CUF sasa dhahiri mambo ni magumu

CUF sasa dhahiri mambo ni magumu

Nimewatazama wale wajumbe wa bodi kupitia ITV, nimewasikiliza pia. Nilichojifunza ni kwamba hivi vyama vya siasa, kwa baadhi ya watu vimegeuka kuwa "vyombo vya kuendeshea" maisha yao. Wale wajumbe, pengine kwa kuelekezwa, wanaugeuza mgogoro uliopo CUF sasa kuwa baina ya CUF bara na CUF Zanzibar. Na ili kunogesha wanamwonyesha Seif kuwa ndiye tatizo. Taasisi zinazoua vyama vya upinzani vinavyosumbua chama tawala huelekeza mashambulizi kwa viongozi BOLD kama ilivyo kwa Seif. Wale wazee kudhihirisha kuwa wanatumika sasa kukimaliza chama, wametumia jukwaa lile kumshambulia Seif tena kwa kutumia hoja zisizoendana na mgogoro uliopo CUF sasa. Kwa hali ilivyo, hawa wazee kama akina Lugeye ndio watatumika kuimaliza kabisa CUF iwe sawa na TLP ya Mrema, UDP ya Cheyo, kile cha Dovutwa; na the like. Sioni kama kuna namna CUF itajinasua katika mbinu hizi za kutumia watu waliochoka!
Baada ya cuf, wanakuja cdm, just weit u ll c...
 
Huu mchezo Lipumba ataibuka mshindi, uzembe wa Maalimu umempa Lipumba uhalali wa Kikatiba.
Busara itumike au wapambane kisheria, ninachokiona ni kwamba kwa upande wa Bara kuna wanachama wengi wanaomuunga mkono Lipumba.
 
Cuf fanyeni upuuzi kwa faida ya wachache, kuweni makini sana na mwenyekiti ampango wa kuua chama na yy hana hofu akifanikiwa tu ana bingo yake lakini ninyi mtabaki mnatoa macho tu, na kibaya mama sakaya imekiwaje mwanamke uliyepigania demokrasia kwa mda mrefu sana! Imekuwaje mama sakaya? au umemfuata kaka yako ambaye alikukimbia ukiwa katibu bara ukabaki peke yako!
 
Huu mchezo Lipumba ataibuka mshindi, uzembe wa Maalimu umempa Lipumba uhalali wa Kikatiba.
Busara itumike au wapambane kisheria, ninachokiona ni kwamba kwa upande wa Bara kuna wanachama wengi wanaomuunga mkono Lipumba.
Maalim Seif kesha chuja!
Kacheza namba ile ile miaka yote na sasa hsta wana CUF wanamwita Sultani wa CUF!

Muda umefika akalee wajukuu na kuandika memoirs zake.
Ni lazima atambue uzee umemfika na afya hamuungi mkono vile vile.
Kustaafu ukiwa na akili timamu ni heshima .
 
Tatizo la Mwalimu Sefu ni kuhadaa watu kuitisha Kikao cha Marafiki zake Zanzibar na kusema wamemfukuza Mwenykt wa Chama chake ambae pia ni Boss wake

Tatizo la Sefu ni kuupeleka Mgogoro wa CUF kwa Freeman Mbowe na kudai eti hawamtambui Prof.

Utakuwa umeelewa uhusiano wa Seif na Mapinduzi yaliyoshindwa ndani ya CUF
Utamfukuza mtu aliejiuzulu? Mbona hueleweki?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom