CUF bara waufyate tuu

Endapo itathibitika sakaya si mwanacuf,uchaguzi jimboni kwake iwekwe kambi kuhakikisha anapotea na profesa wake.
 
Huku ilikua katibu kumkimbia mwenyekiti... Lakini upande wa pili, mwenyekiti kukimbia Chama, yani baba kumkimbia mwanao wa miaka 5, kweli!...njaa mbaya sana jamani
hivi kati ya lipumba na wewe nani ananjaa jamani ..kuwa muwazi
 
Kwa hii fukuzafukuza Maalim amekurupuka, angetumia hekima na busara katika kuumaliza mgogoro. Na hapa badala ya kuutatua mgogoro ndio ameuchochea. Ametengeneza mgogoro na CUF Bara. Sipati picha jinsi Wabunge wa Bara na Visiwani watakavyoweza kuishi ndani ya Bunge. Sipati picha jinsi dhana ya UKAWA itakavyoweza kutekelezwa ndani ya Bunge wakati mshirika mwenza amejigawanya. Hapa kutakuwa na hali ya kutokuaminiana kati ya Wabunge wa Chama kimoja. Je CDM atashirikiana na CUF Zanzibar au CUF Bara? Ni ngumu kumeza! Kwa ujumla Maalim ametibua badala ya kujenga Umoja ndani ya CUF.
 

Upeo wako ni mdogo., siku zote ni bora chama kuliko yooote hayo uliyoeleza, chama kibaki hai na salama kisiasa ndio kitu nyeti tunachoangalia.,

Tanzania ni kubwa, wasomi wapo wengi, there are so many Prof.Lipumba, hao kina Sekaya ndo kabisa, ni bora kujenga chama kikawa imara zaidi. Lipumba aanzishe chama chake na taasisi yake huko Bara, ukitaka kujuwa kilichomkuta HR Lipumba ni zaidi. HR alitarajiwa kuwa mrithi wa maalim seif leo Zanzibar ukimtaja HR hakuna anayemjuwa ni kwa sababu chama kilifanya maamuzi magumu na kuijenga CUF ya sasa.

CUF tokea imeanzishwa ni chama pekee cha upinzani Tz kilicho madhubuti na kinazidi kupiga hatua kila uchao. Katika taasisi hakuna mtu mkubwa zaidi kuliko taasisi, Lipumba alihisi CUF ni yeye na yeye ndo CUF. mwache ajifunze aendako.
 
Nakukubali sana mkuu Mshana Jr. Japo wengi watapinga lakini ukweli unabakia ndio huo uliouwasilisha.
 
Yote haya yanatokea sababu ya mfumo wa uongozi, mfumo wa Katibu kuamua nani awe mwenyekiti badala ya Mwenyekiti kuamua nani awe Katibu. kwa CUF visiwani Katibu Ndiye Mwenyekiti. Naona hili ndilo alilolisahau Lipumba kuwa pale alikuwapo sababu Seif ndiye aliuamua awepo na ndiye anayeamua chama kiendeshwe namna gani. Lipumba na wapenzi wake walisahau kuwa ya uanachama na uongozi wao ni bara wakiwa visiwani yupo Seif na wapenzi wake.
 
Kosa moja kubwa sana alilolifanya Lipumba ni kuondoka CUF yeye mwenyewe kwa hiari yake (tena kwa press conference na barua ya kujiuzulu) halafu anataka kurudi tena kwa kulazimisha arudi kwenye nafasi yake ileile ya uenyekiti. Hata kama mimi ndo ningekuwa Seif nisingemuamini. Angekuwa na busara angerudi kama mwanachama wa kawaida, awape muda CUF warejeshe imani na yeye ndo aombe uongozi tena.
 
Yote haya yamekuja baada ya Jecha kufuta uchaguzi na Maalim Seif Sharif kufungua kesi kule ICC. Hii ndio njia au mbinu walioibuni usalama wa taifa kuhujumu chama cha cuf. Kama wa kurudi na kudai nafasi yake iwe Dr Slaa yeye hata barua sijui kama kaandika.
 
Hiyo haina ubishi wanajisumbua
 
Na mhimili wa CUF upo zanzibar huku bara kuna wawakilishi tu ambao baadhi wameshikwa masikio na Lipumba sasa ngoja wafutwe uanachama wakaanzishe chama chao tuone umwamba wao
Mkuu umesema neno la msingi sana wakitaka waanzishe chama chao kingine lkn uwezo wa kushindana na visiwani hawana
 
Hakuna cha Cuf bara hapo watu wanatolewa uanachama biashara imeisha kasome katiba ya CUF mana najua ccm mpo nyuma kama mafisi mnasubiri mkono uanguke
Huo mgogoro na shinikizo zote ni ccm kuuwa ukawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…