Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Nimemsikiliza Rais wangu kwa utulivu, wakati akizungumza kwenye ghafla ya kupokea ripoti ya uchaguzi ya NEC,hasa alipogusia kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya iliopendekezwa.
Tafakuri zangu zimepelekea kudadisi Katiba pendekezwa na upigaji wa kura ya maoni hususan upatikanaji wa 2/3 wajumbe wa Baraza la wawakilishi na wabunge kutoka Zanzibar ili kura hiyo ipate ridhaa.
Nilimsoma Maalim Seif, tabia na vitendo vyake na bila ya shaka yeyote ana mkono wa kila kandamizi zinazopata Zanzibar kutoka bara:-
1.Katika mwaka 1984 wakati Rais wa Zanzibar Alhaj Jumbe akisaidiwa na mwanasheria wa Tanzania Wolfgang Dourado na Mwanasheria Mkuu Bw. Swanzi walipopanga mkakati wa kuitoa Zanzibar kwanye dhulma ya kutawaliwa(out of bondage) na bara na kuwa na muungano wa kuheshimiana na usawa;Maalim Seif kama moto wa kifuu alimnyonyoa Rais Jumbe na kumwita mhaini na mpinga muungano, kitendo kilichopelekea Jumbe kunyofolewa wadhifa zake zote. Wazanzibari wakarejea tena kwenye Mamlaka ya Tanganyika.
2. Katika mwaka 1995 baada ya mtafaruku wa uchaguzi uliompa ushindi Dr.Salmin Amour (komandoo)Maalim Seif alifanya kikao cha siri na Mwl.Nyerere na hata alipotakiwa hata na chama chake kuwaeleza walichozungumza alikataa zaidi ya kusema " siri yetu". Aliwaambia wafuasi kuwa Dr. Salmini hatofikisha miaka mitano. Aliwabakisha wafuasi wake kubaki na tamaa mpaka mihula yote miwili ikamalizika!
3.Katika mwaka 2015, matokeo ya uchaguzi yasio rasmi yalelekea kumpa ushindi Maalim Seif, CUF ikahemkwa kwa shangwe za ushindi, lakini shangwe hizo zikazimwa na AlhajJecha. Mikutano ya kutafutwa muafaka ilianza. Maalim Seif hakutaka mtu kutoka chama chake kushiriki katika majadiliano. Mshiriki mmoja wa mkutano huo Balozi Seif wa CCM alipohojiwa kinachoendelea kwenye mkutano, alisema " ....nasikia uchaguzi kurudiwa tu ...." Hata Maalim Seif alipoulizwa kuhusu hili la kurejewa kwa uchaguzi alikataa.
4.Katika hatua isiopimika aliwataka wafuasi wake wasishiriki katika uchaguzi wa marudio na walimtii kikamilifu.CUF ikapoteza nafasi zote za kisiasa unguja na Pemba na kuwahadaa tena kuwa Dr. Shein hatofika miaka mitano.
5. Maalim Seif anaendelea kupata mafao yake kikamilifu na hata ya upendeleo
Kizingiti kikubwa ya kukwamisha kupita kwa kura ya maoni na hatimae Katiba pendekezwa ilikuwa ni kura ya turufu(2/3) ya wazanzibari. Sasa pingamizi hiyo haipo na imeeondolewa kidiplomasia na Maalim Seif.
Faradhi ya watu wa Zanzibar imewadia, na kugongomelea msumari wa mwisho wa jeneza kunasubiri nyundo ya mwisho.. Dalali ameshapiga Handek,amelipa ngapi?
Wana CUF mnyang'anyeni nyundo Maalim Seif na mkabidhini Pro.Lipumba awanusuru Wazanzibari kumalizwa rasmi