CUF: CCM imemuonea Edward Lowassa

CUF: CCM imemuonea Edward Lowassa

Swali la msingi sana ulilouliza, why only him and not other 36 candidates, who is complaining about that goli la mkono of Kamati ya maadili?

Mbona hata Membe amelalamika ........... au hujasikia!!

Wengine wanamuogopa Nape, maana kisha watishia watashughulikiwa!!

By the way, Lowasa hajalalamika popote pale. Hao ni wapambe wake tu!!
 
Asante CUF kwa kusema ukweli Lowassa hana kosa lolote ni fitina zao tu mungu anawaumbua tu
 
Chama cha CUF, kimeibuka na kumtetea aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba Chama Cha CCM kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha Kamati Kuu ya CCM (CC).

Kadhalika, CUF kimesema kipo tayari kumpokea Lowassa ndani ya chama hicho kwa kuwa ni msafi na hajawahi kufikishwa hata mahakamani kwa ajili ya kushitakiwa kutokana na madai ya rushwa.

Chanzo: Nipashe

TBC Taifa, Facebook, pia wamesharipoti...!!!
 
He kumbe ni kingunge ndo ameyasema haya,uzee nao tabu jamani,na pia mie hadithi za Lowassa zimenikifu wala sioni mantinki yake,anajifanya yeye ndo alikuwa bora kuliko wote,walikatwa maprofesa,ma dr sasa lowassa,huyu mzee si atulie tu na nyie upinzani hili ganda la muwa la jana mwataka kulipeleka wapi.
 
Hawa CUF naona wananjaa kali sana na wanachama na hasa hasa Tanganyika kwa kiasi kikubwa CUF ipo Zanzibar sasa naona wanatafuta wanachama kwa njia yoyote huku Tanganyika hata kama wanachama wenyewe watakuwa sio waadilifu inashangaza sana kama hata CUF Wataona Lowasa hana matatizo ya kimaadili na hasa ufisadi. OK hawakubaliani na ripoti ya Mwakyembe sasa hata ile orodha ya mafisadi iliyotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga nayo hawakubaliani nayo??

CUF wanasema Lowasa kaonewa kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais nataka tu watueleze wakati wa kuteua mgombea uraisi kwenye CUF Lipumba alishindanishwa na nani???

Halafu waseme pia ni kitu gani kilimfanya Profesa Abdalah Safari akakimbilia Chadema
 
Lipumba "Tumeona CCM watu waliotakiwa wawe Segerea wanataka Urais". Sasa leo wanamuonea huruma mtu ambaye angekuwa Korea Kaskazini au China asingekuwepo.
 
Hii ni mpya. Mwenyekiti Ibrahim Lipumba aliposikia Lowassa kachukua fomu za kugombea urais alisema kuwa inashangaza kuona wezi ambao wanatakiwa wawe rumande ndio wanaotaka kuwa rais wa nchi kupitia CCM. Sasa huyu anayemkaribisha Lowassa ndani ya CUF sijui kaona upepo gani. Au ndio kutafuta kura kwa gharama yoyote hata kama ni kukana maneno yako?
Mkuu, meza taratibu iingie vizuri, dawa kali sana hii.
 
Nipashe kazi mnayo. Huyo hasafishiki. Kwisha!

nipase wameandika taarifa tu iliyotokana na habari star tv

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Pilikapilika za uchaguzi nchini kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Star Tv.
 
Hawa CUF naona wananjaa kali sana na wanachama na hasa hasa Tanganyika kwa kiasi kikubwa CUF ipo Zanzibar sasa naona wanatafuta wanachama kwa njia yoyote huku Tanganyika hata kama wanachama wenyewe watakuwa sio waadilifu inashangaza sana kama hata CUF Wataona Lowasa hana matatizo ya kimaadili na hasa ufisadi. OK hawakubaliani na ripoti ya Mwakyembe sasa hata ile orodha ya mafisadi iliyotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga nayo hawakubaliani nayo??

CUF wanasema Lowasa kaonewa kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais nataka tu watueleze wakati wa kuteua mgombea uraisi kwenye CUF Lipumba alishindanishwa na nani???

Halafu waseme pia ni kitu gani kilimfanya Profesa Abdalah Safari akakimbilia Chadema

CUF wanafanya uchaguzi kutokana na taratibu walizojiwekea, inakuwaje CCM kuvunja kanuni ili kuweka mgombea wa mfukoni
 
Chama cha CUF, kimeibuka na kumtetea aliyekuwa
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba Chama
Cha CCM kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya
Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha Kamati Kuu
ya CCM (CC).
Kadhalika, CUF kimesema kipo tayari kumpokea Lowassa
ndani ya chama hicho kwa kuwa ni msafi na hajawahi
kufikishwa hata mahakamani kwa ajili ya kushitakiwa
kutokana na madai ya rushwa. Source Nipashe.
Unakubaliana na CUF katika hilo?
 
Hivi ni vituko vya CUF ya UKAWA yamekuwa mazito kwao ya Lowassa ndiyo watayaweza?.
 
Back
Top Bottom