Jagermaster
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 654
- 321
.....!!!!!!!!!!!!????????????? tuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu CUF, moja kubwa, si wapinzani kweli kweli, CCM B, hii ipo waziii,
they are not serious with opposition, BUT, BUT, BUT, let us allow Mbowe & CDM wawaruhusu waingie upinzani, no problem, wakubali ombi la Rashid
we will monitor them with magnified lenses Microscope, wakiwa hawaeleweki, as usual makamanda wa CDM FUKUZA CUF no discussions
Makokoto kweli mpo wengi. Mwenyewe unaikubali UD eeh? Usiposoma pale basi wewe sio msomi. Kaah!
Makokoto kweli mpo wengi. Mwenyewe unaikubali UD eeh? Usiposoma pale basi wewe sio msomi. Kaah![/QUOTE
RANKING UNIVERSITY IN AFRICA TOP 100.
13.UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
90. SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE 4 International Colleges & Universities | World Universities Web Ranking
kama Tanzania kwenye vyuo 100 bora Africa tuna vyuo wiwili tu unadhani wasomi wapo tanzania? mnasoma vyuo vya kata mnataka muitwe wasomi waliofanya utafiti wakaweka Ranking Tanzania tukapewa vyuo viwili sio wajinga wanaosoma hivyo vyuo ni wasomi, wewe unasoma Journalism pale Ilala unataka tukuite msomi..kweli makokoto wapo wengi na vyuo vyao vya KATA
Kwa taarifa yako Graduate wa UD na SUA wananafasi kubwa ya kupata International Scholarship nyingi zaidi ya hivyo vyuo vingine vilivyoko huko Tanzania. We speaking through experience. Ni ukweli usipingika kuwa cream ya form six kwa asilimia kubwa imekuwa ikienda, UD, SUA na MZUMBE kwa muda mrefu labda miaka ya sasa baada ya kuongezeka idadi ya wanafunzi na vyuo vya kata
Hivi kanuni zinasemaje kuhusu kuwafukuza wakionekana wanaasi, maana kisije kikawa kitanzi kwa CDM kwamba labda mpaka maamuzi ya Spika. Spika akikataa kwamba hakuna kufukuzwa basi wanaweza kubaki milele. Nakumbuka incidence ya Cheyo mpaka Speaker Sita alivyoitolea ufafanuzi kuwa jamaa amekyuka ndio alitemwa kama waziri kivuri baada ya kuunga bajeti ya ccm. Lakini pia ilifuatana na hekima na maono ya Speaker Sita. Hebu kumbuka mwaka 2005 Mrema alitangaza kumtema uanachama wa TLP bwana Ngawaiya, na kwa kanuni ilipaswa atemwe na Ubunge pia, lakini Speaker wa wakati huo, mzee Msekwa alikataa na akipangana na kanuni za bunge na Ngawaiya aliendelea kuwa Mbunge. Sasa hilo pia la kuliangalia kwa watalaam wa Sheria na huyu Speaker kuwadi wa Mafisadi Anna Makinda, kinaweza kuwa kitanzi kwa Chadema. Kuwa katika Safe side ni kuwakataa kabisa
Wapinzani wamsihi Mbowe
Kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni imemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuomba wachaguliwe kuunda Baraza la Mwaziri Kivuli kwenye Bunge ili waweze kushirikiana kwa dhati kama kambi ya upinzani.
Katika barua ya kambi hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Rashid na katibu wake David Kafulila kwenda kwa Mwenyekiti wa Chadema wamesema wanaomba ushirikiano huo uanze kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza Februari mwaka huu.
Kambi hiyo ilimsihi Mbowe kuunda kambi ya upinzani imara ikishirikisha vyama vyote vya upinzani ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni na kuibana serikali ya CCM kwa pamoja.
Vyama vilivyotoa ombi hilo ni CUF chenye wabunge 33, NCCR Mageuzi chenye wabunge wanne, TLP mbunge mmoja na UDP mbunge mmoja wakati Chadema kikiwa na wabunge 47.
Chadema ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimeunda kambi ya upinzani peke yake huku mwenyekiti wake akichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi hiyo na nafasi nyingine za mawaziri kivuli zikijazwa na wabunge wa chama hicho pekee ..
Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.
Mimi naona bora wawakubalie ili wawe na nguvu kumbukeni Caf wapo 33 Cdm 44 hapo namba hizo zikiwa pamoja kwa CCM ni mwiba wa samki mkiwabwaga imekula kwenu watakuwa na CCM
hawana lolote cuf ni wanafiki, mmesahau mnyaa alivyojitoa kugombea unaibu speaker akisema anaendeleza makubaliano ya kuunganisha vyama vyao? Tena kafulila alinukuliwa akisema yalikuwa maamuzi yake labda na chama chake si ya unofficial kambi ya upinzani? Na mnakumbuka jinsi ccm walivyompa kura nyingi mnyaa za ubunge wa sadc? Mi sidanganyiki, wana agenda ya siri hawa cuf na partner zao nccr.mimi naona bora wawakubalie ili wawe na nguvu kumbukeni caf wapo 33 cdm 44 hapo namba hizo zikiwa pamoja kwa ccm ni mwiba wa samki mkiwabwaga imekula kwenu watakuwa na ccm
Jamani hebu CDM wasikilizeni hao na mkiona kuna dalili ya usaliti au mkigundua wametumwa na green guard muwakatilie mbali
Kuna haja ya kuchangamana nao bse lengo ni kujenga nchi sio kubomoa
Jamani, waacheni waje. Kama Hamadi Rashidi au Kafulila wakienda kinyume cha azma ya upinzani si Mbowe anaweza kuwatimua kutoka kwenye Bara Kivuli?
Hamadi Rashidi (mkuu wa kambi wa upinzani bunge lililopita) alisha mtimua John Cheyo wakati wa kikao cha bajeti mwaka jana pale Mbunge huyo wa UDP alipotoa kauli ya kuiunga mkono bajeti kwa asilimia 100![/QUOTE]
mdau hapo kwenye bluu umesahau kwamba cuf ya bunge lilopita sio cuf ya leo...wamefunga ndoa na watawala ccm kumbuka,..anything you discuss with them they will snitch on you...they can't be trusted anymore