CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

CUF: Profesa Lipumba ndiye rais wetu ajaye

You have made my evening. Kweli nimecheka hadi watu wananishangaaaaaaaa.

But this is very siriaz mkuu, hivi ukipiga fikra pevu, hiki chama kina sehemu kimelenga kufika kweli?

Huyu jamaa na pumba zake akijiweka tena, basi safari hii atapigiwa kura na Mtanzania ambaye alikuwa hajazaliwa wakati anagombea kwa mara ya kwanza. Piga tu hesabu, kijana aliyezaliwa 1996 atakuwa na miaka 19 unapofika mwaka 2015. Hii ina maana kufeli kwa chama kwao sio tatizo
 
Sijawahi kuvutiwa kisiasa na huyu jamaa.

Hata ukiniamsha usingizini hawezi kuwa chaguo langu.
 
Weupe wenyewe wanamtumia ktk UCHUMI,wanamwita USA na ULAYA,kweli mfalme atambi kwao!!! angekuwa mkristo sasa hivi RAISI.

Mbona Wenje ameeleza vizuri tu ni nini Wazungu huwa wanamuitia Lipumba kujadili nae?

Haya ya uchumi ndivyo huwa anawaaga, lkn ukweli ndio ule aliousema Wenje bungeni. Mchumi mwenye akili za kushindwa mara 3 na bado anasimama msikitini kujisifia mimi namtilia mashaka
 
watu wengine nadhani wanazeeka vibaya,mara Zanzibar iwe huru sijui nani kawaambia inatawaliwa?,iwe na mamlaka yake kamili,okey hatukatai sasa kama hiyo ndo sera yake huku Tanganyika anatafuta nini?huyu maalim Seif haeleweki njaa zinamsumbua.aache kuwasumbua wazanzibar bure wakati anacho wapikia hayuko tayari kukila hata yeye.
 
Eti atawajaza watz hela kupitia mitandao ya simu!
Dah,nimecheka sana!
BACK TO TOPIC:
Anafaa sana kuongoza watu wa Mombasa!
 
Huyu anayepiga kampeni msikitini atakuwa Rais wa nani labda Rais wa misikiti.
 
Pro. Lipumba tunakuamini, tunakukubali, nafikiri ni mtu sahihi kugombea kwa sasa! big up cuf!

hatutaki rais anayeshabikia mashoga,yaani mliberali aongeze nchi,aende ulaya au usa ndo maliberali wametamalaki
 
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemnadi Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kugombea kwa mara nyingine kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, huku yeye binafsi akitangaza neema kwa Watanzania ya kuwajaza fedha mifukoni.



Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF.



Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera, uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.



Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya kwenda kuhutubia.



Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.



Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.



Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2 imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).



Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.



NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria.

Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka

Hafai hata ujumbe wa Nyumba moja. Mdini mno
 
Back
Top Bottom