CTV - CHADEMA TV: Karibuni hewani

Jamani kwa nini wasiiweke hewani hii CHADEMA TV..(CTV)..??? Mimi niko Tayari Kuichangia na nadhani kuna wadau wengi wataunga mkono . Tumechoka na uchakachuaji wa TBCCM. Wadau wa CTV tupeni mikakati yenu jamani.
Ndugu Donyongijape, hiyo Television station ipo njiani kuja unachotakiwa kufanya ni kutunza hiyo pesa ili tukiihitaji iwe karibu mimi ni mdau namba moja hivyo hauna haja ya kuona imechelewa.
 
Mkuu umesema jambo la maana. Hivi ruzuku ya CDM inaenda wapi? Kwa nini isitumike kuanzisha vyombo vya propaganda kama Radio, Magazeti na TV? (Sitaki mtu aseme Tanzania Daima ni la CDM). Kazi ya ruzuku si ni pamoja na kuimarisha chama?
 
we are ready to contribute,i can sale even my laptop to make enough contribution in case i dont have money.
 
<b> we are ready to contribute,i can sale even my laptop to make enough contribution in case i dont have money.</b>
<br />
<br />
Wewee yaani unauza laptop kwa ajili ya tv ya Chadema? Ina faida gani kwako?
 
Ndugu Donyongijape, hiyo Television station ipo njiani kuja unachotakiwa kufanya ni kutunza hiyo pesa ili tukiihitaji iwe karibu mimi ni mdau namba moja hivyo hauna haja ya kuona imechelewa.

Asante sana Mkuu..mimi nimehamasisha marafiki zangu wa kutosha na nitaendelea na uhamasishaji, we are waiting for you. Msituangushe, tunaamini hili tatizo la kuwa na habari chakachuzi kwa habari zinazolenga kumuamsha mtanzania kifkra na zinazohusu harakati za chama chetu litaisha.

Wadau mliotoa maoni yenu kwa nia ya kuchangia na wale mliopledge..Mungu awabariki.. cha muhimu msaada wetu utakapohitajika tuwe-available..! It begins with us! VIVA TANZANIA, VIVA CDM.
 
Pamoja na kwamba sijawahi kuona TV ja chama cha siasa duniani, kwani habari za siasa hususani za chama kimoja cha siasa hazijawahi kuwa habari kwani ni lazima kuwe na pande tofauti, ila hii itasababishwa na wenye tv tanzania kushindwa kuwa wanahabari bali wana siasa. Mimi na pendekeza CDM kuwa wana hisa kwenye Tv station ili kupewa muda wa kurusha matangazo yao na shughuli zao za kisiasa zaidi ya wanavyopata tbc kwenye tv ya wote, ili Station hiyo iweze kurusha na taarifa zingine bila upendeleo.

Tatizo kubwa vyama vya upinzani inavyokumbana navyo ni ccm kuhodhi tv zote hususani wakati wa kampeni kwa kutumia fedha na dola.
 
Aliyekuambia Tanzania Daima ni la CDM kakudangany. Kama unajua kupima habari angalia habari inazoandika Tanzania Daima zinazohusu CDM, na habari inazoandika Uhuru zinazohusu CCM, kama huko kishabiki utaona tofauti kubwa. Hakuna siku Uhuru inaweza andika habari za CCM zenye mtazamo hasi, lakini Tanzania Daima linaandika habari za CDM hata zikiwa hazitakiwi na Wana CDM.

hapo umenena ndugu yangu.... ikiwa mtu hajui asikurupuke kuchangia!! kwan lazima utoe mawazo yako uchwara!??
 
Jamani kwa nini wasiiweke hewani hii CHADEMA TV..(CTV)..??? Mimi niko Tayari Kuichangia na nadhani kuna wadau wengi wataunga mkono . Tumechoka na uchakachuaji wa TBCCM. Wadau wa CTV tupeni mikakati yenu jamani.
Haiwezi kwenda hewani mpaka ikubaliwe na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), ambayo in charge wake kateuliwa na mwenyekiti wa CCM, hivi watu tunaposema tunataka katiba mpya tunaeleweka kweli?
 
Pro-CMD-JF, nawashauri fanyeni kazi ebu acheni kukaa vijiweni, hivi mnadhani CDM wakianzisha TV: maisha yenu ndio yatakuwa mazuri? Huko ni kujidanganya.
Natoa wito na nasaa kwenu serikali ya maisha yenu ni vichwa vyenu!
 
Mimi tachangia Dola 30,000 lakini kwanza lazima nione kituo kwanza, na sijui mtakuwa mnarushia wapi matangazo yenu? Moshi au Kilimanjaro
 
Gazeti lenu la TZ Daima limeshindwa kuwa gazeti lenye mvuto, hebu angalia hata jf post from newspapers uone ngapi ni za hilo gazeti pamoja na jf kuwa na pro-CDM wengi.
Kwenye website yao habari zinabadilishwa after 3days
I tell u kama mtataka TV yenu ifanikiwe punguzeni propaganda za ki-CDM, la itabakia TV jina tu.
Zitto mwenyewe ile habari yake ya meli znz hakutuma TZ daima, wala JF, jiulize kwa nini?

Wewe una pepo liitwalo MAGAMBA jitambue ili uombewe. Unaweza kulinganisha gazeti ya TZ Daima na magazeti marehemu Uhuru na Mzalendo yenye propaganda, habari za unafiki wa uhuru na uzalendo bandia chini ya Chama kinachoelekea kuzimu? Yanayotetea maovu ya watawala, yanayopaka mafuta ufisadi na rushwa?

Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini ni mojawapo wa wapendao kusoma magazeti nikiwa mpenda Haki na Amani, mzalendo wa nchi inayofilisiwa wanamagamba. I fill shame kugusa gazeti la Uhuru au Mzalendo mbele ya kadamnasi kwa sababu kati ya makundi ya watu wanaonunua magazeti, ni nadra sana kuona mtu ananunua gazeti la Uhuru au Mzalendo, na ukiona hivyo lazima awe ama mojawapo wa wanafiki ama ni mtafiti anataka kujua unafiki unaozalishwa na magazeti hayo kwa kufanya ulinganifu na magazeti mengine.

TZ daima linajiuza lenyewe kwa habari zake. Nakuonea huruma kwa sababu bado hujajitambua kwamba hapo ulipo wewe watu walishaondoka zamani wewe bado unauchapa usingizi.

Kigumu Chama cha nani hii......
 
Pro-CMD-JF, nawashauri fanyeni kazi ebu acheni kukaa vijiweni, hivi mnadhani CDM wakianzisha TV: maisha yenu ndio yatakuwa mazuri? Huko ni kujidanganya.
Natoa wito na nasaa kwenu serikali ya maisha yenu ni vichwa vyenu!

Ukiona mtu ambaye ni GAMBA anatoa ushauri wa staili hii ili kuvunja moyo, AMEONA HATARI KUBWA ILIYO MBELE YAKE... CTV is another threat to YOU Pro-TBCCM-JF and elsewhere in the country.
 
Nadhani chadema hawajawa serious na kuanzisha Tv station, chama kinavyokubalika mikutano 100 tu na uchangiaji wa kawaida kupitia akaunti maalumu na kupitia huduma za simu ndani ya miezi 6 kimeshaeleweka, na mle kwenye ruzuku wanajibana ndani ya miezi 4 wanaweka hapo milioni mia 2. Jitihada zinatakiwa kabla ya 2013.

Wapi Mnyika, wapi Dr Slaa, wapi Lissu, wapi Mdee, wapi Zitto, wapi Lema, Wapi Wenje. Kamateni wazo letu, weka mipango safi, wekeni namba tuchangie.
 
Jamani kwa nini wasiiweke hewani hii CHADEMA TV..(CTV)..??? Mimi niko Tayari Kuichangia na nadhani kuna wadau wengi wataunga mkono . Tumechoka na uchakachuaji wa TBCCM. Wadau wa CTV tupeni mikakati yenu jamani.
Ndugu Donyongijape sahihisho dogo tu siyo CTV ni Chadema Television Network CTN
 
Back
Top Bottom