CUF Kuwapokea vigogo toka CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Kuwapokea vigogo toka CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 12, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama hii habari ni kweli basi tukae mkao wa kula kwa CUF kuingia madarakani 2010.
  Ni matumaini ya kila Mtanzania kuwa endapo vigogo hao ambao wameonekana kuwa mstari wa mbele katika kukinzana na wenzao na pia kuonekana kujitenga kwa kukemea mambo ambayo hayaendani na taratibu za Chama chao cha CCM ,kujiunga na upinzani ni mwanzo wa kuigawa hadharani CCM.

  Kuna fununu kuwa baadhi ya viongozi wa juu wastaafu wa serikali zilizopita za CCM huenda wakajiunga na Chama Cha Wananchi (CUF) ili kukipa tafu chama hicho baada ya kuchoshwa na matatizo yanayoibuka kila siku yanayokikumba chama tawala CCM,pia baadhi yao wamesikika wakisema wanafikiria kujiunga na vyama vingine lakini bado hawajaamua kutokana na migongano inayoibuka ndani ya vyama hivyo tofauti na CUF ambacho kimeonekana kutulia kabisa na hakina usongo na viongozi wanaohama au kuhamia,jambo ambalo limewafanya vigogo hao kuifanya CUF kuwa ndio chaguo lao.

  Ingawa CUF imewataka vigogo hao kutulia huko waliko mpaka wakati muafaka utakapofika ndipo watangaze rasmi kuachana na CCM na UCCM ,hali sivyo ilivyo kwa wateja hao ambao hamu ya kubwaga manyanga ya Uccm imewazidi na kuona kama wanadhulumiwa kuambiwa wakati wa kujiunga haujaiva ,inaonyesha subira itawashinda.
  Nawapa hongera wale wote ambao wameanza kuona mwanga na kuona ubovu na uzembe bila ya kusahau ubaya wa CCM ambao leo hii hauhitaji mistari mingi kuelezewa mwananchi , wala haihitajiki kamati kuchunguza sera mbovu za CCM ambazo zimeshindwa kutekelezeka na kubaki kuwa ni mikakati ambayo kila siku inapangiwa miyaka ,eti mkakati baada ya miaka mia !!!
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naona hii ni ndoto ya mchana. Na kama si ndoto basi CCM imekwisha na ndiyo mwanzo wa maendeleo ya kweli ndani ya Tanzania.
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi suala la Njelu Kasaka limeishia wapi....? nafikiri Viongozi wote wa Upinzani wawe Makini na hao wanaotaka kutoka CCM for the so called Kujenga Upinzani....isije wanatoka kama alivyofanya Kibaki wa Kenya!!! then alipoingia Madarakani akashindwa kutaka actions...
   
 4. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #4
  Sep 12, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivo wakihama na wakahamia chama kimoja mfano CUF kama ulivyosema, si ndio mwanzo wa CUF kuwa CCM2?
   
 5. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Je hao viongozi wana shutuma zozote za kifisadi au nyie mnapokea tu ili mradi walikuwa viongozi huko CCM? Unaweza kukuta hao ni waroho tu wa madaraka hawajali sera wala vision ya chama chenu wanakuja kuwakoroga zaidi tu.......
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Mambo ya vyama vingi hayana mpango kabisa...Kwani hao wanaotaka kujiunga na CUF walishindwa vipi kuyapigania maslahi ya wananchi wakiwa bungeni?
  Si hao hao waliipitisha bajeti ya kifisadi?
  Kama kweli wana nia nzuri basi wanajuwa cha kufanya.
  Kujiunga na upinzani ni mchezo mchafu wa kupotezeana muda na pesa za walipa kodi wenye njaa kali!
  Hata hiyo mipesa inayotumiwa na ccm kuhonga pamoja na hizo za ruzuku ziende kwenye kilimo na kuwasaidia wananchi na UPUUZI MNAOUITA UPINZANI NA UISHE!
   
 7. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jmushi hata mimi suala la Kiongozi kutoka CCM kwenda kwenye upinzani naona ni aina fulani
  ya usanii, Siasa za Tanzania ni mchezo mchafu na wanasiasa wetu kwa kweli wametawaliwa na
  Ubinafsi, kama mwanasiasa wa CCM ana uchungu na anataka mabadiliko ya kweli basi abaki CCM
  na apiganie mabadiliko wakati yumo CCM, wanasema mpiganaji wa kweli ni yule anayebaki mstari
  wa mbele mpaka dakika ya mwisho, mabadiliko ya Tanzania yatakuja pale CCM itakapoishiwa
  nguvu, CCM itakwisha nguvu sio kwa viongozi kubadili vyama ( walitoka akina Mrema, Seif na
  akina Lipumba CCM haikutetereka) bali itaisha nguvu endapo hawa vigogo watapigania
  mabadiliko ya fikra na kutetea maslahi ya mtanzania wakiwa ndani ya CCM.
   
 8. M

  MKUDE WA MGETA Member

  #8
  Sep 13, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toeni tetesi na data na sio kukurupuka sawa///////////
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Cheap propaganda......ama ndio rejuvinatio tactics baada ya kuona CHADEMA wanatishia nafasi yenu kama upinzani wenye nguvu....

  Mkitaka kufanikiwa muwe tayari kubadili uongozi wa juu wa chama na kuongeza wigo wa siasa zenu zaidi ya "ukombozi wa zanzibar".......siasa za ufisadi ni kete ya CHADEMA ninyi mnapaswa kujenga nyingine na sio kuendelea na mkakati wa "kuibana" CHADEMA

  Ni ushauri wenye nia njema tu......

  Tanzanianjema
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Vita vya panzi furaha ya kunguru....
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Sep 13, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..idadi kubwa ya viongozi waanzilishi wa CUF walitokea/walifukuzwa CCM.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ndio kusema...
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Hivi kama wapinzani wote wakipanga na kuhamia ghafla ccm...Nini kitatokea?
  Maana naona ni bora kubanana humo ndani ya chama kwa maslahi ya Taifa.
  Kwasababu ni rahisi sana kwa ccm na serikali yake kujenga chuki kwa kujidai kuwa niwao tu wenye uchungu na nchi na ku justify kuwatenga wananchi wengine wenye vipaji vya kulitumikia Taifa simply because wao sio ccm...Dawa ni wananchi wote kujiunga na ccm na kuwafutilia mbali mafisadi na kuanzisha mapinduzi mapya....Na kudai haki zao kwasabau tuna utajiri ambao unatakiwa kuwanufaisha wananchi na si ccm tu
  Wananchi wote wajiunge na ccm halafu wadai haki zao na si kujiunga na upinzani na kuachia grupu flani liibe mali za nchi na pia liwe na madaraka eti kwasababu tu wao ni chama flani.
   
 14. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zipo dalili kadhaa za kisiasa zinazoonyesha kuwa CCM iko katika nyakati zake za mwisho.

  Lolote laweza kutokea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Nina imani kuwa CCM ikitingishwa vizuri kwa muda wa mwezi mmoja zaidi ya robo ya makada wake wataondoka.

  Nina uhakika kuwa CCM ikikosa kushikilia dola kwa miezi sita zaidi ya robo tatu ya makada wake watakimbia na kukilaani.

  Nina uhakika kuwa CCM ikiacha siasa za kuwalazimisha wafanyabiasha, wafanyakazi, tume ya uchaguzi na majeshi ya ulinzi na usalama kukiunga mkono chama kwa lazima itapoteza 90% ya wanachama wake.

  NIna uhakika CCM ikitingishwa vizuri, ikipoteza 90% ya wanachama na kunyang'anywa dola basi nchi itapona.
   
 15. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wacheni mzaha wenu hichi cham CCM kina website ya kusema uongo kiasi kuwa hakuna chama kingine hadi sasa chenye website kahiyo yakusema na kutunga uongo kwa manufaa ya wachache
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hilo ni kweli lakini huwezi wadnganya watu wote kwa muda wote.. nadhani ule mwisho wa kudanganya kwa CCm umekaribia
   
Loading...