CUF na NCCR kupasuka Vipande

CUF na NCCR kupasuka Vipande

Unaleta hisia hapa,unajua makubaliano ya Ukawa?Nenda katafute makubaliano ndio uje hapa ufanye analysis yako!
 
Wewe si batili ,Nakubatilisha... .Nenda zako na mapepo ya ufisadi.Rudi Nyuma yetu shetani wewe huwazi kukomboa nchi ,unawaza ccm.
 
Mbona coalition duniani nyingi tu duniani? Mfano mzuri ni kenya. Muda wa kung'angania vichama vidogo vidogo umepitwa na wakati. Viva ukawa!!
 
Sina hakika kama vyyama vya CUF na NCCR vilifanya SWOT analysis, katika project kubwa kama hii ya kuongoza Nchi nashangazwa na mipango ya hawa wanaojiita UKAWA.

Nianze kwa kutoa pongezi zangu kwa Mh. Mbowe na viongozi wote wa UKAWA.


  1. Kwa kutambua na kubadirisha sera na hoja baada ya CCM kumleta Mgombea Mh Pombe Magufuli hakika hii ilikua ni Suprize kwetu wanamapinduzi, zile hoja na kashfa za UFISADI zisingefua dafu ndidi ya huyu bwana, kwa kutambua CCM wameua hoja yetu ya UFISADI kwa kutuletea Mh. Pombe nakupongeza Mh. Mbowe na jopo lako kwa ubunifu na umaridadi wa Kuigeuza hoja hiyo ya ufisadi kuelekea kwetu na kuibua hoja mpya ya “System” kwa sababu sio rahisi kumattack Pombe moja kwa moja.
  2. Kwa kutambua hatuna mtu angeweza kushinda Uchaguzi ukaamua kutuletea Ndugu Lowasa, najiulizza kama lowasa asingejiunga nasi tusingesimamisha Mgombea?
  3. Kuwaburuza wanachama kwa majority rule, na kupuuza wale minority ambao wanaweza kua na ukweli.

UKWELI ULIVYO KUHUSU UKAWA.

  1. UKAWA ni muunganiko usio rasmi hinyo kufanya makubaliano yote kutokua Halali na yakihuni.
  2. UKAWA haitambuliki na NEC wala Msalijili wa Vyama vya Siasa, hivyo kuacha political dilemma hasa kwa wananchi japo halizungumzwi (Uoga wa kuzungumzia ukweli)
  3. Endapo Makubaliano yatakiukwa hakuna namna ya kudai haki popote ni kama mtu asipokupa gift au urithi alikuokuahidi huna mahali pa kumdai hata kama mliandikishana mkataba kwa sababu hana anachogain.
  4. Kila chama kina nadi Ilani yake (Lipumba kunadi Mgombea wa Chadema ambaye anasimamia Ilani tofauti)
  5. Utata wa mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi bado (Chadema wameshaweka wazi uhitaji wa majimbo zaidi ya 140, CUF na NCCR watabaki na nini?
  6. Kukosekana viongozi wenye uwezo wa kuhojji, kupambanua mambo, na kusimamia misimamo yao kunatia shaka aina ya serikali watayoiongoza, tunaona jinsi viongozi wa ukawa hasa wale wenye elimu wanavyoburuzwa bila kuhoji (UKAWA inahitaji kina Dr. Slaa wengi zaidi ili iweze kupewa dhamana kubwa hii, na sio watu wanaoendeshwa na uchu wa madaraka na matukio)


Ikiwa CHADEMA itashinda

  1. CUF na CHADEMA kwa kuwa havitasimamisha mgombea wa URAIS, ndo vitakua vimekufa kisiasa. Kutokua na Presence kutavifanya kuwa mfu katika ulingo wa kisiasa
  2. Kukosa Ruzuku ambayo hupatikana na idadi ya kura alizopata Mgombea urais wa Chama husika (undeshaji wa shughuli za chama kuzorota kwa kutokua na vyanzo vinavyoeleweka)
  3. kama CHADEMA itashindwa pamoja vyote ambavyo wangepoteza kama CHADEMA ingeshinda, wataachwa na vidonda visivyopona vya kuonekana wasaliti na wahujumu wa mabadiliko, maumivu yatakua makali sana kama wasiposimamisha wagombea ubunge katika majimbo yao, watashindwa kuendesha shughuli za chama na ndio utakua mwisho wao. (wanachama wa CUF na NCCR amkeni mdai chama chenu, Juma Duni atarudi CUF akishindwa Uchaguzi?? Kumbuka ni Mchezaji wa kukodi huyu).

Nini cha Kufanya,

  1. Kukubali yaishe, kuua vyama vyao na kujiunga na kimoja chenye nguvu (Chadema). Lipumba, Mbatia, Makaidi etc wapewe majimbo ya kugombea ubunge watajihakikishia maslahi yao endapo Chadema kitashinda au Kupoteza, hata hivyo nani asiyependa kuona bunge lenye watu machachari kama Lipumba, Mabatia, Mbowe, Slaa, Makaidi, Lissu, Zitto n.k (Kwani Mkiungana katika Chama kimoja kwa dhamira safi, ilani ya pamoja na misingi ya pamoja mtakua mmechelewa wapi? Kuliko huu unafiki na ujinga mnaouita UKAWA?)
  2. Itemike Nguvu ya makusudi ya Kumrudisha Dr. slaa kabla jahazi halijazama (Don’t ever underestimate him)Tuanze kwa lowassa kjisafisha mwenyewe, Lowasa akijibu hoja ya Richmond alituachia maswali badala ya majibu tunaomba atuambie ni nani alikua nyuma ya Richmond na atupe ushahidi beyond reasonable doubt, ajibu tuhuma zote zinazomkabili kama Ofisi ya Bunge, “Vodacom Jelo Jelo”, Ubalozi wa South Africa na nyinginezo,

Ndimi,

Batili.

Samora Avenue.

Sikubaliani nao mia kwa mia but nimependa uchambuzi wako!
 
Mbona coalition duniani nyingi tu duniani? Mfano mzuri ni kenya. Muda wa kung'angania vichama vidogo vidogo umepitwa na wakati. Viva ukawa!!
Muungano utakua na maana, kama wakijiunga na Chama kimoja tofauti na hapo ni kujidanganya.
 
Wewe si batili ,Nakubatilisha... .Nenda zako na mapepo ya ufisadi.Rudi Nyuma yetu shetani wewe huwazi kukomboa nchi ,unawaza ccm.
Kama hamjajiandaa acheni, mnakimbilia wapi? Nchi yetu sote - Mwl. Nyerere
 
Unaleta hisia hapa,unajua makubaliano ya Ukawa?Nenda katafute makubaliano ndio uje hapa ufanye analysis yako!
Hata kama yapo sio legal, Wanagawana Madaraka kama Nyanya kama Makubaliano yapo yawekwe wazi kwa Maslahi ya wengi.
 
Huyu...jamaa nayeye mkaguzi si alisema amefanya .....ujasiriamali kwa kuuza nyumba za serekali na kuingiza hasara ya zaidi ya sh....bilion 250 ..na meli ya kipindi kile ,,watanzania wanakumbuka.......sanaa .....
Haimfanyi tukasahau uchafu wa lowassa
 
Yaani, nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani CUF na NCCR_Mageuzi wamejiondoa ufahamu kiasi hiki. Sijui nani kawaloga! Mbona haihitaji degree kwa mtu yeyote kuuona mwisho wa hivi vyama? ? Makaidi yeye hana cha kupoteza kwani kuwa ndani ya UKAWA kuna mjenga yeye binafsi Na wala so chama chake ambacho hata hivo ni kama hakikuwapo. .Mbatia na Lipumba akiri menu mmezibinafsisha wapi??
 
Naona huu uzi Ma ccm wamejipanga kuja na akaunti saba saba kujijibu

Sio mbaya nami nitie neno, hivi unadhani mleta mada maana hii sio hoja, una uwezo mkubwa wa deep thinking zaidi ya Mbowe, Makaidi, Prof Lipumba, Juma Duni, Mbatia, Prof Safari, Maalim seif na jopo lote la walioshiriki kuifikisha hapa UKAWA?

Unadhani hawakukaa na kupima pande zote za RUZUKU, KUSHINDWA, KUSHINDA, THE TOMMOROWS AND THE AFTER TOMMOROWS ya vyama vyao na complications kama izo?

Hivi unadhani walipomkaribisha lowasa hawakuwa na muda wa kupima neno" Ikiwa" na mazao yake na kwanamna yeyote ile? Ikiwa hivi, nini kitakuwa vile?

Unadhani vikao walivofanya Usiku na mchana, huku kukiwa na Hujuma kali sana toka kila pande hawakuwaza vitu vyepesi hivi ulioandika?

Vyovyote utakavyojibu maswali hayo, jibu linabaki, walifikiri zaidi ya ulivofikiri na kuandika

Leave Us, The Destination will justify the Means. Kwasasa Hoja ni CCM must die early in the Morning of 25th October
 
Cdm vchwa maji,ccm itawachezea hadi wachzke,fikra ni zero,wazo ni ikulu na mali za watz,wenzao wanawaza uhai wa taifa.Siasa ni hesabu,ucpoijua hesabu utabaki unahaha na kutegemea neema za kusadikika kama wafuasi wa cdm,ccm hiyo hiyo iliwapa shibuda awavuruge,ikatoa zito mkawehuka, mbatia na wazo la ukawa mkapokea,lowasa nae mmeona mmewini,watatoa mbatia,slaa na lipumba na hamtotambua k2 kw fikra zenu hafifu,jifunzeni kutafakari mambo kuliko ushabiki pacpo fkra,tafakarini sn wazee wnzng.
 
Haimfanyi tukasahau uchafu wa lowassa

Lowasa...kawaambia yeye alitaka kuvunja mkataba...mkuu wa kaya akagoma.....pili mbona serekali yenu dhaifu mbona hamumpeleki mahakaman...???
 
Magwanda mmezidi jazba hata mkieleweshwa kitu muhimu kwa maslahi yenu hamfahamu.

Kwani UKAWA wote wakibatizwa U CHADEMA halafu wakapewa majimbo tukapata bunge la nguvu ni jambo baya?
 
Huyu...jamaa na yeye mkaguzi si alisema amefanya .....ujasiriamali kwa kuuza nyumba za serikali (dalali wa nyumba za serikali) na kuingiza hasara ya zaidi ya sh....bilion 250 ..na meli ya kipindi kile , kuvunja kituo cha mafuta, alitaka kuvunja jengo la TANESCO Ubungo, akawambia Kigamboni wapige mbizi, watanzania wanakumbuka.......sanaa .....


Mkuu sio hivyo tu. Ukweli ni kuwa huyu ni mgombea wa kitengo na anakwenda kupambana na mgombea wa wananchi. Halikadhalika, anaunga mkono Katiba iliyopendekezwa na Kitengo wakati wa UKAWA ni wazi anaunga mkono Katiba ya Wananchi. Kazi ipo. Tutaona kama Wananchi wanapenda kitengo ama wanajipenda wenyewe!

Ama kuhusu uhai ama kufa kwa vyama vilivyounda UKAWA, hilo wala sio suala la maana. Chama ni wanachama. Kikifa si kinaundwa kingine, kuna shida gani? Haohao wanaotia hofu vyama kufa ndi waliokuwa wanashadidia vyama vipya kama Asasi ya Chama Tawala (ACT). Eti leo wamekuwa hodari na wenye ujasiri wa kuelezea masikitiko ya kufa CUF na NCCR. Tuwaulize tu kuwa wao watapata hasara gani? Waswahili wamenena "Inzi kufa kidondani si haramu". Chama kikifa kwa kufanya siasa ni halali rafiki.

Kwa kuhitimisha, jiulize tu kuwa KANU na UNIP vilikufa kwa kushirikiana na chama gani vile? Tafuta hoja nyingine.
 
Yaani, nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani CUF na NCCR_Mageuzi wamejiondoa ufahamu kiasi hiki. Sijui nani kawaloga! Mbona haihitaji degree kwa mtu yeyote kuuona mwisho wa hivi vyama? ? Makaidi yeye hana cha kupoteza kwani kuwa ndani ya UKAWA kuna mjenga yeye binafsi Na wala so chama chake ambacho hata hivo ni kama hakikuwapo. .Mbatia na Lipumba akiri menu mmezibinafsisha wapi??

Pesapesa mdugu
 
Magwanda mmezidi jazba hata mkieleweshwa kitu muhimu kwa maslahi yenu hamfahamu.

Kwani UKAWA wote wakibatizwa U CHADEMA halafu wakapewa majimbo tukapata bunge la nguvu ni jambo baya?

Mimi nionavyo CDM wote Na ccm mnapanic
 
Back
Top Bottom