CUF nao waanza kuonja machungu ya CCM

CUF nao waanza kuonja machungu ya CCM

Hawa ndugu zetu wa CUF huwa wanajidai wanaiponda CHADEMA na kuitetea CCM. Naona sasa na wao CCM imewageuka. It appears harakati za CCM kuumaliza upinzani nchini ni dhahiri. Uwezo wa akina Pinda kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha matatizo ni mdogo kupita kiasi. Sasa kila kitu ni ubabe tu. Msome Mtatiro hapa chini.

Julius S. Mtatiro

NI MATESO, DHULUMA NA UKATILI MTWARA.

Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF - Shaweji Mketo ameyekwa na wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.

Mketo alienda Mtwara MJINI jana na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.

Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama aliofanyiwa.

Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.

Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga 0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya nguoni na kebehi za Hali ya juu.

Tumefanya juhudi za kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa hajawashikilia viongozi wetu. Nimemjulisha kama wako mikononi mwa wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza Hali ya hatari Mtwara??

Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.

Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya mateso makali ya wanyama hawa.

Tunaposema kuwa nchi hii kuna siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.

Tunaendelea kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii unapotezwa kwa faida za watu wachache.

Vyombo vya HABARI hivi sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu wasio na hatia kama siyo mimi na wewe?

Mawakili wetu pamoja na mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759.



Ni kweli inauma. But what realy happened kwenye ule muafaka wa CCM na CUF? Ni kwa nini hawakufikiria athari za kuside na CCM wakati zilikuwa zinaonekana? Ni nani alisema Nyoka huwa ana undugu na binadamu? Kwa nini hawakustuka hata baada ya kuona watu wemgine wote wanawashangaa?

Naamini upinzani ungekuwa na maana kama ile CUF ya miaka ile ingekuwa moja na CHADEMA ya sasa. Tungekuwa hatua nyingi kuelekea kuikomboa nchi yote.

Pamoja na kuwa bado inaumiza kwa yanayotokea Mtwara, napenda iwe fundisho kwa wapinzani wote hapa nchini. There is no siding with CCM that will let you free one day. Take it from me "hakuna utawala wowote duniani utakaounda mpango wa kujiangusha wenyewe, not even CCM"
 
Kwanini uambiwe umiza mtanzania mwenzako nawe kama zuzu ukubali? Majeshi yetu yanatumiwa vibaya sana na serikali ya CCM.

Wakati unakuja wananchi watasema hapana, hapo ndipo machafuko yatatokea na uasi wa wananchi dhidi ya serikali yao.

ENOUGH !!!
Tatizo ni kwamba wanajeshi wa jeshi la wananchi walio wengi ni form four na form six failures. Hawana hata huo muda wa kureason out kabla ya kufanya maamuzi. Likewise polisi wetu. Kuna shida kubwa hapa nchi kwetu maana jeshini ndiyo sehemu ambako wazazi wanapeleka watoto wao walioshindwa shule. Na hilo nina ushahidi wa dhahiri kabisa kwamba vilaza wengi wa darasani kwangu tukiwa A - level hivi sasa wapo jeshini halafu wananipiga mkwara ile mbaya.
 
Imekuwa ni malumbano kila kila kunapotokea vurugu nchini ni punde tu Nimemsikia mwenyekiti wa Cuf akila lamikia kitendo cha kutekwa kwa mkurugenzi wa taifa wa mipango na uchaguzi ndg shaweji mketo na katibu wa Cuf mtwara mjini walipokuwa wakitoka msimbati, huku siku za nyuma chama Hicho ki
Mewahi kulalamikia juu ya jeshi Hilo kuwakamata viongozi wa chama Hicho na wanainchi kuwatesa kisha kuwaachia hii ndio siasa ya nchi yetu ilipofikia ambapo jeshi letu lime ingia Katika mchezo wa siasa.
 
Vyombo vya dola ndio tegemeo la ccm kwa sasa sio wananchi.
 
Back
Top Bottom