CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

utakuwa umevurugwa wewe! Jazba za kijinga kabisa!

Kwa nini usijibu hoja ya mtu aliyevurugwa? Nimeuliza hivi : TANGU CHAMA CHENU CHA KILIBERALI KILIPOANZISHWA KUNA MTU ZAIDI YA SULTANI AMBAYE AMEPATA FURSA YA KUGOMBEA URAIS?
 
Ndugu zangu leo katika viwanja vya
K.ndege mjini morogoro mh.Slaa na
John Heche ndio waliohutubia mkutano
huo kuanzia muda wa saa 9:30.
wakwanza kuhutubia alikuwa John
Heche kaelezea jinsi rasilimali za taifa
zisivyo wanufaisha watanzania,
Baadae Slaa alianza kuhutubia na
alijikita kuelezea suala la amani nchi
kwa kuwaeleza wananchi wasikubali
kudanganywa kuwa tanzania inaamani
na kuongeza kuwa vijana ndio chachu
ya mabadiliko na hivyo wasihofie amani
kuvunjika na kuongeza kuwa bora
ivunjike na lolote liwe,huku
akiwashawishi vijana kuwa hawana cha
kupoteza kutokana na maisha magumu
na ukosefu wa ajira.slaa kaongea kwa
jazba za hali ya juu huku akimtuhum
afisa usalama aitwaye zoka kwa
kuihujumu chadema. Pia amemtuhum
sana Rais Kikwete kwa kuonyesha
kuwa yeye ndio chanzo cha haya yote
na kuwataka wananchi kufanya maisha
magumu.
Baada ya Slaa kumaliza kuhutubia alitoa
muda wa kuulizwa maswali
kadhaa.Kijana mmoja alijitoa muhanga
akauliza"CHADEMA MMEITUHUMU CUF
KUWA INAUNGA MKO USHOGA KWA
SABABU INAMLENGO WA KILIBERAL.
NA CHADEMA NI CHAMA RAFIKI WA
CHAMA CHA CHRISTIAN DEMOCRATIC
UNION (CDU) CHA UJERUMANI
AMBACHO KINACHOFUATA MISINGI YA
KIKRISTO,JE?CHADEMA NI CHAMA CHA
KIKRISTO? baada ya kuuliza swali hili
watu wote walikaa kimya!!!kusubiri jibu
la dr.slaa,kiukweli slaa akasema kuwa
ujerumani ni nchi ya kikristo hivyo naye
akauliza"we ulitaka kuwe na chama cha
kiislam katika nchi ya kikristo?baadae
akaishia kumshambulia muuliza swali
badala ya kujibu swali.
Aliharibu hutuba nzima maana watu
wameondoka wskiwa na mjadala
mkubwa juu ya slaa kushindwa kutoa
majibu juu ya swali lililoulizwa.
My take:siasa hazihitaji mtu mwenye
jazba kama mzee wetu slaa.maana
huyu ni hatari kwa mustakabali wa Taifa
hasa anapotumia umaskini wetu kuwa
hoja ya uvunjaji wa amani."TAIFA LETU
NI ZAIDI YA VYAMA ,DINI NA
MAKABILA YETU"
Adha za ukimbizi nimezishuhudia kwa
macho katika makambi kadhaa ya
NYARUGUSU,RUGUFU,MTABILA NA
KANEMBWA,mkoani kigoma. pamoja na
umaskini wetu watu wa kigoma
wanaheshimiwa na wakimbizi kama
amvavyo wstanzania
tunavyowaheshimu wazungu. Watu
maskini wa kigoma ndio waajiri wa
wakimbizi mashambani.utu wa
wakimbizi umeshapotea na wanatamani
kama wangezaliwa tanzania.
TUENDELEE KUDAI HAKI NA
MABADILIKO YA TAIFA LETU LKN
AMANI YETU NDIO JAMBO
TUNALOJIVUNIA MBELE YA WENZETU.
tumpuuze kibaraja yeyofe atakaechezea
amani ya watanzania. Tumeshajifunza
LIBYA"BURUNDI,SOMALIA,RWANDA,AN
SYRIA.
Vita vikitokea
Slaa,Mbowe,Lipumba,Kikete na familia
zao watakuws ulaya na Amerika na
watatuacha tukifa kama nzige huku
wakitutazama kwenye TV.
MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Just now
 
Eti atawajaza watz hela kupitia mitandao ya simu!
Dah,nimecheka sana!
BACK TO TOPIC:
Anafaa sana kuongoza watu wa Mombasa!
Inapaswa kuwa atawajaza "waislamu" hela kupitia mitandao ya simu.Au mnafikiri vision and mission za CUF zimebadilika?THUBUTUUU!!!!
 
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemnadi Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kugombea kwa mara nyingine kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, huku yeye binafsi akitangaza neema kwa Watanzania ya kuwajaza fedha mifukoni.



Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF.



Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera, uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.



Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya kwenda kuhutubia.



Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.



Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.



Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2 imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).



Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.



NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria.

Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka
[h=2]Ukweli Kuhusu Mabadiliko ya Sera Ndani ya CUF na Ushoga!!!!!!!!!!![/h]
Nakumbuka Mwaka 2009 April Chama Cha CUF Kiliitisha mkutano mkuu wa mabadiliko ya Katiba na Sera. Mkutano huo ambao ulikuwa na agenda za uchaguzi Mkuu ambapo Prof Lipumba kupitia idara ya Blue Gad alimufanyia Umafia Prof Safari ili asipate nafasi ya Mwenyekiti Taifa kwa Kumuundia zengwe na kumuwinda kama mhalifu.

Kufuatia kampeni hizo Chafu Prof Safari alimuhoji Lipumba kuhusu mkewe kuwa mbano hatumuoni kwenye chama??
Lipumba akasema mke wake anafanya kazi UN ambapo hawatakiwi kujihusisha na Mambo ya Siasa.
Pili Sfari alihoji ni kwa nini CUF viongozi wake wengi katika nafasi za Juu ni waislamu hata katika majimbo yenye Wakristo wengi??. Pia alihoji ni kwa nini CUF haina hata moja???. Pia alihoji kwa nini CUF ibakie ZNZ pekee wakati wapo waasisi bara???

Kura zilipigwa Safari akaambulia kura sita (6).

Kwenye Uchaguzi huo Julias Mtatiro aliletwa na Seif kama Mwangalizi wa Uchaguzi na kusimamia uchaguzi huo wakati si Mwanachama . Na baadaye ikaja kuonekana walikuwa na Lengo la kumuanda Mkristo kuchukua nafasi ya Naibu katibu mkuu bara baada ya kutengeneza njama za kumutimua Wilfred Lwakatare.

Kabla ya mabadiliko ya sera CUF ilikuwa ina amini katika Utajirisho na Mwaasisi wa sera hii ni marehemu Shabani Khamis Mloo .
Muasisi wa sera ya uliberali ni Maalim Seif na alimtumia Imail Jussa mtu wa karibu na Julius Mtatiro kuleta mabadiliko ya katiba .
Watu ambao walikuwa wanapinga sera hiyo ni pamoja na prof Safari , Marehemu Shabani Mloo,Mhe Masoud na idara ya Blue Gad .
Kwenye mjadala wa kupitisha katiba hiyo Seif na Lipumba walikuwa kitu kimoja huku Hamadi Rashid akiwazunguka.
Marehemu Mloo alipinga hadi akatoa machozi na baada ya tukio hilo Masoud ambaye alikuwa mkurungenzi wa blue gad Taifa naye aliumia sana kwa hakutaka Ulibelali na kufanya mkakati wa kupinga kwa nguvu zote.

Aliwapanga vijana wa blue gadi wakiongozwa na desk officer Mzee Wandwi. Kazi hiyo ilipo anza , Maalimu seif alipata taarifa na kumutuma Jussa kumushughurikia Wandwi.
Jussa alikwenda kumutukana Mzee Wandwi kwa kumwita Mbwaa!!!

Baada ya Mzee Wandi kutukana Mbwaa alikasirika sana ndipo Mzee Saidi Miraji ambaye akaingilia kati na kuweka msimamo kuwa ulibelali haufahamiki vizuri hivyo sio vema kuiga mambo ya kigeni kwa kuwa yanaweza kupotosha taswira ya chama.

Prof Lipumba alimpinga Mzee Saidi Miraji na mpasukoa ukawa mkubwa. Mpasuko huu ni sehemu ya chanzo cha baadhi ya watu kuunda chama kingine cha ADC.


NB:
Mimi nimeshangaa sana Mhe Masoudi kumushambulia Wenje wakati hata yeye alipinga sera hiyo ndani ya CUF . Mimi nawashauli CUF waitishe Mkutano mkuu Taifa na kujadili suala hilo tena
CUF inaburuzwa na Maalimu Seif na ni chama cha Wapemba na sakata la Ushoga lina mkono wa Seif. Nawaomba CUF kama wana ujasiri wapinge maneno haya. pia namtaka mtatiro aje humu atoe mchango wake hapa!!!
Nawaomba waandishi nenda kawahoji niliowataja ili ukweli ujulikana ndani ya CUF sera ya Ushaga ipo lakini hawakujua!!




SEHEMU YA TAARIFA YA WENJE


3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ‘United Nations University'(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania ‘Donor Assistance and Political Reform in Tanzania', inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.

Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada hiyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.

Mheshimiwa Spika, CCM wao ‘wanajiita' kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni ‘Socialist International' kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na "kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga". Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.

Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: "tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji". Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .​
 
Mliberali huyu wanini siye, tena mdini. Akaoe kwanza, labda tutamuelewa.
Hivi huyu mliberali 'mzee wa tigo'hana mke?Kati ya viongozi wasio na busara katika jamii ni huyu prof mchumi-udini Lpumba.2010 alimfanyia kampeni Kikwete,kwa sababu ya udini.Amekosa credibility ya kuwa kiongozi.
 
Baada ya kuangalia kwa macho yangu video inayoonyesha udini wa Prof. Lipumba, nasema na naomba watanzania wote tumpe kisogo huyu mgombea kwa 100%, ni MDINI HAFAI KUWA KIONGOZI hata wa serikali ya mtaa.
 
hivi cuf si chama cha wapemba?hao kina sharif hamad si ndio wanashadadia muungano uvunjike?au wanataka baada ya muungano kuvunjika watawale na huku tanganyika?au me ndio sijaelewa hapa may be wanazungumzia rais wa jamhuri ya pemba!!!!
 
Mkuu, SadamHussein nanukuu: Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bi lioni (USD5 milioni) kwa mwaka
Mwenyekiti wa chama mbona anatuelezea pato dogo sana hizo USD 4 million mpaka USD 5 milioni ni ndogo sana au hakusoma mkataba vizuri kama vile alivyosaini mkataba wa ki-liberali?
 
Rais wa mashoga........ mwenzake seif kaolewa ccm ...
 
Back
Top Bottom