CUF sasa dhahiri mambo ni magumu

CUF sasa dhahiri mambo ni magumu

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,410
Reaction score
14,119
Wajumbe wa bodi ya wadhamini toka Bara wameonyesha kutokubaliana kabisa na msimamo wa upande wa pili unaopingana na Mwenyekiti wa CUF, Prof Lipumba.

Kulingana na habari za ITV saa mbili, mtanange unaoonyesha kuwa Bodi ya wadhamini imegawanyika kabisa, huku wajumbe toka bara wakisema mambo kutoka kwa Maalim, enough is enough.

Upande unaolalamikiwa kwa ukiukwaji wa taratibu ndani ya chama cha CUF, ni ule unaoongozwa na Maalim Seif. Mjumbe mmoja ameenda mbali zaidi na kudai tatizo ni usultani wa Katibu wa chama Maalim Seif.

Mjumbe huyo amedai Maalim amekuwa akijilimbikizia madaraka na hatimae kuwafukuza wanachama waanzilishi kama James Mapalala, Mzee Mloo na hata Hamad Rashid.

Mjumbe huyo akimfananisha Maalim na Napoleon aliyeshinda vita nyingi na hatimaye kuzidiwa nguvu katika mji wa Waterloo huko Ulaya, mjumbe huyo kasema Maalim sasa kafika Waterloo yake. Hapa ndo kafika.

Mjumbe mwingine amesema vikao vilivyoitishwa kinyemela huko Zanzibar bila kushirikisha wajumbe toka Bara ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za chama.

Sinema inaendelea.
 
Basi kama mbwai na iwe bwai tu tumechoka na hizi drama
 
Hao wajumbe hawana majina. Mbona hawajatajwa? Tunachojua sisi ni kwamba wajumbe wote 9 wa bodi ya wadhamini wakiongozwa na mwenyekiti, Mh. Khatau toka wilayani Masasi, walikuwepo kwenye kikao kilichofanyika Zanzibar hiyo juzi.
 
Uliwekwa uzi hapa kuhusu hili mkadai ni uzishi, haya sasa!! Watano kati ya tisa wamekataa kikao hicho cha zanzibar na hawamtaki Seif.
Kweli mkuu asante sana kwa kunote hilo.
Tatizo kubwa wana JF wengi wanakosa kuwa analytical katika matukio kama haya.
Na huu si ushabiki bali extrapolation ya events na matokeo yake katika jamii.
 
Hao wajumbe hawana majina. Mbona hawajatajwa? Tunachojua sisi ni kwamba wajumbe wote 9 wa bodi ya wadhamini wakiongozwa na mwenyekiti, Mh. Khatau toka wilayani Masasi, walikuwepo kwenye kikao kilichofanyika Zanzibar hiyo juzi.
Kijana endelea kubishana na redio.
 
Tatizo la cuf ni kukosa umoja sio kama chadema wakiamua na iwe moja wote inakuwa moja hakuna kurudi nyuma na kugawanyika
 
Kuna watu walipumbazwa na vile vi Press conference uchwara vya haraka haraka vya Kina Mtatiro na Mbowe wakadanganywa eti Prof yupo na kundi la wahuni tu!

Wakili Mkongwe Mzee Twaha Issa Taslima kaona Maji Marefu kakabidhi Uongozi hewa wa Muda kwa Julius Mtatiro nae kaingia kichwa kichwa akadhani kuongea kwa sauti ya Juu na kufoka fola kwny Mikutano ndio ushindi. Taratibu watu Wataanza kuelewa kuwa Siasa ni Sio kitu cha Mchezo mchezo na kosa kubwa kwny Siasa ni kubeza nguvu ya adui
 
Wajumbe wa bodi ya wadhamini toka Bara wameonyesha kutokubaliana kabisa na msimamo wa upande wa pili unaopingana na Mwenyekiti wa CUF, Prof Lipumba.

Kulingana na habari za ITV saa mbili, mtanange unaoonyesha kuwa Bodi ya wadhamini imegawanyika kabisa, huku wajumbe toka bara wakisema mambo kutoka kwa Maalim, enough is enough.

Upande unaolalamikiwa kwa ukiukwaji wa taratibu ndani ya chama cha CUF, ni ule unaoongozwa na Maalim Seif. Mjumbe mmoja ameenda mbali zaidi na kudai tatizo ni usultani wa Katibu wa chama Maalim Seif.

Mjumbe huyo amedai Maalim amekuwa akijilimbikizia madaraka na hatimae kuwafukuza wanachama waanzilishi kama James Mapalala, Mzee Mloo na hata Hamad Rashid.

Mjumbe huyo akimfananisha Maalim na Napoleon aliyeshinda vita nyingi na hatimaye kuzidiwa nguvu katika mji wa Waterloo huko Ulaya, mjumbe huyo kasema Maalim sasa kafika Waterloo yake. Hapa ndo kafika.

Mjumbe mwingine amesema vikao vilivyoitishwa kinyemela huko Zanzibar bila kushirikisha wajumbe toka Bara ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za chama.

Sinema inaendelea.

3683b3a3dd9e95ad27592fb24e69cf2f.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom