CUF, CHADEMA watunishiana msuli kumrithi Rostam CCM yasema bado hawajajipanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, CHADEMA watunishiana msuli kumrithi Rostam CCM yasema bado hawajajipanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 25 July 2011 21:13 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  KILA MMOJA ATAMBA CHAMA CHAKE KUCHUKUA JIMBO, CCM YASEMA BADO HAWAJAPANGA

  Waandishi wetu

  SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza kuwa kiti cha Jimbo la Igunga liko wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rostam Aziz, vyama vya siasa vimeanza mbio za kuwania jimbo hilo.Rostam alijiuzulu ubunge wa Igunga Julai 13 mwaka huu, kutokana na kile alichokiita siasa uchwara ndani ya CCM, na wiki iliyopita Spika Makinda, alitangaza kuindikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuieleza kuwa kiti hicho cha ubunge, sasa kiko wazi.

  Hatua ya Spika Makinda kuijulisha Nec kuhusu kujiuzulu kwa Rostam, ni mwanzo wa mchakato wa kukijaza kiti hicho cha ubunge kilichokuwa kikikaliwa na kada huyo wa CCM kwa miaka 18 iliyopita.Baada ya taarifa hiyo ya Spika Makinda, Nec sasa itatakiwa kutangaza uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo ndani ya siku 90 kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

  Lakini katika kile kinachoonekana harakati za kukitwaa kiti hicho, vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, TLP, UDP, CCM na SAU, jana vililithibitishia gazeti hili kwamba vitasimamisha wagombea wao wa ubunge katika uchaguzi mdogo utakaotangazwa na Nec hivi karibuni.

  CUF yataja wagombea wao
  CUF kimetoa onyo kwa vyama vya upinzani kuwa ni bora vingeacha kugombea jimbo hilo kwa kuwa tayari chenyewe kimelitwaa.

  Katika kuonyesha majigambo, chama hicho kilisema kina nafasi kubwa ya kuchukua ushindi katika jimbo hilo kutokana na mgombea wao, Leopard Mahana, kuombwa na wananchi kugombea tena ubunge baada ya kubwagwa na Rostam kwenye uchaguzi wa mwaka jana.Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, CUF haitafanya kosa la kuliacha jimbo hilo tena.

  Alisema hayo muda mfupi baada ya kutoa rambirambi kwa Ubalozi wa Norway nchini kutokana tukio la vifo vya watu 93 vilivyotokana na milipuko ya mabomu nchini humo. “Vyama vya upinzani wasijidanganye kusimamisha mbunge katika jimbo hilo kutokana na chama chetu kuwa na nafasi kubwa ya kushinda kutokana na wananchi wa eneo hilo kumchagua kijana wetu kugombea jimbo hilo,” alitamba Lipumba na kuongeza:

  “Katika uchaguzi wa mwaka jana chama chetu ndio pekee kilichosimamisha mgombea kati ya vyama vya upinzani kushindana na Rostam, hivyo vyama vya upinzani kwa sasa vinapaswa kuachia nafasi kama vilivyofanya kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,”alisema Lipumba.

  Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Jimbo la Igunga lillikuwa na wagombea wawili ambao ni Rostam kupitia CCM pamoja na Mahana kupitia CUF.

  Chadema waja na Opesheni Chukua Igunga
  Kwa upande wake,Chadema kimesema kitaweka mipango yake hadharani hivi karibuni ya namna kilivyojipanga kuingia kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.

  Katibu Mkuu wa Chadema hicho, Dk Willibrod Slaa aliliambia Mwananchi jana kuwa chama kimedhamiria kuweka mgombea katika jimbo hilo na hata sasa vijana wako jimboni.“Mikakati ipo,na tutaiweka hadharani baadaye kwa sasa ni mapema mno, lakini vijana wetu wapo kule,”alisema Dk Slaa.

  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, John Heche aliliambia Mwananchi juzi kuwa wanakwenda Igunga kuzindua Opresheni ya Chukua Igunga.“Kama tulivyo na utaratibu wa kuwa na operesheni za kujenga chama ambazo mara nyingi zimejulikana kwa jina la Operesheni Sangara, safari hii katika moja ya mikakati ya kulichukua Jimbo la Igunga, Chadema imeandaa Operesheni Chukua Igunga,”alisema Heche.

  Oparesheni hiyo ya siku ilianza juzi Jumapili na inaongozwa na vijana ambapo Mwenyekiti huyo alisema kazi ya kuchukua jimbo imekabidhiwa kwao.

  NCCR-Mageuzi yapeleka ujumbe Igunga
  Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema chama hicho kitasimamisha mgombea katika Jimbo la Igunga na kusisitiza kuwa kwasasa kimetuma timu ya watu sita kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa ilivyo.

  “Timu tuliyoituma itakapolejesha majibu ndio tutaweza kutanzaga watakaochuana kuwania nafasi ya kugombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR,” alisema Ruhuza,

  Hata hivyo, Ruhuza alisema kuna dalili za wazi kwamba idadi kubwa ya vyama vya upinzani vitasimamishwa wagombea katika jimbo hilo, huku akionyesha wasiwasi hali hiyo inaweza kuipa CCM mwanya wa kushinda.

  “Kuna dalili za wazi kila chama cha upinzani kitataka kuweka mgombea katika jimbo la Igunga. Ni vyema vyama vya upinzani kukubaliana na kusimamisha mgombea anayekubalika ili iwe rahisi kushinda, lakini waking’ang’ania wataishia kugawana kura tu,” alisema Ruhuza.

  Sau nao wamo
  Mwenyekiti wa Sau, Paul Kyara alithibitisha kuwa chama hicho pia kitaweka mgombea katika jimbo hilo huku akisisitiza kuwa katika uchaguzi huo mdogo jimbo hilo litachukuliwa na wapinzani.

  “Tumetuma timu ya wajumbe watatu kwa ajili ya kutizama hali ya kisiasa wilayani Igunga, timu hiyo itarudi wiki hii na majibu kamili, pamoja na hayo mchakato wa kupata mgombea tayari umeshaanza kufanyika,” alisema Kyara.

  UDP yavuta pumzi

  Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alisita kuzungumzia uchaguzi huo huku akifafanua kwamba ni mapema mno.“Ndio kwanza imetangazwa kuwa jimbo liko wazi…, sasa ndio kila mtu aseme kuwa atasimamisha mgombea, ni mapema sana kuzungumzia suala hilo,” alisema Cheyo kwa ufupi.


  CCM bado inavuta pumzi

  Kwa upande wake, CCM kimesema bado hakijakaa kujadili namna kitakavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga.Akizungumza jana Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM bado haijakaa vikao kujadili suala hilo.

  “Chama chetu hufanya uamuzi wake kwa kupitia katika vikao, hadi sasa sisi hatujakutana kujadili suala hilo, ”alisema Nnauye.Jimbo la Igunga limeachwa wazi kufuatia aliyekuwa Rostam kujuuzulu nyazifa zake zote ndani ya CCM kwa kile kilichodaiwa ni kujivua gamba, ingawa mwenyewe alikataa.


  Nec yapokea barua ya Spika
  Kwa upande wa NEC, imekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa Rostam baada ya Spika Makinda kuiandikia.Kaimu Mkurugenzi wa Tume hiyo, Sisti Cariah, alisema barua hiyo imewasilishwa jana kutoka bungeni.“Ni kweli leo (jana) tumepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz,” alisema Cariah
  Kwa mujibu wa Cariah, uteuzi unafanyika kuanzia siku ya 20 hadi 50 tangu Spika wa Bunge kupokea barua na kuiarifu Nec.

  Imeandikwa na Fidelis Butahe, Hadija Jumanne na Aziza Masoud, Geofrey Nyangóro
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi sipendekezi chama chochote kuchukua jimbo la Igunga,bali napenda mbunge yeyeyote mwenye hekima,busara na uwezo wa kuongoza apatikane kwa ridhaa ya wananchi.Tusichague chama kufanya hivyo turuhusu mafisadi kukimbilia kwenye vyama.
   
 3. w

  woyowoyo Senior Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uchaguzi uliopita vilikuwa wapi? au walimuogopa rostam? cuf kazeni buti mna mtaji wa kura 11000
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mimi naenda kama mgombea binafsi
   
 5. A

  Ammynito New Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kutambiana huko na kutunishiana misuli nn itakua hatma ya wakazi wa Jimbo la Igunga???????????
   
 6. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Una maana mgombea binafsi?
   
 7. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Naona una hoja. Kwa bahati mbaya taratibu zilizopo ni kwa mgombea lazima apitie kwenye chama. Hivyo indirectly, ni chama ndicho kinakuwa kimechukua jimbo kupitia ushindi wa mgombea wake. Tunayo mifano ya kutosha ya wagombea wabovu kabisa waliobebwa na chama na wakashinda ila wakashindwa kuwawakilisha wananchi,
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya ingekuwa imepatikana imepitisha mgombea binafsi ningekwenda kuchukuwa ilo jimbo la Igunga
   
Loading...