pumba tupu, cuf ina sifa kuliko vyama vyote vya kisiasa, sifa kubwa na kuwa kila upande wa jamuhuri ya muungano kina wabunge, hichi chama toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kinaitesa ccm.

Hichi chama hakina mmiliki, zaidi ni viongozi, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
Imekuingia sawia kamanda!
 
Wahenga walisema masaa 24 katika siasa ni muda mrefu sana.

Lakini katika siku na wiki za hivi karibuni tumeshuhudia jinsi CUF inavyozidi kudidimia na kukosa sura ya kuitwa chama cha siasa chenye ushawishi nchi nzima. Kitendo cha CUF-Zanzibar kuwa na mgongano mkubwa na CUF-Tanganyika knaanza kuleta sura isiyotegemewa katika chama hicho.

CUF-Zanzibar mhimili wake ni katika ungozi wa Maalim Seif na wafuasi wake ambao hawasikii la muidhini wala shehe mwingine. CUF-Tanganyika inaanza kuonekana ina ongozwa na Prof Lipumba. Jaribio la CUF -Zanzibar kumweka Mtatiro, ambaye anaonekana kuwakibaraka wao, linaelekea kuwa limegonga mwamba.

Sioni jinsi CUF kuendelea kuwa chama cha kitaifa, bali pengine kuwa vyama viwili katika kila upande wa muungano.

Naomba kuwasilisha.
Uongo huu ndio ulikuwa njama zenu , na mmeshindwa kudadeki !
 
kiukweli mgogoro wa cuf umetengenezwa na mfumo kwa maana system. kwa maoni yangu chanzo cha mgogoro huu ni msajiri wa vyama vya siasa....
 
CUF inavyozidi kudidimia na kukosa sura ya kuitwa chama cha siasa chenye ushawishi nchi nzima.
Sio CUF tu hata CCM kimekosa kukubalika Pemba bila mgogoro na hakina ushawishi wa demokrasia Pemba na hivyo kukosa kuitwa chama cha siasa nchi nzima.
Sioni jinsi CUF kuendelea kuwa chama cha kitaifa, bali pengine kuwa vyama viwili katika kila upande wa muungano.
CUF ni taasisi sio Seif wal Lipumba, wote hao watapita na kuondoka lakini chama cha CUF kitaendelea kuwa chama ch kitaifa kama ilivyo sasa ambavyo kina safu kamili ya uongozi kitaifa.Mbona hukiiti CCM ni chama cha bara kwa vile mgombea wao wa urais SMT kila siku anabwgwa na CUF Zanzibar?
 
Pumba tupu, cuf ina sifa kuliko vyama vyote vya kisiasa, sifa kubwa na kuwa kila upande wa jamuhuri ya muungano kina wabunge, hichi chama toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kinaitesa ccm.

Hichi chama hakina mmiliki, zaidi ni viongozi, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
Kinachomuumiza Maalim Seif ni madaraka. Tangia alipobwagwa na Hayati Abdulwakil kule Dodoma basi hajawahi kurudi kuwa sawa. Maalim aliamini kwamba baada ya Mwinyi kule Zanzibar ni yeye lakini watu wakamuona hafai wampa Abdulwakil.
 
Kwa sie tunaoijua historia ya CUF, tunaelewa Masopakyindi na Kimbunga wanachoeleza na kutaadharisha.

Kwa wewe unayeijua CUF ya Mtatiro tu, una haki ya kubisha.
Muache aendelee kujifariji wakati hajui chochote. Hajui chimbuko la CUF
 
Kwa mbali ninaona shoka iliyonolewa sana ikiegeshwa kwenye mizizi ya CUF.
 
Kwa sie tunaoijua historia ya CUF, tunaelewa Masopakyindi na Kimbunga wanachoeleza na kutaadharisha.

Kwa wewe unayeijua CUF ya Mtatiro tu, una haki ya kubisha.
Unajua historia ya CUF kwa kuisoma halafu unajisifu..endelea kujivukiza ubani utoe gundu
 
Hizi porojo tupu., si lazima kuja hapa na kuandika chochote kama hakileti mantiki yeyote., CUF gani bara na Tanganyika inamuunga mkono Lipumba zaidi ya Abdalla Kambaya? Sekaya? yale mengine ni mapandikizi ya CCM huvalishwa sura ya CUF., huoni Lipumba amefungiwa ndani anapewa hadi ulinzi na jamuhuri??

Uchochezi mtupu ulioandika hapa., lete maneno yenye mashiko CUF ni taasisi na ipo imara zaidi, CUF sasaiv ndio inapaa zaidi na zaidi Tz.,
sababu ya Prof. Lipumba kujiuzulu hii hapa. hayo mengine ni porojo tu. huu ni ushahidi sa Seif na Lipumba mwenyewe.

ushahidi kutoka seif uliopelekea hata kuzomewa na wana-CUF



Ushahidi kutoka kwa Lipumba



ukweli daima utatuweka huru.
 
Wahenga walisema masaa 24 katika siasa ni muda mrefu sana.

Lakini katika siku na wiki za hivi karibuni tumeshuhudia jinsi CUF inavyozidi kudidimia na kukosa sura ya kuitwa chama cha siasa chenye ushawishi nchi nzima. Kitendo cha CUF-Zanzibar kuwa na mgongano mkubwa na CUF-Tanganyika knaanza kuleta sura isiyotegemewa katika chama hicho.

CUF-Zanzibar mhimili wake ni katika ungozi wa Maalim Seif na wafuasi wake ambao hawasikii la muidhini wala shehe mwingine. CUF-Tanganyika inaanza kuonekana ina ongozwa na Prof Lipumba. Jaribio la CUF -Zanzibar kumweka Mtatiro, ambaye anaonekana kuwakibaraka wao, linaelekea kuwa limegonga mwamba.

Sioni jinsi CUF kuendelea kuwa chama cha kitaifa, bali pengine kuwa vyama viwili katika kila upande wa muungano.

Naomba kuwasilisha.
Kama walivyotaka serikali tatu na muungano wa mkataba, dhambi ya ubaguzi haitawaacha!Chama chao nacho kinaanza kuwa cha vyama ofisi tatu na cha mkataba
 
kiukweli mgogoro wa cuf umetengenezwa na mfumo kwa maana system. kwa maoni yangu chanzo cha mgogoro huu ni msajiri wa vyama vya siasa....
Msajili anapokea maagizo tu, wachoraji wa ramani ni wale ving'ang'anizi wa madaraka wa nchi hii. Chama cha kuwagawia umasikini wadanganyika.
 
Kuiba ushindi wa Seif mara tano kunahitaji vichwa vinavyoweza kufikiri kwa matukio?

Kwa nini CCM iibe ushindi wa CUF? Kwa nini CCM ilazimishe kung'ang'ania madaraka?
Wewe Jidu na CCM yenu mnajifanya mbuni lakini kila mtoto, kijana, mzee, Afrika na dunia inajua CCM ilishindwa uchaguzi wa 25 oktoba,2015.
Hizi kitu mnafanya ni kujaribu kumrubuni ili akubali kushindwa. This time amewagomea na kwa kweli inaeleweka kwa nini mmekuwa mbogo. Mna hasira kweli, mnapanga mengi.

Link Moyo: Nilitumwa kumshawishi Seif akubali matokeo 2010

Link CUF: Maalim Seif akishinda urais hatakubali matokeo Zanzibar
Ya Jecha mwachie Jecha!
 
Back
Top Bottom