Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 18/1/2017
Na kurugenzi ya Habari
JAJI FRANCIS MUTUNGI NI MWIZI MZOEFU, UFAFANUZI ALIOUTOA KUHUSU RUZUKU YA CUF UNATHIBITISHA HILO:
The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi) kimepokea kwa mshangao mkubwa ufafanuzi wa aibu uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi juu ya “WIZI” wa fedha za Umma zilizopaswa kutolewa kama Ruzuku ya Chama cha CUF kiasi cha Shilingi Milioni 369 ambazo yeye Msajili ameshiriki kikamilifu kupanga, kutoa na kuchotwa kwa fedha hizo. Tuliratajia Msajili angejitokeza hadharani na kuomba radhi na hata kujiuzulu wadhifa wake kwa kushiriki katika wizi huo wa wazi lakini badala yake anajaribu kufafanua mambo yasiyofafanulika. Huwezi kushiriki kwenye ubadhirifu wa fedha za umma kisha ukatafuta pa kujisafishia. Chama chetu kina uhakika na wizi huo na kina uhakika Jaji Mutungi amehusika kwa asilimia 100 huku akitambua kuwa kinachofanywa ni wizi;
Ameshindwa kujibu hoja za wizi huo;
1. Tunao ushahidi kuwa, wakati wizi huu unapangwa, Jaji Mutungi alikubaliana na wezi wenzake kuwa fedha hizo zisiwekwe kwenye akaunti Kuu ya CUF ambayo inatambulika na vikao halali vya CUF na ambayo mara zote Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa huweka fedha za Ruzuku humo.
2. Siku moja kabla Jaji Mutungi, Ofisi yake na wezi wenzake hawajatorosha fedha hizo – kwa maelekezo ya Jaji Mutungi, na huku akijua ni makosa kisheria na kikanuni, (wezi wenzie) waliwasiliana na viongozi wa CUF Temeke na (wezi hao) wakapewa hadhi ya kuwa watia saini kwenye akaunti namba 2072300456 ya Benki ya NMB tawi la Temeke ambayo inamilikiwa na ngazi ya Wilaya ya chama. Mpango huu mahsusi ulifanywa na Jaji Mutungi na wezi wenzake ili fedha hizo zisiwekwe kwenye akaunti kuu ya chama na hivyo iwe rahisi kuzitorosha bila mamlaka zenye dhamana na masuala ya fedha na mali za chama (yaani Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini) kujua wala kuidhinisha. Aliyekuwa anawezesha michakato yote hii ni Mutungi.
3. Mbinu aliyotumia Msajili wa vyama vya siasa kushiriki katika wizi na utoroshaji wa fedha hizi za CUF siyo mpya sana, mwezi Oktoba mwaka 2016, bila aibu wala kufuata utaratibu wala kuheshimu vyombo vinavyosimamia masuala ya fedha ndani ya CUF, Msajili wa Vyama vya Siasa, alimuandikia Meneja wa NMB Tawi la Ilala akimtaka amfungulie Ibrahim Haruna Lipumba, akaunti ya Benki yenye jina la ‘The Civic United Front”. Chama chetu kilifanikiwa kuzuia njama za wizi huo na hicho kilikuwa kipimo tosha kwamba Jaji Mutungi anatafuta kila mbinu kutorosha fedha za CUF na kuziweka kwenye akaunti yoyote ile ilimradi akaunti hiyo iwe na Jina la ‘The Civic United Front”. Utaratibu na “uhuni” huu wa Jaji Mutungi ni kinyume kabisa na Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama vya siasa, ndiyo maana hata siku moja hajawahi kuchukua fedha za CCM akaziweka kwenye akaunti ya CCM ya wilaya ya Ilala na kuzipuuza akaunti kuu za CCM.
4. Ukisoma Katiba ya CUF ambayo Jaji Mutungi anajidai kuisimamia katika kubariki baadhi ya uhuni anaoufanya dhidi ya CUF, kifungu cha 93(1) (i) kinaelekeza kuwa “Katibu Mkuu wa CUF ndiye muwajibikaji wa mambo yote ya fedha na mali za Chama katika ngazi ya Taifa (Chief Accounting Officer)” na ndiyo maana mwezi Oktoba mwaka 2016, mbinu ya Msajili ya kumpa fedha Lipumba ilipokwama, Msajili haraka sana akamuandikia Katibu Mkuu wa CUF kwa anwani ya Makao Makuu ya chama Zanzibar akimjulisha kuwa amesitisha utoaji ruzuku kwa CUF kwa sababu kuna mkanganyiko mkubwa kwenye uongozi (bila kujali kuwa anayeleta mkanganyiko huo ni yeye Msajili mwenyewe).
5. Mwaka jana mwezi Oktoba pia, Msajili wa Vyama vya Siasa aliwaandikia Makatibu Wakuu wote wa Vyama vya siasa vinavyopokea Ruzuku nchini, kupitia anwani za Makao Makuu za vyama hivyo na kuwajulisha kuwa wampe akaunti maalum za vyama ambazo serikali itakuwa ikiweka ruzuku na kwamba akaunti hizo zisiwe zinahusika na uwekaji wa fedha zingine za chama. Katibu Mkuu pia alipokea barua hiyo kupitia anwani ya Makao Makuu ya chama ambayo yako Zanzibar, kisha akaiomba bodi ya Wadhamini ikutane na kuidhinisha akaunti kuu maalum kwa mujibu wa maelekezo ya Msajili. Kisha Katibu Mkuu alimuandikia Msajili na kumpa akaunti hiyo Kuu kwa mujibu wa vigezo alivyotaka Msajili. Hii ni kwa ajili ya kuwaonesha kuwa Jaji Mutungi anazo akili timamu na anazitumia kila mara akiwa na malengo maalum. Mutungi anaujua utaratibu wa mawasiliano yanayohusu fedha kwa vyama vya siasa lakini kwa CUF ameamua kuyapuuza kwa manufaa ya walomtuma. Katika hili la wizi na utoroshaji wa fedha, hakuwahi kumwandikia Katibu Mkuu lakini amelitekeleza.
6. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura 258 (The Political Parties Act No. 5 of 1992) kwenye kifungu cha 15 (1), kila chama cha siasa kupitia BODI YAKE YA WADHAMINI kinapaswa kumiliki akaunti ya Benki na pesa zote zinazoingia katika chama kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria hiyo (ikiwemo Ruzuku ya kutoka serikalini) zinapaswa kuingizwa katika akaunti hiyo. Hili ni takwa la lazima la kisheria na si hiyari. Hadi Mutungi anatoa ufafanuzi wake wa kipuuzi, Bodi ya Wadhamini ya CUF yenye mamlaka ya kisheria katika udhibiti wa akaunti za chama cha siasa, haina taarifa na haikuidhinisha akaunti ya CUF Wilaya ya Temeke iwekewe fedha zozote za Ruzuku ya CUF.
7. Jaji Mutungi ni mpuuzi, anasema “ofisi yake inaamini kuwa ndani ya CUF hakuna mgogoro”, hii ni kauli ya mtu mwenye hadhi ya Jaji! Ni huyu huyu Jaji Mutungi ndiye mwaka jana tarehe 10 Oktoba amemuandikia Katibu Mkuu wa CUF kuwa anasitisha ruzuku ya CUF kwa sababu kuna mgogoro ndani ya CUF na akaonesha kuwa zipo pande mbili zinazoiandikia ofisi yake zikivutana. Leo, baada ya Mutungi kufanikisha wizi wa ruzuku ya CUF, anasimama hadharani na kusema CUF hakuna mgogoro, huu ni upuuzi wa ‘kiwango cha PhD’ kufanywa na mwenye hadhi ya Ujaji. Na, je kesi iliyoko mahakamani na ambayo yeye Msajili ni Mlalamikiwa namba moja anaichukulia kama bonanza au? siyo Mgogoro, tena uliotengenezwa nayeye kwa maslahi anayoyajua?
8. Mutungi anasema ametoa Ruzuku ya chama kwa uongozi wa CUF unaotambuliwa. Ni upi huo? Unawezaje kutoa fedha za chama cha siasa ukawapa watu waliofukuzwa ndani ya chama hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali anavyokuja kuikagua CUF atamuita Katibu Mkuu wa chama na si mtu mwingine, Katibu Mkuu hawatambui hawa waliopewa hizo fedha. Jaji Mutungi ndiye atakuja kutoa maelezo ya matumizi ya fedha hizo? Jaji Mutungi leo kajitia wazimu wa kutokuijua katiba ya CUF? Na kwamba Katibu Mkuu wa Chama si kiongozi halali wa CUF?
9. Mutungi anasema mgogoro wa ndani ya CUF ulishamalizwa na tangu mwaka jana alipotoa muongozo kwa CUF kuwa Lipumba ni Mwenyekiti halali. Hivi hizi ni akili timamu? Maamuzi yale ya Mutungi yalifanywa kinyume kabisa na Katiba ya CUF, kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa na kinyume na maamuzi mbalimbali ya Mahakama Kuu yaliyowahi kufanyika juu ya mamlaka yake. Mutungi hakuwa na mamlaka ya kufanya alichokifanya na kilichotokea ndicho alichokuwa ametumwa kukitengeneza. Leo Mutungi anasema CUF haina mgogoro wowote! Yeye mdiye aliyeiandikia CUF kuzuia ruzuku kwa kusema kuna mgogoro tumuulize mgogoro huo umemalizika lini na kesi ipo mahakamani? Huyu naye ni Jaji wa Mahakama Kuu!!!!
10. Chanzo chetu cha taarifa kimetuhakikishia kwamba, katika Shilingi Milioni 369 zilizotoroshwa na Mutungi na wezi wenzake, Mutungi ameshagawiwa asilimia 25% ya fedha hizo kama gawio la kufanikisha wizi huo. Chama kinazichukulia taarifa hizo kwa uzito mkubwa na tunaendelea na uchunguzi wa namna alivyopata gawio hilo. Tunaahidi kuwa tukikamilisha suala hilo tutaita vyombo vya habari na kuweka kila kitu hadharani. Jambo moja ambalo tunazidi kulihakikisha ni kuwa, Jaji Mutungi hana rekodi nzuri katika masuala ya fedha za umma, tutatoa taarifa za kina juu ya ushiriki wake kwenye ‘kuhonga’ vyama mbalimbali ili vishiriki uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016.
Mwisho;
Tunawataka wanachama CUF, wapenzi na wapenda mabadiliko kwa ujumla kuondoa wasiwasi na kuendelea kuwa na subira. CUF ni taasisi makini na imara ya kisiasa nchini. Wanasheria wanaendelea kukamilisha taratibu mbalimbali za hatua za kisheria dhidi ya wezi wote. Na wakati ukifika Tutazungumza yote hayo ili watanzania watambue kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa sasa inaongozwa na mtu hatari kwa ustawi wa demokrasia nchini na ni mtu wa hovyo kupita kiasi.
HAKI SAWA KWA WOTE
____________________________________
MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA