Heshima mbele wana jamvi wenzangu,
Dk. Slaa ametoboa siri ya namna CUF ilivyoamua kuwa sehemu ya ufisadi kwa kodi za watanzania, baada ya kufichua barua mbili ambazo Seif aliomba fedha kwa ajili ya kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.
Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa CUF Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao wa chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh milioni 34.
Dk. Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za Kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.
Aidha Dk. Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya Makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.
Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemea hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa waziwazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na serikali ya CCM.
Jamani huu ni wizi wa waziwazi, na ndo maana CUF nayo inakufa, CDM tukaze buti tuondoe ufisadi na ujinga wa kutumia hovyo rasilimali ya nchi kwa private and personal issues, maana kesho tutasikia wanaomba posho za bibi, mjomba, na kufanikisha harusi ya mdogo wake rafiki wa bibi mzaa shangazi kwa mke mdogo wa babu aliyeko omani
Source: Mkutano wa CDM tandahimba