CUBA yarudisha Marekani Kombora lililopelekwa nchini humo kimakosa!

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Dunia INA maajabu kwa uhasama uliopo kati ya Marekani na Cuba ni vigumu kutafakari kama tukio hili linaweza kutikea baina ya nchi hizo!

Cuba imerudisha kombora la Marekani aina ya Hellfire ambalo lilipelekwa mjini Havana kimakosa kutoka bara Uropa mwaka wa 2014.
Kombora hilo linanoelekezwa na teknolojia ya laser lilifika mjini Havana Julai mwaka wa 2014 kutoka Paris, wizara ya mambo ya nje ya Cuba imesema. "Ilitutia hofu kuona kombora lililotengenezwa Marekani hapa bila stakabadhi za kuidhinisha kuingizwa kwake humu nchini," taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ilisema.
Cuba ilianzisha mpango wa kurudishia Marekani kombora hilo baada ya maafisa wa serikali ya Marekani kutoa maelezo kulihusu na kutoa ombi kwamba lirudishwe. Maafisa wa ulinzi wa Marekani walisafiri hadi Havana siku ya Jimamosi na kulisafirisha hilo kombora hadi Marekani.
source: China Xinhua News
 
Taswira inayonijia kichwani kuhusu hilo kombora ni kama vile hata aliyelipeleka huko hajulikani, wacuba walijikuta tu hilo kombora lipo nchini mwao
 
walijua je kama ni la Marekani
 
Wenzetu walisha endelea sana kwahiyo wanafanya chochote wanacho taka na vitu vingi wanafanya kama bahati mbaya kumbe ni makusudi.
 
Dunia INA maajabu kwa uhasama uliopo kati ya Marekani na Cuba ni vigumu kutafakari kama tukio hili linaweza kutikea baina ya nchi hizo!

Cuba imerudisha kombora la Marekani aina ya Hellfire ambalo lilipelekwa mjini Havana kimakosa kutoka bara Uropa mwaka wa 2014.
Kombora hilo linanoelekezwa na teknolojia ya laser lilifika mjini Havana Julai mwaka wa 2014 kutoka Paris, wizara ya mambo ya nje ya Cuba imesema. "Ilitutia hofu kuona kombora lililotengenezwa Marekani hapa bila stakabadhi za kuidhinisha kuingizwa kwake humu nchini," taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ilisema.
Cuba ilianzisha mpango wa kurudishia Marekani kombora hilo baada ya maafisa wa serikali ya Marekani kutoa maelezo kulihusu na kutoa ombi kwamba lirudishwe. Maafisa wa ulinzi wa Marekani walisafiri hadi Havana siku ya Jimamosi na kulisafirisha hilo kombora hadi Marekani.
source: China Xinhua News

Trojan horse
 
Back
Top Bottom