CRJE na ufisadi serikalini

Engineermsuya

Member
May 23, 2011
32
7
1-26.jpg

Hii ni kampuni ya ujenzi ya waChina hapa Tanzania

hii kampuni inaongoza kwa kutuhumiwa kuwatajirisha maofisa wa serikali ambao wanahusika kwa namna moja au nyingine kutoa tenda za ujenzi.

CRB nao inaonekana hawana uwezo wa kuwafanya kitu lakini kwa sababu kampuni za wazalendo hazipendwi na maofisa waserikali kwani hazitoi rushwa, sasa hivi wazalendo wengi wameamua eidha kuuza au kuhamia nchi za jirani huku Tanzania inaachiwa CRJE

Kama hamumini tazameni nani anapitisha tenda za hiii kampuni na hali zao za kimaisha zikoje. Pia kwa kuwa waChina bei zao ni za chini mno lakini ukweli ni kuwa wanaweka materials ambazo ni hafifu sana kwenye majengo lakini of course kwa sababu washawanuanua ma inspectors hakuna anayeweza kutia neno.

sisi kama wama taaluma hiii tumefika hatua ya kukata tamaa na juzi nilikutana na wanafunzi toka ardhi ambao ilibidi niwape hali halisi ilivyo huku nje ya shule.

Kama serikali ispoliangalia hili kwa undani basi muda si mrefu mtaona industry nzima inaanguka Tanzania wakati Rwanda na Kenya serikali zao zina linda local companies.
 
soma hapa: https://www.jamiiforums.com/habari-...uuza-magufuli-ujenzi-barabara-ya-mbagala.html
 
kweli kabisaa kwa mfano kuna jamaa yangu ananiambia udom inamiaka mitatu na nusu lakini majengo yake yana crake za kutisha,tiles zinacheza ukikanya majengo hayajakabidhiwa lakini yanahitaji repair na ni hao hao CRJE,they do not know if cheaper things comes with costs
 
China Railways Jiangchan Engineering - CRJE
China Construction Company -CHICO
China Geo Engineering Company - CEGC
CCCE

wachina kiboko .... tumekwisha
 
China Railways Jiangchan Engineering - CRJE
China Construction Company -CHICO
China Geo Engineering Company - CEGC
CCCE

wachina kiboko .... tumekwisha
Mbona wapo wengi zaidi ya hapo mkuuu! na wanahonga mbaya! Bahati mbaya sana wafanyakazi wa hapo hawana mikataba!espl ma QS,
Jamaa kila site kunawachina kibao ambao hata permit hawana, wanaishi kihuni tuu, Serikali ifuatilie hawa watu wanafanya kazi nchini wengine hata Visa hawana (wameletwa kwenye makontena kama mzigo) NI AIBU kwa serikali!
 
kweli kabisaa kwa mfano kuna jamaa yangu ananiambia udom inamiaka mitatu na nusu lakini majengo yake yana crake za kutisha,tiles zinacheza ukikanya majengo hayajakabidhiwa lakini yanahitaji repair na ni hao hao CRJE,they do not know if cheaper things comes with costs

Ni kweli kabisa!! Wakina Mlacha na Weja wanajifanya hawayaoni
 
RJE ndio waliopewa tenda na mashirika mbali mbali ya serikali kujenga University of Dodoma

sasa hivi nadhani mmeona jinsi yale majengo yanavyoleta matatizo ya nyufa.

In short hawa wachina ni mafisadi kuliko wahindi na wanatoa rushwa ndefu kuliko hata hao wahindi

makampuni ya wazalendo yanaishia kufanya kazi za bidding na kutolewa dola 100 za tenda dokoments lakini hawapewi kazi yoyote hata kama wame qualify steji zote
 
From what I know, moja kati ya masharti ya misaada kutoka China ni kuhakikisha kuwa kampuni kutoka China zinapata Tender/kazi mbalimbali kwa urahisi. Msishangae kuwaona, ndio matokeo ya vitu kama Uwanja mpya wa Taifa, Airport Terminal III nk
 
Na sasa hivi wanapewa kazi ya uwanja wa Mwanza japo mfadhili alisema kazi inatakiwa ifanywe na contractor mzalendo
 
Hapa sasa mchina ana kosa gani?

Any way sijui uwezo wa wakandalasi wetu wa ndani katika hasa katika kazi na ubabaishaji kama wameacha au bado wapo vilevile ambapo unakuta kuna kampuni hata osifi haina ila zipo ndani ya begi na brief case.

Mto mada ebu tupe details kidogo juu ya uwezo wa makampuni ya ndani?
 
ukiambiwa wachina ni wa china kayaangalie yale majengo ya udom, hadi waziri x aligomea lakini wakapewa go on. Jengo la ku accomodate watu 4oo. Flow 3 yamekamilishwa kwa miez si zaid ya mi3. Wakati kuna sheri ya x inajengwa na hao hao tangu 2009 mpaka leo bado.
 
RJE ndio waliopewa tenda na mashirika mbali mbali ya serikali kujenga University of Dodoma

sasa hivi nadhani mmeona jinsi yale majengo yanavyoleta matatizo ya nyufa.

In short hawa wachina ni mafisadi kuliko wahindi na wanatoa rushwa ndefu kuliko hata hao wahindi

makampuni ya wazalendo yanaishia kufanya kazi za bidding na kutolewa dola 100 za tenda dokoments lakini hawapewi kazi yoyote hata kama wame qualify steji zote

Jamani!!,naona tusiweze vitu kwa ushabiki!!!,kwamtu wa kawaida nyufa ina maana tofauti kabisa na wataaluma wa uhandisi wanavyoelezea,bahati nzuri nilikua kati ya timu walio sanifu baadhi ya majengo ya UDOM(structure design), majengo yote ni frame structure yaani kuta za matofali hazihusiki na ubebaji wa mzigo!!!Mpaka hapo msuya umenipata!

Sasa ni nadra sana kupata failure cracks kwenye aina hii,vitu waweza pata ambavyo ndio wengiweni mnazani ni failure cracks ni shrinkage cracks kwenye either kuta za tofali au kwenye skimming ambazo ni kawaida kwenye region ambazo evaporation iko juu,with time vitu hivyo uisha.

Wengine wamefikia hata kuita expansion joints ni nyufa, hii balaaa!!!!!!!

Kuhusu wakandarasi wazawa na wachina, kwa kweli sisi wazawa tunaitaji kwa kweli tujifunze hata nidhamu ya kazi, kwa taalifa tu kuna wazawa walipewa tenda huko UDOM lkn wengi wao ilikua aibu mtu analamba advance tu anakimbilia VOGUE na kuacha kazi ya watu baadhi yao walifukuzwa.

Mi naamini kama usimamizi ni mzuri wachina wanaperfome nenda UDOM angalia projects za mifuko tofauti utajifunza kitu.
 
Makandarasi wengi wa kitanzaania hawana uzoefu wa kusimamia miradi mikubwa. kibaya zaidi kazi ya ujenzi ukiihariba metengenezo na matumizi yake yanakuwa aghali zaidi! so .... no client is willing to risk his investment. Otherwise nakubaliana na Fighter hapo juu . hata hivyo nitoe angalizo kwamba kuna wakti ujenzi unakuwa hovyo kiasi cha kusababisha failure of structural members. [ kaanagalie beams za jengo la Millenium tower upande wa parking kunambili au tatu zina moment failure]
 
Thread imekaa kifitna fitna tuu

hamna la zaidi mnataka kuharibia watu majina

unless mtu alete ushahidi uliokamilika ku support hizi tuhuma.

au aje mtu atupe direct from the industry
 
Back
Top Bottom