CUF katika mkutano leo DSM

CUF katika mkutano leo DSM

Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Posts
6,932
Reaction score
4,697
Naona chama cha wananchi cuf kwa sasa hivi wana mkutano katika viwanja vya soko kuu kariako. Anaezungumza kwa sasa ni mtu anaejitambulisha kama mchungaji naona anamshambulia Dr Slaa na Chadema.
Umati wa watu wa Kariakoo ni kama hawawapi usikivu wowote kila mtu anaendelea na shughuli zake. Hivyo wale waliojikusanya kuwasikiliza wazungumzaji ni kama watu 70 to 80 hivi. Maspika ndoo yamebaki kuvuma ndani ya soko hadi watu hawasikilizani.
My take; Cuf wametumwa dakika za mwisho kupunguza moto wa mkutano wa wapinzani kesho?
.

.
 
Naona chama cha wananchi cuf kwa sasa hivi wana mkutano katika viwanja vya soko kuu kariako. Anaezungumza kwa sasa ni mtu anaejitambulisha kama mchungaji naona anamshambulia Dr Slaa na Chadema.
Umati wa watu wa Kariakoo ni kama hawawapi usikivu wowote kila mtu anaendelea na shughuli zake. Hivyo wale waliojikusanya kuwasikiliza wazungumzaji ni kama watu 70 to 80 hivi. Maspika ndoo yamebaki kuvuma ndani ya soko hadi watu hawasikilizani.
My take; Cuf wametumwa dakika za mwisho kupunguza moto wa mkutano wa wapinzani kesho?
.

.

waache waendelee kupaka rangi upepo hata wakitaka hiyo kesho wao wakafanye mkutano zakiem mbagala wajanja watakuwa tmk mwisho tuone
 
Nilikuwepo eneo la tukio,hakika cuf inatumika vibaya na viongozi wa cuf wamekubali kukiua chama kwa malipo ya ngawira na madaraka kutoka chama cha genge la wahuni linalopigania kutawala milele ili kuficha maovu yao na kuendeleza uzandiki na kuifilisi nchii hii kwa faida ya genge la wachache na familia zao ila sio wote ambao tupo tayari kutumikia majambazi ya kisiasa!!
 
Hawana madhara hao,achana nao we nenda kafue ile bendera ya taifa mahsusi kwa shughuli ya kesho,mi nitawashangilia kutokea Jf,kwani nipo vichaka flani mbali kabisa na dsm,msituangushe!!
 
CUF kwa Chadema ni kama Joka la Kibisa, ukitaka walala nalo. Tunawaandalia mwingine Kesho mtongani
 
Naona mzungumzaji wa pili eliyepanda jukwaani kajitaja kwa jina refu mno ambalo sikuweza kulikariri. Kaanza kuiponda sisiemu kwa kuua maendeleo ya mikoa ya kusini zaidi sana wakimlenga Nyerere. Ghafla kageuka na kurudi kwenye kile kinachoonekana kuwa kusudio la huu mkutano kwa kusema kuwa Chadema hawakuweka mgombea mwaka 1995 kwa sababu walikuwa na mgombea wao Benjamen W. Kaongeza kuwa hata mwaka 2000 hawakusimamisha mgombea maana bado walikuwa na chaguo lao Mkapa, lakini 2005 wamemweka Slaa kugombea kwa sababu tu sisiemu wamemweka mgombea mwisilamu Kikwete kugombea.
.
 
DSC00617-502x600.jpg picha inajieleza
 
Chama cha udini aka muslim brotherhood branch@work!
 
CCM B yupo kazini ili kutetea matashi ya mmewe!!!!
 
Sasa hivi anaitwa jukwaani m/kiti wa wa cuf wilaya. Mzungumzaji aliyeshuka jukwaani kamaliza kwa kuwataka wananchi kuwa tayari kujitoa mhanga mwaka 2015 maana ccm wameazimia kutoachia madaraka kwa makaratasi. Hivyo cuf ipo tayari kuwaondoa kwa njia ile ambayo ccm wanapendelea kuondolewa kwayo.
M/kiti wilaya anazungumzia uchaguzi wa 2014 kwa kusema kuwa ccm imewasababishia umasikini wa kutupwa. Anawaambia kuwa sii kweli kwamba kuna mtu anaekula milo mitatu kwa sasa. Wananchi wasiwe zuzu kucheka na kikwete halafu jioni wanaambiwa waende nyumbani kulala katika neti za dawa na njaa yao.
.
 
CUF wameshakata tamaa ni future ya siasa za tanzania..naona kilichobaki ni kuhubiri maandiko ya CCM. Kaazi kweli kweeli.
 
Hawatunyimi usingizi!waseme wasemalo lakini wajue Chadema ni gharika,inazoa mpaka miti!hawana lolote.
 
Sasa hivi ndo kapanda mkurugenzi wa habari wa cuf jukwaani. Anatangaza kuwa mkutano utaenda mpaka saa 1915 maana polisi ndio wametuzubaisha.
Anawatangazia watu kuwa kesho hakuna mkutano wa vyama vya upinzani. Hayo matangazo yanayotangazwa na chadema ni matamanio yao. Hakuna kitu cha namna hiyo. Anaongaza kuwa ukienda masokoni utakaowakuta ni kina nzirai/hamidu na majina kama hayo. Lakini ukisikia mkurugenzi ni kina masawe na kazi zote zenye hadhi ni kina Mbowe.
.
 
Mkurugenzi habari cufu anaendelea kuwa mkoa wa morogoro mjini hajawahi tokea mluguru mwenye uwezo wa kuwa mbunge na sasa hivi mbunge kwa sasa ni mchaga kamtaja jina ila sikuweza kulishika.
Morogoro wamenyimwa elimu kiasi kwamba kwa miaka 51 ya uhuru hakuweza kutoka mtu mwenye uwezo wa kuwa mbunge.
.
 
Acha na hiyo ndoa ya CCM na CUF, tena ni ndoa ya jinsia moja, wakiwa nje kila mmoja hujidai mwanaume wa shoka ila wakiwa chumbani kuna dume na jike.
Sio kosa lao wanatekeleza matakwa ya mume wao ili wasije wakatalakika.
 
Chama cha CUF kinajiua chenyewe.

Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya ukabila

Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya udini

Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya usisi na wao

UBAGUZI - Haukubaliki na haunanafasi wala usipewe nafasi kutugawa watanzania kwa maana yoyote ile iwe ni, din, ukabila, wao au sisi

Hapa CUF wanajiteketeza kwa mafuta yao wenyewe Raia wanateseka kwa ugumu wa maisha, bungeni tunashuhudia waziwazi

nini kinatendeka, mitaani watu wanashuhudia kwa vitendo mfumuko wa bei, huduma mbaya za afya na elimu, viongozi wakishinda

angani kutwa kucha na safari, nani atakubali kuendelea kuwa dodoki la kusafisha mapito ya mafisadi? Kama CUF wameamua

kuendelea kuwa washika pembe ccm wakamue maziwa ni hatari kubwa
, watanzania watajitenga, na CUF itapotea kabisa

kwasababu wanafaham mchawi wa maendeleo yao ni serikali Dhaifu na kujiunga nayo nikujitenga na watanzania waliowengi

yaani walalahoi.
 
Mkurugenzi anaendelea kwa kusema sii morogoro tu bali hata mikoa ya kusini walinyimwa elimu. Anatoa mfano wa majimbo yaliyo na maendeleo waliopewa uwaziri kama kina Danieli yona, Msuya na Mramba.
Anasema nimewataja hawa kuonyesha kuwa utajiri wa sehemu moja unahudumia sehemu nyingine. Anaendelea hii serikali imezidi kwa dhulma.
.
 
wapuuzeni hao...! ukisikiliza nyimbo za mpumbavu taratibu nawe utaanza kuingiwa na upumbavu. utaanza kwa kutikisa tikisa mguu...kichwa na mwishowe utainuka mazima kucheza! tayari wote mmekuwa wapumbavu!
 
Back
Top Bottom