SI KWELI Cristiano Ronaldo amewazawadia gari wazazi wa Sadio Mané?

SI KWELI Cristiano Ronaldo amewazawadia gari wazazi wa Sadio Mané?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
A beautiful gesture of respect and gratitude. ristiano Ronaldo surprising the parents of Sadio Mané with a brand-new Mahindra Scorpio — a moment that shows true brotherhood and appreciation for the people who raised a legend.
Mane zawadi 1.jpg
Zawadi 2.jpg
 
Tunachokijua
Cristiano Ronaldo na Sadio Mane ni wachezaji wa timu ya Al-Nassr inayoshiriki ligi ya Saudi Pro League.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo X wamechapisha picha ikieleza kuwa Mchezaji Christiano Ronaldo amewazawadia gari wazazi wa Sadio Mane.

Taarifa hiyo imeambatana na picha inayowaonesha Mane, Ronaldo, wanaodaiwa kuwa ni wazazi wa mane pamoja na hilo gari.

Uhalisia wa madai hayo

Baada ya ufuatiliaji, Jamiicheck imebaini kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Kupitia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa hakuna chanzo chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ukilinganisha na ukubwa wake kwa upande wa michezo.

Hakuna taarifa yoyote katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Sadio Mane ama Cristiano Ronaldo kuonesha kuhusu tukio ama picha za tukio hilo.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa picha hiyo iliyoambatanishwa na taarifa hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde. Nyenzo ya hive moderation imebainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa AI kwa takribani asilimia 99.
1773416428820-png.3557563
Back
Top Bottom