CUF na serikali damu damu

CUF na serikali damu damu

petrol

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
643
Reaction score
464
wanajamvi mmemsikia Dk. Slaa akieleza jinsi CUF inavyotegemea serikali hata kugharamia vikao vya chama. Hapa upinzani wa kweli unakuwa mashakani. Msikieni Slaa akiunguruma

"Dk. Slaa atoboa siri ya CUF
Naye Dk. Slaa alitoboa siri ya namna CUF ilivyoamua kuwa sehemu ya utawala, baada ya kufichua barua mbili zikiomba fedha kwa ajili ya kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa CUF Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao wa chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh milioni 34.Dk. Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za Kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.Aidha Dk. Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya Makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemea hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa waziwazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na serikali ya CCM."
 
Mtatiro yuko hapa jamvini??? Atujuze kidogo!
 
CCM imewashinda?

Taarifa nyeti za serikali zimebanwa siku hizi na umaarufu wa wizi wa nyaraka umeisha sasa unakurupukia kwa CUF?

Kweli Mitanganyika ina wivu wa kike kama alivyosema Mh 6

We mbona hukujibu tuhuma za mchumba wako!

Inauzi sana, nitapasua Laptop sasa hivi!
 
Guys, these people are now One. Ni vema mkajua hilo. Kwa hiyo ni kwamba Maalimu Seif na familia yake pamoja na CUF na familia yake ni sehemu ya SUK na CCM. Sasa ati nyie kwa kufikiri kuwa Maalim tofauti, of course kutokana na ujinga wenu, mnadhani kuwa anaweza enda Mombasa, au popote pale ndani na nje ya nchi, halafu mkewe akabaki Ikulu Znz. Kalaga baho
 
Heshima mbele wana jamvi wenzangu,
Dk. Slaa ametoboa siri ya namna CUF ilivyoamua kuwa sehemu ya ufisadi kwa kodi za watanzania, baada ya kufichua barua mbili ambazo Seif aliomba fedha kwa ajili ya kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa CUF Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao wa chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh milioni 34.

Dk. Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za Kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.

Aidha Dk. Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya Makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.

Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemea hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa waziwazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na serikali ya CCM.

Jamani huu ni wizi wa waziwazi, na ndo maana CUF nayo inakufa, CDM tukaze buti tuondoe ufisadi na ujinga wa kutumia hovyo rasilimali ya nchi kwa private and personal issues, maana kesho tutasikia wanaomba posho za bibi, mjomba, na kufanikisha harusi ya mdogo wake rafiki wa bibi mzaa shangazi kwa mke mdogo wa babu aliyeko omani

Source: Mkutano wa CDM tandahimba
 
Tena hao CUF ndiyo watajizika wazima wazima pindi bwana wao nyinyiemu atakapopigwa chini na nguvu ya umma. It is just a matter of time.
 
Mkubwa!CCM na CUF ni wanandoa,walikula kiapo cha kupendana kwenye chida na raha na ndio maana kwenye kifo wanaenda sambamba,lakini pia kwenye ndoa yao Mungu kawajalia mtoto anaitwa NCCR
 
Mkuu tuanikie vitu ili wale wa chuya 2015. Huu ni wizi na ufisadi wa hali ya juu. Maalimu jamani tangu zamani mimi nilijua anatafuta ulaji tu. He is the product of GAMBAZ
 
Tena hao CUF ndiyo watajizika wazima wazima pindi bwana wao nyinyiemu atakapopigwa chini na nguvu ya umma. It is just a matter of time.
Nyetk,
Mkuu CUF walishajimaliza zamani, kilichobaki ni kivuli tu.
 
Last edited by a moderator:
Kama wamewawezesha CUF kuchota hela ya Serikali kwa Matumizi ya Ki-Chama, Je Nyinyiemu wanachukuaga Shilingi ngapi toka Serikalini kumkodishia ndege Nape kwenda Bukoba? Amka Mtanzania. Saa ya Ukombozi ni Sasa!
 
Tanzania nchi yenye neema kila kitu kinawezekana, Mkuu ameingia akaona wenzake wanavyofanya naye ameamua kucheza ngoma hiyo hiyo. Viongozi/ wanasiasa wengi wanahubiri ukweli na kutenda kinyume chake. Huu ndiyo ukweli. Wanaoumia ni wananchi wa kawaida na walipa kodi.
 
Anaetumia pesa za walipa kodi kumlipa yaya, wa hawara (mke wa mtu) aliyezaa nae nje ya ndoa, perdiem zaidi ya laki kwa siku na kumchukulia hoteli ya zaidi ya laki kwa siku leo anaweza kupanda jukwaani kuyasema hayo, tena bila ushahidi? kweli wajinga ndio waliwao.

TUNTEMEKE yuko wapi?
 
Back
Top Bottom