CUF, CHADEMA kuvunja kambi ya upinzani bungeni:Mafisadi kuchekelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, CHADEMA kuvunja kambi ya upinzani bungeni:Mafisadi kuchekelea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Jan 17, 2009.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kambi rasmi ya upinzani kuvunjika hivi karibuni. Hatua hiyo inatokana na msuguano kati ya CHADEMA na CUF. Wadadisi wa mambo wanasema kwamba kwa kanuni za bunge zinasema kwamba chama au ushirikiano wa vyama utaunda kambi rasmi bungeni ikiwa una zaidi ya asilimia 12 ya wabunge. Vyama vya CUF na CHADEMA vyote vina chini ya asilimia 12 kila kimoja ingawa kupitia umoja huo wameweza kutimiza sharti hilo na hivyo kuwa na kambi rasmi. Habari toka ushirikiano wa vyama hivyo bungeni zinaeleza kuwa Dr Slaa kama makamu wa upinzani aliitisha kikao cha Wenyeviti wa vyama hivyo kilichofanyika nyumbani kwa kiongozi wa upinzani Hamad Rashid ili kuepusha hali hiyo. Katika kikao hicho inaelezwa kwamba CHADEMA waliwapatia wenzao wa CUF ushahidi wa mikanda ya video iliyoonyesha viongozi wa NCCR na TLP wanavyotumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi kuhujumu harakati za vyama hivyo. Katika kikao hicho inaelezwa kwamba CHADEMA waliwaomba wenzao wa CUF kuvunja rasmi ushirikiano na vyama hivyo na kubakisha ushirikiano kati ya CUF na CHADEMA ambao upo pia bungeni. Chanzo chetu kinaeleza kuwa Prof Lipumba alimweleza Mbowe kukabiliana na msimamo huo, hata hivyo alimjulisha kuwa chama cha CUF kingependa kupata muda wa mwezi mmmoja kuweza kufanya maamuzi hayo. Hata hivyo, mara baada ya kikao hicho kilichofanyikwa mwezi Septemba 2008, Lipumba alikaa kikao na Mbatia na Mrema na kuwaeleza mambo yote yaliyojadiliwa. Katika kikao hicho cha viongozi watatu ambacho hakikumhusisha Mbowe iliamuliwa kwamba vyama hivyo vimuunge mkono mgombea wa NCCR katika uchaguzi wa Tarime. Mwezi mmoja baada ya uchaguzi huo wa Tarime ambapo CHADEMA iliibuka mshindi, palifanyika kikao kingine kati ya Hamad Rashid, Dr Slaa na wabunge wengine wenye ushirikiano bungeni kujadili suala hili na kupokea maamuzi kutoka chama cha CUF hata hivyo chama hicho kilijulisha kuwa Baraza Kuu la chama hicho limeelekeza wapewe muda zaidi kuweza kutafakari kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho. Na kwamba CUF iliijulisha CHADEMA kuwa katika kipindi hicho cha subira chama hicho kitasitisha ushirikiano na vyama vya TLP na NCCR. Hata hivyo, uamuzi wa CUF kurejea kuwa na ushirikiano na vyama hivyo wa karibu katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini umefanya majadiliano ya dharura kati ya Dr Slaa na Hamad Rashid kuweza kufanyika kuhusu hatima ya ushirikiano bungeni. Kama majadiliano hayo yatafikia hitimisho la kuvunja ushirikiano baina ya vyama hivyo, ni wazi kwamba kambi rasmi ya upinzani itavunjika bungeni. Hali hii itaathiri nguvu ya pamoja katika kupambana na ufisadi. Wachambuzi wa mambo walishabashiri toka mwaka 2008 kwamba watuhumiwa wa ufisadi wangepenyeza nguvu yao katika ushirikiano wa vyama hivyo hali ambayo inaelezwa kuweza kuanza kujitokeza.

  PM
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  nashindwa kuelewa kwa nini CHADEMA wanang'ang'ani kutoshirikiana na NCCR na TLP badala ya kuelekeza nguvu zao kwenye kuinfluence vyama hivi kuacha ''kutumiwa''!!! Na kwanini CHADEMA walipoombwa kuwaachia CUF kugombea Mbeya Vijijini walitoa haraka sana jibu la NO? Inavyoonekana ni kwamba CHADEMA wanaishi kwenye illusion kuwa wao ndio chama kikuu cha upinzani nchini, kitu ambacho si kweli. CUF kama wana busara watagundua kuwa CHADEMA sio kwamba inapenda kushirikiana ila imegundua kuwa CUF ndio chellenger wake kwa upande wa upinzani, ndio maana NCCR na TLP wanaonekana hawavumiliki wanapaswa kutengwa huku CUF inavumiliwa, pamoja na kuwepo kutokuelewana mara kadhaa katika masuala nyeti!!!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Linapokuja suala la ushirikiano wa vyama vya upinzani, hapa ndipo ubinafsi wa viongozi wa vyama vya upinzani unapotia kichefuchefu. Nilisema wapiga kura wengi wamechoshwa na CCM ila kwa vile hakuna chama mbadala, kuliko kupoteza kura ya urais kwenye utitiri wa vyama, afadhali kumchagua mgombea wa CCM na kuishia bora liende.
  Ushindi wa Tarime umevimbisha kichwa Chadema sasa kinajiona Kidume wakati ukweli wa mambo hakina lolote.
  Chama chenye nguvu za kikweli kweli ni CUF, japo ngome yake ni
  Visiwani, huo ni mwanzo mzuri. Kwa bara, chama hiki kingepata nguvu zaidi kama kitamsimamisha mtu mwenye dini ya Kikristu
  Kwa lengo la kufuta hisia hiki ni chama chenye udini. Bahati mbaya safu ya uongozi wa juu wa CUF hawana Mkristu mwenye
  calibre ya Presidential labda warecruit. Dawa pekee ni ushirikiano.

  Baada ya ushindi wa Tarime, Chadema wameonyesha mwanga kwamba kama Wanatarime wameweza, kwanini Watanzania wote tusiweze 2010?. Udhaifu wa Chadema ni kama wa CUF, hawana strong electable presidential candidate wa kupose serious challenge kwa JK, 2010. Freeman bado mbichi. Mh. Zito ana uwezo na ni tishio lakini bado mchanga. Aliyebaki ni Dr. Slaa ambaye ana uwezo, tatizo ukimshindanisha na JK, Dr. Slaa hauziki sana. Hivyo suluhisho ni ushirikiano.
  Mrema na TLP yake is bypased by time, hawezi tena na ameshaanza kudhoofu kiakili na kimwili. Anaonyesha ni mtu aliyekata tamaa. Alianticipate great expectations and he is disapointed and despaired.
  James Mbatia na NCCR Mageuzi yake ni 'barking dog', seldom bite.hata akiongea, unamuona mkali mdomoni lakini muoga machoni. Nafasi zao wote hawa ni kujitahidi watinge bungeni sio urais.

  Kwenye wapinzani waliopo sasa sioni anyone serious labda angalau John Memose Cheyo. Akipata support na akasimama yeye na JK wawili pekee. CCM itakuwa na hali mbaya 2010.

  Vinginevyo CCM itaendelea kupeta mwaka hadi mwaka mpaka utimie ule ubashiri wa Baba wa Taifa usemao 'Kiongozi bora wa ngazi ya urais, atatoka CCM'.
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  umesema vizuri lakini hili la Cheyo kuuzika kuliko wapinzani wengine sidhani
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kila kukicha na-reconfirm hoja yangu,,, kwamba tuna tatizo kama taifa... na si kama CCM, kama CHADEMA, kama CUF etc.

  Yanayotokea sasa hivi kuna kila sababu tena wazi kwamba hakuna chama cha upinzani hata kimoja ambacho hata kimfumo, kimkakati, kimaadili, ki-sera etc kimejiandaa kupewa kuongoza taifa...

  Na hata wananchi wakiamua kuwapa... wawe tayari pia kuwapa at least miaka 5 kujifunza namna ya kuongoza taifa.

  Kila la kheri na mijadala...
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Waache izo huu ni mda wa kuungana sio kutengana.
  That being the case watawapa CCM nguvu
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Are you kidding us????? Au ndio uko kwenye kampeni za kuwakatisha wananchi tamaa ili waone CCM ndio mambo yote.
  NB: Samahani kama hayo ni mawazo yako ya ki-ukweli na sio kutupoteza lengo!!!
   
Loading...