Maprofesa ni watu makini wanaopenda vyama makini.CUF ina mwanachama mmoja tu ambaye ni Profesa naye ni Profesa Lipumba ingawa si full profesa.CHADEMA pia kina mwanachama mmoja tu ambaye ni profesa naye ni Profesa BAREGU.
CCM ina maprofesa kibao list yao haitoshi kujaza JamiiForums.
Maprofesa baada ya kutafakari kwa kina naona wamegundua ubabaishaji kwenye hivyo vyama.
Kukosa maprofesa wengi kwenye chama kuna madhara makubwa.Mojawapo ni hili la meya wa Dar es salaam ambaye ni meya pia wa kusimamia vyuo vikuu kama Dar es salaam.
Kwa mara ya kwanza toka tanzania ipate uhuru Dar es salaam imepata meya mwenye kiwango kidogo cha elimu kuliko meya yoyote aliyewahi kuweko dar es salaam.Ni aibu kwa CHADEMA.
Mara nyingine ni bora ubaki kimya kuliko kudhihirisha ujinga ulionao,kama nawe ni miongoni mwa vile vibudu 46 vya Lumumba vilivyoombewa "pepo ya uongozi" na mkwere,ni vema ukatulia na mzee huko Mombasa Maana hata Kazi ya kuwafanyia "massage" wageni walalao Kebby's Hotel huwezi kupewa.
Umetumia njia gani iliyokuwezesha kuwafahamu wanachama wote wa Chadema na CUF pamoja na Elimu zao?Ulifanya lini utafiti uliokuwezesha kugundua kuwa maprofesa wengi wapo ccm?Au umeangalia wingi wao katika nafasi za serikali ndiyo ukakurupuka kuleta mada jukwaani?
Ni upumbavu usiomithirika kuwafananisha watendaji wa chama na watendaji wa serikali.Mfano wako ungekuwa na mashiko kama ungetuorodheshea maprofesa waliopo CCM katika ngazi ya chama na si kuwajumuisha maprofesa waliopo serikalini.Hata UKAWA ingepewa fursa ya kuongoza nchi ingekuwa na maprofesa wa kutosha kutokana na muundo wa serikali ulivyo tofauti na muundo wa vyama vyetu.
Nafikiri ukivilinganisha Chadema na CCM kwa ngazi ya chama,Chadema ina wasomi wengi zaidi walio kwenye nafasi za uongozi wa chama Taifa kuliko ccm.Mlinganishe katibu mkuu wa Chadema na wa ccm,nani Mwenye Elimu ya juu?Dkt.Mashinji na jangili Kinana nani msomi? Makamu mwenyekiti wa Taifa ccm na Chadema,namaanisha Profesa Safari na Filip mangula nani msomi?
Ukiuruhusu ulevi wa kiitikadi utamalaki katika fahamu zako,utakufikisha mahali ushindwe kutofautisha hadi aina za rangi badala yake kila ukionacho utakinasibisha na ccm.OK,tufanye maprofesa na wasomi wote wa Taifa hili ni wanaccm kama unavyotulazimisha tuamini,Usomi wao umelisaidia nini Taifa zaidi ya kukaa kimya na kuiacha serikali na vyombo vyake ikiendelea kutenda jinai kwa kupora haki za kikatiba za kuchagua na kuchaguliwa?
Hao unaowaita wasomi hawaoni namna ccm inavyolazimisha kubaki madarakani kwa kufuta chaguzi za haki na kuitisha chaguzi feki ili wajibakishe madarakani?
Hao vimeo unaowaita maprofesa ni wapi walitumia Elimu zao kuzuia Wizi,ubadhirifu na ufisadi wa kutisha unaolitafuna Taifa kwa miaka zaidi ya 50 sasa?Si haohao ambao hutumiwa kama wachora ramani za ufisadi?
Hivi kwani huwa mnachomolewa ubongo kabla ya kuwa wanaCCM?Haiingii akilini mtu akajitoa ufahamu wa kutojua madhira yaliyoletwa na CCM.Hakuna reference mbadala zaidi ya CCM katika siasa za Tanzania tangu Uhuru,maovu yote yanayolikumba Taifa letu mwasisi wake ni ccm,hakuna mwingine mnayeweza kumuhusisha na Takataka zote zinazolikumba Taifa letu zaidi ya ccm yenyewe.Yote tunayokabiriana nayo ni Kazi tukufu ya mikono ya CCM na serikali zake.Hata anayejinasibu kutumbua majipu,anajuwa fika kuwa vimelea vilivyoyasababisha majipu hayo ni CCM ambayo yeye mwenyewe ni sehemu yake.Au mleta mada hufahamu kuwa hata wimbi la uvccccmm kukimbilia Mombasa kutafuta "malisho halamu" ni matokeo ya kushindwa kwa Sera za cccccmm?
Wapumbavu wa aina yako mnaoishi kwa kusubiri fadhira za mafisadi wa serikali ya ccm huku mkijikomba kwa kujaribu kuupotosha Ukweli ni janga kwa Taifa letu.Ninyi ni maadui wa hatari zaidi kuliko wale maadui watatu wa Taifa letu waliotangazwa na Mwl. Nyerere.
Yawezekana umezoea vya bure na ndiyo maana umeishia kuwa mnafiki hadi kwa nafsi yako,unatenda kinyume na dhamiri yako.Lakini kwa sababu unaendeshwa na tumbo,imeamua kuwa zezeta usiyetaka kusikia chochote zaidi ya uhayawani wa ccm.
Kweli kuishabikia ccm unapaswa uwe taahira mwenye hisa ya akili ya chini kiasi cha kushindwa hata kujimudu kifikra.Thamani ya utu inadharirishwa na mnaojiita wanaccm,ninyi ndiyo wapumbavu halisi mliotangazwa pale jangwani na mpumbavu mwenzenu.Inatia kinyaa na ni najisi kabisa kujiita mwanaCCM mbele ya jamii ya walioelimika,bora ufe kuliko mtu kukuita L46b7.