CUF kwishne, ya Juma Duni Haji sasa rasmi majimboni, Tabora Mjini hali tete

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Baada ya ule mchezo wa CHADEMA wa kumhamisha Juma Duni Haji kutoka CUF kwenda kwao ili awe mgombea mwenza wa Lowassa ambaye naye amejinunua kwenda CHADEMA ili agombee urais mambo sasa yamehamia Majimboni ambapo sasa CHADEMA wanacheza mchezo uleule wa kuwashawishi wanachama wao wajifanye kuhamia CUF ili waombe ridhaa ya kugombea UBUNGE katika Majimbo ambayo CUF wamesimamisha wagombea kwa mujibu wa makubaliano ya UKAWA.

Sintofahamu ndani ya jimbo la Tabora Mjini ni kubwa baada ya Wanachama wa CUF jimboni humo kuandamana kupinga Mgombea wao kuenguliwa kugombea Ubunge ili kumpisha mwanachama wa CHADEMA aliyehamia CUF kwa madai kuwa ndiye anayekubalika.

Chanzo: Taarifa ya habari leo saa 12 asubuhi
 
CCM wanaumia mno kwa kipigo cha mbwa mwizi watanzania hatuwataki CCM jamani kwanini mnatulazima tuwapende !!!Ukawa ata mtugombanishe vp tutasamehana na kusonga mbele.
 
Nlikuepo jana hadi kikao kinakwisha mambo yamekwisha na atagombea mgombea wa CUF UKAWA mambo mdundo.
 
Tata madiba Mumeo unamuhudumia saa ngapi maana unashinda kutwa kwenye mitandao angalia utaachika.Nashindwa kukuelewa yani upo radhi uvuruge ndoa yako kwa ujira wa buku 7?
 
Kwenye kuifuta ccm ni lazima kila mbinu itumike, plan A,B,C mpaka Z kwa hiyo hiyo ni kawaida tu, ukawa wakiweza kuzuia mbinu za wizi, mapema tarehe 25 lazima uende labor
 
Badala utumie muda huu kukizungumzia chama chenu unajisumbua na ya UKAWA, kwa sasa umechelewa sana.
 
Back
Top Bottom