CUF nao waanza kuonja machungu ya CCM

CUF nao waanza kuonja machungu ya CCM

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,209
Hawa ndugu zetu wa CUF huwa wanajidai wanaiponda CHADEMA na kuitetea CCM. Naona sasa na wao CCM imewageuka. It appears harakati za CCM kuumaliza upinzani nchini ni dhahiri. Uwezo wa akina Pinda kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha matatizo ni mdogo kupita kiasi. Sasa kila kitu ni ubabe tu. Msome Mtatiro hapa chini.

Julius S. Mtatiro

NI MATESO, DHULUMA NA UKATILI MTWARA.

Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF - Shaweji Mketo ameyekwa na wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.

Mketo alienda Mtwara MJINI jana na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.

Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama aliofanyiwa.

Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.

Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga 0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya nguoni na kebehi za Hali ya juu.

Tumefanya juhudi za kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa hajawashikilia viongozi wetu. Nimemjulisha kama wako mikononi mwa wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza Hali ya hatari Mtwara??

Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.

Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya mateso makali ya wanyama hawa.

Tunaposema kuwa nchi hii kuna siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.

Tunaendelea kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii unapotezwa kwa faida za watu wachache.

Vyombo vya HABARI hivi sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu wasio na hatia kama siyo mimi na wewe?

Mawakili wetu pamoja na mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759.

 
Hili jeshi linalotumika hivi leo kuwatesa na kuwanyanyasa wananchi namna hii ndiyo hilohilo litageuka na kuwanyonga hawa akina Pinda na Kikwete na kuwaburuza barabarani kama vifurushi vya mchanga. Ni wanajeshi hawa hawa ambao leo wanaonekana waaminifu kwa Kikwete na kukubali kutumiwa vibaya kama wanavyofanya sasa; kufanya kazi za polisi, ndiyo watageuka na kuwanyonga hawa wanaowatumia.

Sina imani na sitawahi kuwa na imani na jeshi la wananchi. Hawa binadamu ni vigeugeu kupita kiasi. Haitashangaza kama wakiamua kugeuka ghafla na kuipindua serikali. Ni vizuri sana akina Kikwete wakajiangalia namna wanavyowatumia hawa watu ambao hawakuwahi kupata mafunzo yoyote ya kudeal na raia bali walipewa mafunzo ya kuua. Unawezaje kumkamata na kumtesa raia kama vile ni mateka wa vita? Tanzanians lets say no to this.

Naungana na Mtatiro kuupinga na kuulaani kwa nguvu zote uonezi na ukatili huu unaofanywa na serikali hii ya Kikwete dhidi ya raia wa Tanzania.
 
poleni sana ccm b. mlidhani ndoa na hao jamaa ingewasaidia kumbe wanawagusa na minuit.! ni heri mkawaomba radhi watz na mkaamua kufanya siasa za utetezi kushirikiana na wenzenu kuliko kujikomba kwa wauaji hawa wasioaminika. wanawatumia kama kondomu kisha qanawatelekeza. ccm watu?
 
Mtwara kuna mateso ya ajabu na vyombo vyote vya habari vimepigwa bonge la mkwara kutoripoti issue yeyote ile lasivyo chombo chao kitafungiwa. Mtwara pamekuwa Kama Syria
 
Kwanini uambiwe umiza mtanzania mwenzako nawe kama zuzu ukubali? Majeshi yetu yanatumiwa vibaya sana na serikali ya CCM.

Wakati unakuja wananchi watasema hapana, hapo ndipo machafuko yatatokea na uasi wa wananchi dhidi ya serikali yao.

ENOUGH !!!
 
Haya mambo huwezi yapata nchi yoyote inayoongozwa kwa utawala wa sheria, ni Tanzania tu!! Hata lini tutaendelea kuteseka hivi, nchi yetu tunaishi kama wakimbizi sasa!! Tunakoelekea Syria itakuwa chamtoto...!! Uoga wetu, upole wetu unafika kikomo sasa!!
 
Ndugu wana JF,

Mapenzi ni kikohozi hata ungeficha vipi litajulikana tu. Tarehe 25/6/2014 kamanda Jobs kwa mbwembwe zake alisitisha maandamano kwasababu rukuki na akaenda mbali Saudi kwa kukemea kwa taasisi na vyama vya soda Fulani vilivyopanga kunyenyua mabango wakati waujio wa Rais Obama. Bila yoyote hapa alikuwa anazisema taasisi za kiraia na CHADEMA.

Kama haitoshi akasema CUF wamekuwa wastaarabu kwani wameandika barua ikulu halo wamekataliwa nakwamba barua yao hiyo ameletewa yeye kutoka Ikulu na yeye amewaandikia CUF. Pasipo kujali Kama watu tunajua mahusiano ya CCM na CUF, kamanda Kova alikisifia CUF kwa uzaledo wake.

Kiuhalisia hapa kamanda Kova amewahadaa wageni wa Rais Bush na taasisi za kiraia za kimataifa ambapo pamoja na mambo mengine zingeibana serikali kwa kutofuata utawala wa sheria na kuvibana vyama siasa bass CHADEMA ambacho kimeonyesha dies uelewa wa kanuni za utawala wa sheria. Katika kuwepa hili, serikali ya CCM kwa kupitia kinywa cha Kova a viongozi wa CUF imeamua kuficha ndoa yao kwakisingizio kuwa sio CHADEMA pekee bali hata vyama vingine vimekuwa vikifanyiwa hivyo na ushahidi jai barua hizo.

Kwa maana hiyo basi CCM wamewashawishi CUF kuandika barua ya maandamano Huku wakijua kuwa haitakubalika.
Wana JF mnalionaje hili.
 
CCM nchi imewashinda na Pinda amekiri wamechoka kilicho baki ni kupiga tuu.wanajeshi na polisi ni kaa mbwa wasio na mafunzo.
 
Mi siamini kama hali ipo hivyo!suala la kutesa watuhumiwa wa uhalifu sio geni Tanzania.Wapo wengi wameteswa ili wakiri uhalifu wanaotuhumiwa nao na pengine wengi hawajui kuwa wapo wengi magerezani wa jinsi hiyo.Iwapo jeshi lingekuwa linatesa raia kweli,CCM ni wazi wasingeshinda kiti cha udiwani huko Mtwara.Sasa kama hao wanaoteswa taarifa zao hazitolewi na vyombo vya habari,huoni wao waliamua kutoa taarifa kwa njia ya kura?Je ni kweli haya yanaweza kutokea kwa chama cha wastaarabu kama mwenyekiti wao alivyobainisha?Siamini habari hizi.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
hawa watu wa CUF wanajiteka wenyewe iliqapate kura za huruma by CUF na CCM...najuta kwanini ninafamilia ningefanya kitu ambacho kingekumbukwa miaka 100 ijayo kupiga huu uhuni na hivi Kagame, Museven na Uhuru tuna bifu naona...
 
Hayo ndo matokeo mazuri ya kuwa na waziri mkuu mwenye hekima kama mfalme Suleman
 
Hawa cuf waache longolongo wenyewe ndo chanzo kikubwa cha haya yote wanachotanguliza kwao ni udini kisha mengine baadae,,hata hivyo hawajachelewa sana ni wakati sasa upinzani uweke nguvu ya pamoja kumwondoa mkoloni mweusi ccm
 
ni unyamma ambao haukubaliki CUF watu wake wameonewa zamani hasa kule Zanzibar kwa hivyo hayo sio mageni

il mimi nitafautiane na mtowa mada wanao onewa sio CUF bali ni Watanganyika
 
Hawa cuf waache longolongo wenyewe ndo chanzo kikubwa cha haya yote wanachotanguliza kwao ni udini kisha mengine baadae,,hata hivyo hawajachelewa sana ni wakati sasa upinzani uweke nguvu ya pamoja kumwondoa mkoloni mweusi ccm
Umenena Vyema.Lipumba Kaidhibitishia Dunia kupitia Mahubiri yake pale Msikiti wa Idrisa kwamba alipiga Kampeni Kidini ili Rais awe wa Dini yake.Nashauri akubali matokeo maana Mungu hamfichi MNAFIKI.
 
Umenena Vyema.Lipumba Kaidhibitishia Dunia kupitia Mahubiri yake pale Msikiti wa Idrisa kwamba alipiga Kampeni Kidini ili Rais awe wa Dini yake.Nashauri akubali matokeo maana Mungu hamfichi MNAFIKI.
CCM inampiga mke wake cuf sisi wa CDM tuchukue jembe tukalime
 
Back
Top Bottom