CUF na CHADEMA kipi Chama bora?

labda ungewashindanisha wale wanandoa ndo ingemata, lakini kwa hii hoja yako ni lazima ni :A S thumbs_down:
 
Si mumunyi wala kutafuna kwa sera CUF wako vizuri sana.Chadema ni wapambanaji ila kwa sera Cuf kwere
 
Si mumunyi wala kutafuna kwa sera CUF wako vizuri sana.Chadema ni wapambanaji ila kwa sera Cuf kwere

Inajulikana wazi kuwa CUF ni tishio na kiboko ya CCM ,hili halina ubishi ,Chadema au makobe hawa ni wapita njia wageni na kawaida mpita njia anapopita huwa anafuatwa na kuangaliwa na wenyeji.

CUF ipo na itakuwepo ila Chadema ni chama kisichokuwa na dira ,hizi mbio inazokwenda Chadema siku ikipigwa ngwara basi itaangukia upua.

CHADEMA
aldabra-giant-tortoises.jpg
CDM
 
CHADEMA ndicho chama bora Tanzania..kwasababu
1.kimeonesha dhamira ya kweli ya kumkomboa mwanachi..in short angalia mchango/hoja za chadema katika bunge then linganisha na za CUF
2.hakina udini..hapa najiwa watu watanipinga lakini ukiangalia uongoz wa chadema kwaanzia mwenyekiti hadi ngazi za chini utaona dini zimebalance.(nadhan kuna uzi humu ndan ulonesha uongoz mzima na dini zao unaweza ku-refer)..lakini CUF uongoz wao dini hazija balanc
3.hakina ukanda.kuhusu ukanda kuna dhana potofu inayotumika sana kujudge kwamba kama chama kimeenea sana kanda flan basi hicho chama kinaukanda..hilo mimi naona its the wrong way of judging..kwavyovyote chama chochote kina ngome zake muhim..by the way operesheni okoa kusini imewafumba mdomo..
ngoja niende lunch ntaendelea siku nyingine.
 


hahaha!! issue ya udini chadema si ndio nyumbani ... rejeo tamko la muasisi wa CDM ... na ile kauli ya LEMA arusha kwamba watu wa arusha wawe makini na wanao vaa ma baibui na kujistri kiislam kwani ni alshabab... need to say more! ? hilo bandiko lipo humu JF

tuwekee limk mnafiki mkubwa wewe na kama itapishana manen uliyyasema ule ban
 
tuwekee limk mnafiki mkubwa wewe na kama itapishana manen uliyyasema ule ban

SOMA KWENYE RED NDIO CDM HII NA KAULI ZA VIONGOZI WAO....

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/223669-shahidi-lema-alimkashifu-dk-buriani-jukwaani.html

Huyu ni mwanasiasa ambaye anadhamana ya kuwawasikilisha wananchi bila kuwabagua.

MDAI wa pili katika shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Arusha mjini, jana aliieleza mahakama kuwa alimsikia mdaiwa kwa kwanza katika kesi hiyo, Godbless Lema (Chadema), ikiwataka wapiga kura kutomchagua aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian kwa kuwa ameolewa Zanzibar na ana ujauzito wa mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Akiongozwa na wakili wake, Alute Mughwai, mdai huyo, Agnes Mollel (44) alidai kumsikia Lema akitamka maneno hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita uliofanyika eneo la Big Sister, Mtaa wa Roman Catholic, Kata ya Olorien, Manispaa ya Arusha.

Aliieleza mahakama mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila kuwa mkutano huo ulifanyika eneo hilo ambako yeye ni Mwenyekiti wa mtaa Septemba Mosi, mwaka juzi.

Agnes alikuwa akitoa ushahidi wake, akiwa shahidi wa pili baada ya mdai wa kwanza, Mussa Mkanga kumaliza ushahidi wake, ambapo alidai kumwona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio Lema akihutubia jukwaani na kuwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba Dk Batilda hastahili kuchaguliwa kwa sababu ni mwanamke.

"Msimchague huyo mwanamke Dk Batilda kwa sababu ameolewa na Mzanzibari na hapo alipo ana mimba ya Lowassa. Hivyo mkimchagua jimbo hili mtakuwa mmeliuza kwa Lowassa na amesema akichaguliwa atakifunga kituo cha Radio cha Safina," alisema Agnes akidai kumkariri Lema.

Shahidi huyo alidai maneno hayo yalimkera na kumfanya aondoke kwenye mkutano huo kabla Lema hajamaliza hotuba yake na siku iliyofuata alitoa taarifa kwa Dk Burian kuhusu tuhuma na kashfa zilizotolewa dhidi yake na mgombea huyo wa upinzani.

Hata hivyo shahidi huyo alikiri kuwa madai ya Lema kutamka kuwa Dk Burian alizaa na mwanamume mwingine hayako katika hati ya madai waliyowasilisha mahakamani na wala jina la muhusika halikutajwa kwa kile alichodai inawezekana ilisababishwa na makosa ya kiuchapaji.

Aliiomba mahakama kutengua matokeo na kumvua ubunge Lema iwapo itaridhika na ushahidi wao pamoja kuamuru wadai kulipwa gharama za shauri hilo namba 13/2010 ambayo awali ilikuwa ikisilikizwa na Jaji Aloyce Mujulizi aliyejitoa baada ya mdai wa kwanza kukosa imani naye.

Akihojiwa na wakili wa Lema, Method Kimomogoro, shahidi huyo alikana maelezo yaliyo kwenye hati yao ya madai kuwa yeye alimsikia mbunge huyo akitoa kauli za kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian katika mkutano wa hadhara uliofanyika Saa 10:00 jioni ya Septemba 22, 2010 eneo la Fantastic, Olmatejoo, Kata ya Elerai.

Hata baada ya kuonyeshwa maelezo yaliyo katika hati hiyo ya madai aliyotia saini yeye pamoja na wenzake Mkanga na Happy Kivuyo, shahidi huyo alisisitiza kutotambua maelezo hayo na kudai kauli yake mbele ya mahakama ndiyo sahihi kwamba mkutano aliohudhuria ni ule uliofanyika Big Sister na siyo vinginevyo.

"Mimi maneno niliyosikia na kumshuhudia Lema akitamka ni yale ya Big Sister, siyo Olmatejoo. Kwanza mie sipafahamu hata huku Fantastic na niliweza kuyakariri kauli hizo bila kuzinasa kwa kinasa sauti wala kuziandika sehemu yoyote," alisisitiza Agnes.

Katika hatua nyingine, shahidi huyo alidai kutosoma wala kusomewa maelezo ya Dk Burian katika barua yake ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha akilalamikia kauli za Lema dhidi yake.

Hali hiyo ilimfanya wakili Kimomogoro kumhoji iwapo alilazimishwa kufungua shauri hilo mahakamani bila ridhaa yake ndio maana hajui undani wa viambatanisho vilivyo kwenye hati yao ya madai, lakini alipinga kwa maelezo kuwa aliungana na wenzake kufungua kesi hiyo baada ya kuchukizwa na kauli za udhalilishaji na ubaguzi kijinsia, kidini na kikabila zilizotolewa na Lema dhidi ya Dk Burian.

Katika madai yao, walalamikaji hao wanadai kuwa katika mikutano yake kadhaa ya kampeni, Lema alisikika akiwaasa wapiga kura kutomchagua Dk Burian kwa sababu atarejea Zanzibar kwa mumewe baada ya uchaguzi na kuhoji iwapo mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamasai) na Wachaga mwanamke anaweza kuongoza wazee wa mila.

Kupitia kwa wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida, walalamikaji hao pia
wanadai Lema aliwatahadharisha wapiga kuwa kuwa makini na wanaovaa ushungi, vitambaa na hijabu wasije kujikuta wamechagua Al-Qaida huku pia akimtuhumu Dk Burian kuwa mwanamke asiye mwaminifu aliyezaa na kupata mimba nje ya ndoa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo anawakilishwa na mawakili wa Serikali, Timoth Vitalis na Juma Masanja


Source: Mwananchi la leo
 
Hakuna cha kujadili hapa, kama mtu huna mambo ya msingi bora usome uzi za wenzio jamani,
 
Ngoja tuweke jedwali hapa na watu wajaze
Weka Marks 0 mpaka 100%
Title
CUF
CHADEMA
Makini
Wachama wengi
Sera nzuri
Ukabila
Ubabe
Uongo
Viongozi Makini
Demokrasia Shirikishi
Chochezi
Kinacho linda
Muungano



















Haya kazi kwako.
 
Back
Top Bottom