CUF: Ndugai awaombe radhi wapinzani

CUF: Ndugai awaombe radhi wapinzani

gomba

Member
Joined
May 6, 2013
Posts
18
Reaction score
5
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aiombe radhi Kambi ya Upinzani kwa kitendo cha kumtoa ndani ya Bunge kiongozi wa kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe. Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro alisema kitendo hicho ni ukiukaji wa kanuni na sheria za Bunge, na kimeidhalilisha kambi hiyo.

“Tukio lililotokea jana (juzi), si la kawaida, Naibu Spika ni kiongozi wa Bunge lakini wapo watu wakubwa ambao anapaswa kuheshimika sana.

“Kambi ya Upinzani ina kiongozi wake ambaye ni Freeman Mbowe mwenye nafasi kubwa kama aliyonayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

“Tofauti ya Pinda ipo nje ya Bunge wakiwa ndani ya Bunge wote wana heshima ya kufanana.

“Sijui jeuri ya Ndugai imetoka wapi hivi Pinda angekuwa amesimama Naibu Spika angewaamuru askari wa Bunge wamtoe? Ndugai anapaswa kuomba radhi kwa njia ya ustaarabu tu,”alisema Mtatiro.
 
Hawezi kuomba radhi huyo! anajiona anaweza sana kumbe zuzu tu!
 
****** ni mbinafsi, ni wale wanao taka vyeo/uspika kwa KUKANYAGA wengine... hajali maumivu unayo yapata wakati ANAKUKANYAGA............ Yanamwisho na uzuri mambo ya bunge yako recorded. Historia itawahukumu. Kind of people ambao hata kizazi chake kinaweza kataa tumia jina lake sababu ya aibu watakayo kuwa wanapata kipindi hicho....wapo kina Hitler, Mobutu, ........jamaa zao na vizazi vyao wamebadili majina.....shame on him.
 
Ndugai ni Kati ya viongozi wanaojiona Miungu watu, wanasahau kuwa cheo ni dhamana waliyopewa na wananchi.!!
 
Chaajabu upinzani ambao hawana akili eti ndiyo wamepewa fulsa za uongozi ajabu sana.
 
ndugai amelewa madaraka mno
Sio kosa lake jamani ni mtoto wa mtaani bado hali hiyo inamsumbua. Anajaribu kujitutumua ili naye aonekane. Si unajua Kongwa inazalisha ombaomba wengi Tanzania, na kisaikologia ni vigumu kuondoa mabaki ya historia aliyokulia mtu.
 
Chaajabu upinzani ambao hawana akili eti ndiyo wamepewa fulsa za uongozi ajabu sana.

Nina Imani kwa Tanzania Mbowe ni muhimu kuliko Kagame.Kama Kagame anabembelezwa yaishe kwa nini ishindikane kwa Mbowe?.
 
CCM hawajui kama "this fire now is out of control, So they build their world in great confusion
To force on us the devil's illusion.
But the stone that the builder refuse
Shall be the head cornerstone,
And no matter what game they play,
Eh, we got something they could never take away;
We got something they could never take away: " Bob Marley
 
Maccm yatasema mtatiro kanunuliwa kumtetea mbowe. Ccm mmekwisha hadi 2o15 mtaikimbia nchi.
 
Hawezi kuomba radhi huyo! anajiona anaweza sana kumbe zuzu tu!

ningekuwa mchawi nikempatia kichomi cha tumbo mpaka angekoma, simpendi kweli KAMA membe anajionaga anajua kila kitu plus kiburi na dhalau
 
huyu ndugai uongozi alio pewa ni mkubwa unamzidi umri.
 
huyu ndugai kwanza anA matatizo mengi kwanza alinyamazia muongonzo wa kile kimemo cha vitisho.
 
yap,,huo ndio ukweli,,,sasa,,,ikiwa wapo wanaopingana na kauli hio ya mtatiro,,wanapaswa kupitia katiba ipoje,,,
 
2015 mizengo Pinda atakuwa anaongoza kambi rasmi ya upinzani lakini tutamuheshimu na hatutalipiza visasi.
 
Ndugai ni mtovu mkubwa wa nidhamu,na ana upeo mdogo sana,kiufupi ni kilaza,alitia aibu sana kwenye kipima joto ITV alikua na Lisu,ndugai alipwaya sana.
 
Kambi ipi? manake bungeni kuna kambi mbili za upinzani.
 
Back
Top Bottom