CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemnadi Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kugombea kwa mara nyingine kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, huku yeye binafsi akitangaza neema kwa Watanzania ya kuwajaza fedha mifukoni.



Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF.



Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera, uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.



Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya kwenda kuhutubia.



Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.



Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.



Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2 imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).



Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.



NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria.

Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka
 
Wetu na nani? Huyo ni rais wako labda alete u cuf nan anataka
 
Labda anaweza kuwa Rais wa Bakwata sio wa Tanzania, nendeni mkajipange tena.
 
Huyo atufai mamluki wa ccm labda raisi wa cuf sio raisi wawa tanzania
 
huyu prof nlimwamini sana, ila ameni discourage sana sasa sisi ambao tuko familia moja mrengo wa kiimani tofauti si anataka kutuletea matatizo.
 
Huyu ndie kiongozi makini kwa sasa tanzania na international community wanamjua
 
Mliberali huyu wanini siye, tena mdini. Akaoe kwanza, labda tutamuelewa.
 
kizuri chajiuza kibaya chajitembeza he is a good economist yes world class but not a good leader at all
 
Hivi ktk waliberali Lipumba na Maalim nani ni consevative kidogo?tunaweza guess toka ktk viburi vyao.ila ni vyema mkatueleza hata kwa jazba tuu km bungeni.
 
Hivi lipumba nae ni mpinzani!??
Na waziri mkuu atakuwa nani PONDA, ilunga au sheikh Basalleh
 
Pro. Lipumba tunakuamini, tunakukubali, nafikiri ni mtu sahihi kugombea kwa sasa! big up cuf!
 
KIUKWE HAMNA MWENYE SIFA KAMA PRF.LIPUMBA,SIYO YULE MWENYE PhD ya kwaya.
 
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]
Hivi lipumba nae ni mpinzani!??
Na waziri mkuu atakuwa nani PONDA, ilunga au sheikh Basalleh

mkuu remote hiyo list ya uongozi unataka ituchezeshe ngoma kama hiyo tunayoiona hapo kwenye hiyo picha uliyoweka hapo, mbona itakuwa songombingo.
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Huu ulikuwa ni muda mzuri kama Pr Lipumba angekaa pembeni kuwapisha wengine naamiini wangepatikana tu.Lakini kuendelea kuwa mgombea uraisi kunafanya tujiulize maswli mengi sana kuliko majibu kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Weupe wenyewe wanamtumia ktk UCHUMI,wanamwita USA na ULAYA,kweli mfalme atambi kwao!!! angekuwa mkristo sasa hivi RAISI.
 
Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF.

Ina maana Maalim Seif Leo alikuwa pia Morogoro.
Huyu si leo alikuwa Zanzibar Kibanda Maiti wakidai Zanzibar Huru, yanini tena Kuja Kwetu tena.
Huyu Mze ni Hasidi wa Siasa for Real
 
Back
Top Bottom