CUF imeiuza Zanzibar, Maalim Seif ndio dalali

Kizingiti kikubwa ya kukwamisha kupita kwa kura ya maoni na hatimae Katiba pendekezwa ilikuwa ni kura ya turufu(2/3) ya wazanzibari
Ni mimi ndo nimesahau; au?! Ni 2/3 ipi unaizungumzia hapa?! For what I know 2/3 ya Law Makers ilishapita na kura ya maoni iliyosalia ni ya wananchi! Refer simulizi za wabunge kupiga kura wakiwa Hijja na wengine wakiwa kitandani kwa ugonjwa!

Kuhusu Maalim Seif; naungana na wewe! Watu tunapenda tu siasa za kishabiki; lakini Maalim Seif ni jipu ndani ya CUF ingawaje amefanikiwa kuishika! Kwanza hizi siasa za kususa susa CCM wala hawajali... na ndio maana nimeshawahi kuwahoji CHADEMA hapa ikiwa wameshawahi kufanya impact assessment ya staili yao ya kususia vikao vya bunge! CCM wala hawaoni aibu kubaki peke yao bungeni hata kwa miaka 10 yote; kwahiyo ukiwasusia ndo kwanza wanafurahi....
 
Kususa ni moja ya adhabu kwa mwenye kususiwa na kwaalie muungwana name ndio maana kwa silaha hii kila siku inayopita ya M/Mungu watu wanaoichukia CCM wanadhidi kuongezeka..

Kumbuka hii tabia ya kususia na kuwabagua watu hawakuianzisha CUF au wapemba! Bali watawala.

Niwao walioanza kuwafukuza watu makazini Kwa kisingizio cha siasa, niwao waliokuwa wakiwakataa watu na kuwanyima khaki zao za msingi zikiwemo za kupata ajira, vitambulisho vya ukaazi, khaki ya kupiga kura n. k.

Kumbuka siku zote usimfundishe PANYA KULA USUFI maana akijua itakuwa hatari kwako, sasa PANYA ni bingwa wa kula usufi!! Mwisho Mh. Karume alijitahidi kuyaondoa haya na kwa kiasi Fulani alifanikiwa!! Lakini CCM wakaona hana maana hivyo wakaamua kuwarudisha wazanzibar kule kule enzi za uhasama maana kwao madaraka kwao ni bora kuliko hata umoja wa wazanzibar!!
 
niliwahi kuandika humu kwamba watu wasikurupuke kwanza wa msome Seif Sharif Hamad katika historia yake ya siasa na hasa siasa za zanzbar wengi waka beza na kutoa maneno ovyo ukiwemo wewe ndugu yangu Barghash!
 
Kususa ni moja ya adhabu kwa mwenye kususiwa na kwaalie muungwana name ndio maana kwa silaha hii kila siku inayopita ya M/Mungu watu wanaoichukia CCM wanadhidi kuongezeka..

Kumbuka hii tabia ya kususia na kuwabagua watu hawakuianzisha CUF au wapemba! Bali watawala.

Niwao walioanza kuwafukuza watu makazini Kwa kisingizio cha siasa, niwao waliokuwa wakiwakataa watu na kuwanyima khaki zao za msingi zikiwemo za kupata ajira, vitambulisho vya ukaazi, khaki ya kupiga kura n. k.

Kumbuka siku zote usimfundishe PANYA KULA USUFI maana akijua itakuwa hatari kwako, sasa PANYA ni bingwa wa kula usufi!! Mwisho Mh. Karume alijitahidi kuyaondoa haya na kwa kiasi Fulani alifanikiwa!! Lakini CCM wakaona hana maana hivyo wakaamua kuwarudisha wazanzibar kule kule enzi za uhasama maana kwao madaraka kwao ni bora kuliko hata umoja wa wazanzibar!!
Umeanza vema kwamba "kususa ni moja ya adhabu kwa mwenye kususiwa na kwa alie muungwana!" Na ikiwa umenisoma vizuri nilitangulia kusema kwamba CCM hawajali wala kuona soni linapokuja suala la kususiwa kwa sababu huo uungwana wa kisiasa CCM hawana!! Nishawahi kuzungumza hapa mara kadhaa kwamba kususa kwenye tija ni kule ambako mwenye kususiwa angalau atashituka lakini kuisusia CCM ni kunaakisi ule msemo wa mitaani, kwamba "ni sawa na kumsusia fisi bucha iliyojaa nyama!" Kwa CCM hapo nyama hiyo ataitengeneza supu; nyama choma, ya mchuzi n.k kisha atashushia maji bila ya soni-- na ukitokea atakuuliza "vp umekula nyama...?" Atakuuliza hivyo ili hali wanafahamu wameiponda hadi mifupa na hawajasaza japo pune... kwavile HAWAJALI na uungwana wa kisiasa hawanao! Matokeo yake ni kwamba; mara zote linapokuja suala la kususa anayenufaika ni CCM na wataendelea kunufaika kv hadi sasa ni kama Upinzani hawajapata best alternative ya ku-deal na CCM! Kususa haijawahi kutoa good results zaidi ya kuinufaisha CCM!
 
Nashukuru kwa kuuweka ukweli hadharani, siku zote maalim Seif alikuwa anatanguliza maslahi yake binafsi kwanza badala ya maslahi ya wananchi wake wanaomwamini kama kurejeshewa mafao ya waziri kiongozi na sasa makamu wa kwanza wa rais.Hata mwaka 2010 inasemekana alishinda uchaguzi ila alikubali kuachia nafasi hiyo baada ya kuahidiwa umakamu wa kwanza wa rais.Katika mazungumzo yaliyofanyika baada ua uchaguzi huu alikuwa akizungumza bila viongozi wenzake wa chama kujua nini kinazungumzwa fikiria alikuwa akizungumza na marais wote wastaafu huku akiwa yeye pekee.Ni wakati umefika kwa CUF kuanza safari mpya bila yeye.
 
Kususa ni moja ya adhabu kwa mwenye kususiwa na kwaalie muungwana name ndio maana kwa silaha hii kila siku inayopita ya M/Mungu watu wanaoichukia CCM wanadhidi kuongezeka..

Kumbuka hii tabia ya kususia na kuwabagua watu hawakuianzisha CUF au wapemba! Bali watawala.

Niwao walioanza kuwafukuza watu makazini Kwa kisingizio cha siasa, niwao waliokuwa wakiwakataa watu na kuwanyima khaki zao za msingi zikiwemo za kupata ajira, vitambulisho vya ukaazi, khaki ya kupiga kura n. k.

Kumbuka siku zote usimfundishe PANYA KULA USUFI maana akijua itakuwa hatari kwako, sasa PANYA ni bingwa wa kula usufi!! Mwisho Mh. Karume alijitahidi kuyaondoa haya na kwa kiasi Fulani alifanikiwa!! Lakini CCM wakaona hana maana hivyo wakaamua kuwarudisha wazanzibar kule kule enzi za uhasama maana kwao madaraka kwao ni bora kuliko hata umoja wa wazanzibar!!
Naona nikukumbushe aliyeanza kuwafukuza watu makazini ni Seif Sharif wakati huo yupo waziri kiongozi na kwa bahati majority waliofukzwa walikuwa ni watu wa Unguja na siku ya pili analetwa mtu katika nafasi ile huwa ni mpemba na ali disguise huo ujanja ati watu wanacherewa makazini na watu walifukuzwa makazini bila kufuta sharia za utumishi serikalini.
Na ubaguzu mwengine seif alofanya wakati yupo waziri wa elimu na watu hawajasahau mpaka leo.. aliandaa mfumo wa kuzigawa nafasi za kusoma nusu unguja na nusu Pemba huku akisahau ya kuwa population kubwa ipo unguja na akafanya ujanja zile nafasi za Unguja anawapa wapemba waliozaliwa unguja au wanaokaa unguja na matokeo yake 80% huzo nafasi huenda kwa wapemba. lakini tatizo lenu mna memory ndogo sana nyote mnazungumzia 1995.. huo basi siyo mwanzo wa matatizo..Matatizo ameyaanzisha yeye mwenyewe Seif.
 
Kila anaemfanyia nwenzake ubaya hatuonja umauti hadi ubaya hule umrudie zaidi ya yule aliefanyia
uharamia wote unaofanyika zanzibar unapikwa na watanganyika wakae wakijua kwamba utawarudia ubaya mkubwa zaidi ya waliowafanyia wazanzibari
muda utapotamalaki
 
Lipumba ana uchungu na CUF kuliko Maalim Seif. Maalim ana uchungu zaidi na maslahi yake binafsi!
Mbona Lipumba kafundishwa na Maalim kuhusu maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano.
Naona mkwezi wewe umeamua kukwea mnazi huku umevaa ndala. CUF ni ya Seif.
 
Nimemsikiliza Rais wangu kwa utulivu, wakati akizungumza kwenye ghafla ya kupokea ripoti ya uchaguzi ya NEC,hasa alipogusia kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya iliopendekezwa.

Tafakuri zangu zimepelekea kudadisi Katiba pendekezwa na upigaji wa kura ya maoni hususan upatikanaji wa 2/3 wajumbe wa Baraza la wawakilishi na wabunge kutoka Zanzibar ili kura hiyo ipate ridhaa.

Nilimsoma Maalim Seif, tabia na vitendo vyake na bila ya shaka yeyote ana mkono wa kila kandamizi zinazopata Zanzibar kutoka bara:-

1.Katika mwaka 1984 wakati Rais wa Zanzibar Alhaj Jumbe akisaidiwa na mwanasheria wa Tanzania Wolfgang Dourado na Mwanasheria Mkuu Bw. Swanzi walipopanga mkakati wa kuitoa Zanzibar kwanye dhulma ya kutawaliwa(out of bondage) na bara na kuwa na muungano wa kuheshimiana na usawa;Maalim Seif kama moto wa kifuu alimnyonyoa Rais Jumbe na kumwita mhaini na mpinga muungano, kitendo kilichopelekea Jumbe kunyofolewa wadhifa zake zote. Wazanzibari wakarejea tena kwenye Mamlaka ya Tanganyika.

2. Katika mwaka 1995 baada ya mtafaruku wa uchaguzi uliompa ushindi Dr.Salmin Amour (komandoo)Maalim Seif alifanya kikao cha siri na Mwl.Nyerere na hata alipotakiwa hata na chama chake kuwaeleza walichozungumza alikataa zaidi ya kusema " siri yetu". Aliwaambia wafuasi kuwa Dr. Salmini hatofikisha miaka mitano. Aliwabakisha wafuasi wake kubaki na tamaa mpaka mihula yote miwili ikamalizika!

3.Katika mwaka 2015, matokeo ya uchaguzi yasio rasmi yalelekea kumpa ushindi Maalim Seif, CUF ikahemkwa kwa shangwe za ushindi, lakini shangwe hizo zikazimwa na AlhajJecha. Mikutano ya kutafutwa muafaka ilianza. Maalim Seif hakutaka mtu kutoka chama chake kushiriki katika majadiliano. Mshiriki mmoja wa mkutano huo Balozi Seif wa CCM alipohojiwa kinachoendelea kwenye mkutano, alisema " ....nasikia uchaguzi kurudiwa tu ...." Hata Maalim Seif alipoulizwa kuhusu hili la kurejewa kwa uchaguzi alikataa.

4.Katika hatua isiopimika aliwataka wafuasi wake wasishiriki katika uchaguzi wa marudio na walimtii kikamilifu.CUF ikapoteza nafasi zote za kisiasa unguja na Pemba na kuwahadaa tena kuwa Dr. Shein hatofika miaka mitano.

5. Maalim Seif anaendelea kupata mafao yake kikamilifu na hata ya upendeleo

Kizingiti kikubwa ya kukwamisha kupita kwa kura ya maoni na hatimae Katiba pendekezwa ilikuwa ni kura ya turufu(2/3) ya wazanzibari. Sasa pingamizi hiyo haipo na imeeondolewa kidiplomasia na Maalim Seif.

Faradhi ya watu wa Zanzibar imewadia, na kugongomelea msumari wa mwisho wa jeneza kunasubiri nyundo ya mwisho.. Dalali ameshapiga Handek,amelipa ngapi?

Wana CUF mnyang'anyeni nyundo Maalim Seif na mkabidhini Pro.Lipumba awanusuru Wazanzibari kumalizwa rasmi
Mkuu Salaam kwanza

Kama kawaida unadhihirisha chuki zako binafsi kwa Maalim seif kwa mara nyengine tena. Bahati mbaya unamzulia na kuwafanya wengine waamini hayo mawazo yako kuwa ndio ukweli.

Tuanze taratibu tu. Suala la kura ya maoni ya hio katiba pendekezwa ambayo umeguswa nayo baada ya rais kugusia Katiba imepelekea bila kujijuwa ukiona unamshambulia Maalim bure. Umesahau kuwa CUF walikuwemo kwenye Bunge la katiba na wajumbe wa Zanzibar walikuwemo lakini mazingaombwe yaliyofanyika hadi kupatikana katiba pendekezwa unajifanya kusahau. Kwa hivyo kuwepo CUf au kutokuwepo haizuwii mtawala kufanya anavyotaka.

Suala la jumbe na muungano unaendelea kushirikiana na maadui wa Maalim Seif kumzushia bila ushahidi. Tuwekee ushahidi wa wazi vipi maalim Seif alihusika kufukuzwa kwa Jumbe na hatutaki hekaya za Waraka ulioibwa kwa siri kama baadhi ya wahafidhina wanavyozusha. Suala hili alishawahi kukanusha mwenyewe lakini naona bado mnaliendeleza pasi na ushahidi wa kweli.

Suala la uchaguzi wa 1995. Yaani tuweke wazi ina maana mazungumzo yake na nyerere yalikuwa kwamba akubali kushindwa au una habari gani tuweke wazi pengine na wewe uliota kilichozungumzwa. Una maana gani au ndio alisaliti tufahamishe kwa uwazi.

Uchaguzi wa 2015 ndio unazidi kabisa kuonesha chuki. Ni wapi maalim alisema wenzake wasishiriki kwenye mazungumzo. Aina ya mazungumzo aliyasisi yeye kama kiongoz /Makamo wa kwanza kutaka kuonana na rais wakati ule kujadili namna ya kuondowa sintofahamu. Hapa akiwa kama kiongozi wa nchi na si katibu wa chama. Kumbuka hakukuwa na maazimio ya vyama si CUf wala CCm viliamuwa kutaka kikao hilo ulijuwe. Pili Rais Shein hakujiamini alitaka washiriki viongozi (marais wastaafu wa zanzibar) labda umesahau. Nikwambie hata hivyo mashauri yote ya mwenendo wa kikao hicho yalikuwa na baraka ya chama chake na akipata ushauri wa kitaalamu na kisheria kwa kila hatua. wewe unakuja na chuki zako tu.

NOTE: suala la Zanzibar ni nyeti na muungano ni zao la maridhiano, Hatua zozote za kutumia hilba na nguvu hazitaufanya muungano huu kustawi na kudumu.

Kwa ujumla unamchukia Maalim bure na sasa unaona Lipumba ni shujaa wa Zanzibar kweli kila mtu na ufahamu wake. Maalim ni alama ya mapambano ya kweli ya Zanzibar na watawala wanaumiza kichwa.

Binafsi sikatai kuwa Maalim ana mapungufu yake kama binadamu lete mapungufu yake lakini usimzulie mzee wa watu
 
Naona nikukumbushe aliyeanza kuwafukuza watu makazini ni Seif Sharif wakati huo yupo waziri kiongozi na kwa bahati majority waliofukzwa walikuwa ni watu wa Unguja na siku ya pili analetwa mtu katika nafasi ile huwa ni mpemba na ali disguise huo ujanja ati watu wanacherewa makazini na watu walifukuzwa makazini bila kufuta sharia za utumishi serikalini.
Na ubaguzu mwengine seif alofanya wakati yupo waziri wa elimu na watu hawajasahau mpaka leo.. aliandaa mfumo wa kuzigawa nafasi za kusoma nusu unguja na nusu Pemba huku akisahau ya kuwa population kubwa ipo unguja na akafanya ujanja zile nafasi za Unguja anawapa wapemba waliozaliwa unguja au wanaokaa unguja na matokeo yake 80% huzo nafasi huenda kwa wapemba. lakini tatizo lenu mna memory ndogo sana nyote mnazungumzia 1995.. huo basi siyo mwanzo wa matatizo..Matatizo ameyaanzisha yeye mwenyewe Seif.

Huu ni mwendelezo wa hekaya za kale. Watu wanajadili hoja mnakuja na maigizo ya zamani. Serikali sio mtu mmoja. By the way maalim alikuwa waziri juu yake kuna rais na kulikuwa na mawaziri mchanganyiko. Maamuzi hawezi kufanya peke yake na kuwa ndio sera ya serikali nzima kwa nini aliachwa afanye hivyo bila kukemewa na kuchukuliwa hatua(lete ushahidi sio stori)

umakini wa Maalim ndio uliopelekea kupanda vyeo kuanzia serikalini mpaka chamani(wakati huo CCM)

Baada ya wapinzani wake kukosa hoja walikimbilia mawazo mfu kugeuza uchapa kazi wake kutengenezwa kuwa majungu.

Seif anabaki vile vile wa uhodari na umakini
 
Wacha kutudanganya wewe.. Seif sharif amepanda vyeo baada kuamuwa kuwa puppet wa nyerere na kumuuza Aboud jumbe.Kama hizo ni hikaya basi kwako wewe tu kwa sababu huna hata idea ya nini kilikuwa kinatokea wakati huo na ndiyo maana juu ya kuungwa mkono na Ali Hassam Mwinyi mwaka 1985 alikosa kiura za kuteuliwa na Ijapokuwa zililazimishwa kura mara tatu( ndiyo Uchaguzi pekee ndani ya CCM kura zilipigwa mara tatu) lakini matokeo yake alikosa kiti cha kugombea uraisi baada ya kukosa tu ndiyo hapo alipodhihirisha rangi yake..na akatoka kuwa rafiki mkubwa sana wa mwinyi na kuwa adui yake No moja. Huyo Mwinyi wa leo mnaosema kaiuza ZNZ basi alipigania kwa hali na mali ndani ya CCM ili SEif awe Rais wa ZNZ. Lakini kutokana na madudu aliyoyafanya ya ubaguzi kwa watu wa unguja na Uchu wa madaraka akashindwa.
Sasa wewe endelea kuleta ngonjera zako na naona mmeshaanza kuchanganyikiwa.
 
Mkuu Salaam kwanza

Kama kawaida unadhihirisha chuki zako binafsi kwa Maalim seif kwa mara nyengine tena. Bahati mbaya unamzulia na kuwafanya wengine waamini hayo mawazo yako kuwa ndio ukweli.

Tuanze taratibu tu. Suala la kura ya maoni ya hio katiba pendekezwa ambayo umeguswa nayo baada ya rais kugusia Katiba imepelekea bila kujijuwa ukiona unamshambulia Maalim bure. Umesahau kuwa CUF walikuwemo kwenye Bunge la katiba na wajumbe wa Zanzibar walikuwemo lakini mazingaombwe yaliyofanyika hadi kupatikana katiba pendekezwa unajifanya kusahau. Kwa hivyo kuwepo CUf au kutokuwepo haizuwii mtawala kufanya anavyotaka.

Suala la jumbe na muungano unaendelea kushirikiana na maadui wa Maalim Seif kumzushia bila ushahidi. Tuwekee ushahidi wa wazi vipi maalim Seif alihusika kufukuzwa kwa Jumbe na hatutaki hekaya za Waraka ulioibwa kwa siri kama baadhi ya wahafidhina wanavyozusha. Suala hili alishawahi kukanusha mwenyewe lakini naona bado mnaliendeleza pasi na ushahidi wa kweli.

Suala la uchaguzi wa 1995. Yaani tuweke wazi ina maana mazungumzo yake na nyerere yalikuwa kwamba akubali kushindwa au una habari gani tuweke wazi pengine na wewe uliota kilichozungumzwa. Una maana gani au ndio alisaliti tufahamishe kwa uwazi.

Uchaguzi wa 2015 ndio unazidi kabisa kuonesha chuki. Ni wapi maalim alisema wenzake wasishiriki kwenye mazungumzo. Aina ya mazungumzo aliyasisi yeye kama kiongoz /Makamo wa kwanza kutaka kuonana na rais wakati ule kujadili namna ya kuondowa sintofahamu. Hapa akiwa kama kiongozi wa nchi na si katibu wa chama. Kumbuka hakukuwa na maazimio ya vyama si CUf wala CCm viliamuwa kutaka kikao hilo ulijuwe. Pili Rais Shein hakujiamini alitaka washiriki viongozi (marais wastaafu wa zanzibar) labda umesahau. Nikwambie hata hivyo mashauri yote ya mwenendo wa kikao hicho yalikuwa na baraka ya chama chake na akipata ushauri wa kitaalamu na kisheria kwa kila hatua. wewe unakuja na chuki zako tu.

NOTE: suala la Zanzibar ni nyeti na muungano ni zao la maridhiano, Hatua zozote za kutumia hilba na nguvu hazitaufanya muungano huu kustawi na kudumu.

Kwa ujumla unamchukia Maalim bure na sasa unaona Lipumba ni shujaa wa Zanzibar kweli kila mtu na ufahamu wake. Maalim ni alama ya mapambano ya kweli ya Zanzibar na watawala wanaumiza kichwa.

Binafsi sikatai kuwa Maalim ana mapungufu yake kama binadamu lete mapungufu yake lakini usimzulie mzee wa watu
Aleikum salam Mkuu

Umejitahidi kuutetea usaliti na ulichobakisha nikuupaka rangi tu. Mimi sijawahi na wala sitowahi kumchukia mtu kwa mtizamo wa mambo anayoyafanya kama hayatagusa uhuru wa mtu au jamii nyengine.Lakini ni wazi pia sitampigia zumari, mcheza kumbwaya ambapo najua mchezo wake ndio maangamizi yetu. Nitamsema tu

1. Kumbuka kufanyika kwa kura ya maoni kunahitajika ridhaa ya 2/3 ya baraza la wawakilishi. Sizungumzii upitishwaji wa Katiba pendekezwa.Sasa kura ya maoni inapita kwa asilimia moja 100% wala hiyo ghilba mara hii haihitajiki kufanyika. Unasema kuwepo CUf au kutokuwepo haizuwii mtawala kufanya anavyotaka. Ni sawa na kusema kuwa hakuna maana, mantiki au uhalali wa kuwepo chama cha CUF kabisa
2.Kuhusu kusalitiwa Jumbe, nitafuta kauli zangu zote kama Maalim Seif atakataa hakutamka wala hakumwita Wolfgang Dourado kuwa ni mhaini, na Rais Jumbe anataka kuvunja muungano. Lakini nayakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyoyasema Lumumba College katika mikutano yake ya kutuliza kuchafuka kwa hali ya kisiasa na nanukuu " .... tokea nilipoingia kwenye " system" kila siku napokea ujumbe mbali mbali, kutoka International Amnesty.... ikitutaka tumuachie huru Dourado.....eti kidurado......mhaini...." mwisho wa kunukuu.Dourado alipotoka kifungoni alimfuata Maalim Seif na kumuuliza amwambie uhaini wake!
3.Kuhusu mkutano wake wa siri na Nyerere hajawahi kueleza waziwazi kipi walizungumza ili alisema tu tena kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti kuwa ni " Siri yetu". Tabia hii ya usiri hata kwa wenzake ameizowea sana ambayo inayoambatana na ubishi na hivyo hata kuasiana na wenzake, Hamad Rshid ni mfano hai.
4.Eti mashauri yote ya mwenendo wa kikao hicho yalikuwa na baraka ya chama chake na akipata ushauri wa kitaalamu na kisheria kwa kila hatua.Usiwatukane wanasheria makini wa CUF kutetea ujuha wako. Hakuna mwanasheria mwenye taaluma atakaependekeza kumwacha Maalim Seif peke yake akiiwakilishe CUF wakati CCM ikiwakilishwa na wanasiasa wakongwe wenye uzoefu watano (5) na muhusika mtuhumiwa kuwa Mwenyekiti wa Vikao.
5. NOTE: suala la Zanzibar si nyeti na muungano si zao la maridhiano, Hatua zozote za kutumia hilba na nguvu zitaufanya muungano huu kustawi na kudumu kwa gharama ghali ya kuzidi kupoteza uhuru na mustakabali wa watu wa Zanzibar.
6. Kwa ujumla simchukii Maalim bure ila ni kutokana na vitendo vyake vya kisaliti. Namuona Lipumba ni shujaa wa CUF kwa sababu hanunuliki! Maalim ni alama ya usaliti anaye dhihaki mapambano ya kweli ya Zanzibar na watawala wanafurahishwa na kukunwa na hatua zake.
 
Mbona Lipumba kafundishwa na Maalim kuhusu maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano.
Naona mkwezi wewe umeamua kukwea mnazi huku umevaa ndala. CUF ni ya Seif.
Graduate kumfundisha profesa,Bunge la Katiba! Kukwea mnazi huku umevaa ndala labda ulikuwa unagida tembo.

Ulitaka kusema Seif ni CUF na CUF ni Seif?
 
Haswaa!!! Huyo bwana ni kiongozi wa kiroho wa Wapemba. Akiamua kesho wapemba washinde wanatazama jua basi utekelezaji mara moja. Nafikiri cuf bado haijafika pabaya na mchango wa Lipumba ni muhimu hasa kwa mkakati wake wa kuijenga ngome huko kusini. Kusema eti hakuwapo tumeshinda ni kujidanganya kwani kazi ya kuijenga hiyo ngome ilikuwa si kazi ya miezi miwili ya kampeeni.
Mshaurini Maalim aelewe kama uchaguzi ufanyike au kuifuta barua na kumrejesha Lipumba yote kheri. Ila hizi kauli mnazokuja nazo hazifai kwa sasa.
 
Kama maalim Seif angekuwa na ukufi tu wa kujali maslahi yake binafsi basi tungeshamfukuza zamani kutoka Cuf. Sisi tunamwirika kwa saatul khabari (kitabu cha mambo ya dini) hata shati lake analolivaa, na mpaka watoto wake pia tunawachunguza kujua kama alau kuna yoyote alie na usaliti ama maslahi binafsi. Tunamjua seif tokea uchanga wake kwamba ni mtu mwema
Ramli kharamu shekhe! Hivi mkipewa nchi si itakua hatari na ramli zenu
 
Aleikum salam Mkuu

Umejitahidi kuutetea usaliti na ulichobakisha nikuupaka rangi tu. Mimi sijawahi na wala sitowahi kumchukia mtu kwa mtizamo wa mambo anayoyafanya kama hayatagusa uhuru wa mtu au jamii nyengine.Lakini ni wazi pia sitampigia zumari, mcheza kumbwaya ambapo najua mchezo wake ndio maangamizi yetu. Nitamsema tu

1. Kumbuka kufanyika kwa kura ya maoni kunahitajika ridhaa ya 2/3 ya baraza la wawakilishi. Sizungumzii upitishwaji wa Katiba pendekezwa.Sasa kura ya maoni inapita kwa asilimia moja 100% wala hiyo ghilba mara hii haihitajiki kufanyika. Unasema kuwepo CUf au kutokuwepo haizuwii mtawala kufanya anavyotaka. Ni sawa na kusema kuwa hakuna maana, mantiki au uhalali wa kuwepo chama cha CUF kabisa
2.Kuhusu kusalitiwa Jumbe, nitafuta kauli zangu zote kama Maalim Seif atakataa hakutamka wala hakumwita Wolfgang Dourado kuwa ni mhaini, na Rais Jumbe anataka kuvunja muungano. Lakini nayakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyoyasema Lumumba College katika mikutano yake ya kutuliza kuchafuka kwa hali ya kisiasa na nanukuu " .... tokea nilipoingia kwenye " system" kila siku napokea ujumbe mbali mbali, kutoka International Amnesty.... ikitutaka tumuachie huru Dourado.....eti kidurado......mhaini...." mwisho wa kunukuu.Dourado alipotoka kifungoni alimfuata Maalim Seif na kumuuliza amwambie uhaini wake!
3.Kuhusu mkutano wake wa siri na Nyerere hajawahi kueleza waziwazi kipi walizungumza ili alisema tu tena kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti kuwa ni " Siri yetu". Tabia hii ya usiri hata kwa wenzake ameizowea sana ambayo inayoambatana na ubishi na hivyo hata kuasiana na wenzake, Hamad Rshid ni mfano hai.
4.Eti mashauri yote ya mwenendo wa kikao hicho yalikuwa na baraka ya chama chake na akipata ushauri wa kitaalamu na kisheria kwa kila hatua.Usiwatukane wanasheria makini wa CUF kutetea ujuha wako. Hakuna mwanasheria mwenye taaluma atakaependekeza kumwacha Maalim Seif peke yake akiiwakilishe CUF wakati CCM ikiwakilishwa na wanasiasa wakongwe wenye uzoefu watano (5) na muhusika mtuhumiwa kuwa Mwenyekiti wa Vikao.
5. NOTE: suala la Zanzibar si nyeti na muungano si zao la maridhiano, Hatua zozote za kutumia hilba na nguvu zitaufanya muungano huu kustawi na kudumu kwa gharama ghali ya kuzidi kupoteza uhuru na mustakabali wa watu wa Zanzibar.
6. Kwa ujumla simchukii Maalim bure ila ni kutokana na vitendo vyake vya kisaliti. Namuona Lipumba ni shujaa wa CUF kwa sababu hanunuliki! Maalim ni alama ya usaliti anaye dhihaki mapambano ya kweli ya Zanzibar na watawala wanafurahishwa na kukunwa na hatua zake.

Naam

Bado unapita kwenye anga zile zile tu.

Kwanza tutangazie interest zako kuwa Wewe ni miongoni mwa mnaoamini kuwa Uchaguzi wa 2015 wa Zanzibar ulisatahili kufutwaii tujuwe tuazungumza na nani(Mimi siko upande huo) Unahalalishaje CUF kuingia kwenye uchaguzi wa hilba wa machi, 2016 ili Wawakilishi wa CUF wapatikane waende wakazuiye hiyo katiba na wakati hyuo huo mzigo badala ya kuiangushia CUF na Baraza kuu wewe unamtishwa zigo Maalim Seif (Hio ni chuki ingawa hutaki kukubali)

Halafu Kumbuka katiba ni mchakato hivyo uchafu uliofanywa kupitisha katiba pendekezwa huridhiki mpaka CUF ishiriki hatua yengine hata kama kulishakuwa na ubatili wa kupindishwa maamuzi kabla. Chuki yako iko wazi kwa mAALIM BAADA YA KUJADILI ISHU NA UOVU WA UTAWALA KWA HILO DUBWANA KATIBA LINALOLAZIMISHWA, wewe unamraruwa Maalim tu kwa chuki zako.

Kuhusu Kikao na Marais wastaafu juu ya uchaguzi wa 2015 hujajibu hoja. Nakushauri pitia tena maelezo yangu. Kwa ufupi Baraka za kuendelea na mazungumzo kama Makamo wa Rais kutaka kuinusuru Zanzibar na mkwamo kuzungumza na rais wake si suala la chama. Hata hivyo ni wazi chama kilielezwa kilichoendelea na kumbuka ilikuwa si initiatives za kichama.

Bado unamuhukumu Maalim kwa kauli za kisiasa. Kuhusu huyo Durado na kauli ya Uhaini inahusiana vipi na usaliti wa Maalim kwa Zanzibar hebu weka wazi usiweke jumla jumla tu kuwa Maalim ni Msaliti wa Zanzibar ( Weka wazi kwa ushahidi na si kwa kauli za kisiasa)

Unampamba Mwinyi leo, Dhamira ndio huhukumu. Siri ya Mwinyi na hata huyo Jumbe unaijuwa? Jiulize suali hili. Ikiwa Kulikuwa na dhamira njema kwa Mzee Mwinyi kwa Zanzibar tuangalie kafanya nini walau kunusuru umoja wa Wazanzibari? umezugwa na kurudiwa Uchaguzi mara tatu lakini hujuwi dhamira iliyojificha na kwa hivyo hupaswi kuhukumu kwa kufikiria tu.

Tuletee ushahidi concrete wa Usaliti wa Maalim kwa Zanzibar na hatutaki siasa za kihafidhina na chuki.
 
Maalim hatumchukii, na anapendwa mpaka na wanyama kwa taarifa yako. Nendeni kwa Mwenyezi Mungu mukamuombe ili watu wamchukie. Na yeyote yule atakaetokea kuwasemea wanyonge basi nyinyi kwenu atakuwa adui yenu
 
Tuletee ushahidi concrete wa Usaliti wa Maalim kwa Zanzibar
Nimekupa usaliti wa Maalim Seif ni wa kuzuia vuvugu la kujinasua na Tanganyika na waliosimamia vuguvugu hilo Jumbe,Dourado na Dr. Swanzi, kwa pamoja Maalim kwa kauli yake akawaita wahaini mbele ya kadamunasi ya wazanzibari na mbele ya Nyerere, unataka ushahidi gani? Ushahidi wa Kinyamwezi mimi sina!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom