Mwitongo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2009
- 312
- 360
Ndugu zangu, katika hali isiyo ya kawaida, leo nimeshuhudia tukio la kusikitisha. Nilikuwa katika Benki ya CRDB, Tawi la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam; nimeshuhudia mhudumu wa dirisha namba 2 akikataa kupokea fedha za mteja mmoja kijana. Kisa ni kwamnba kijana huyo alikuwa na fedha nyingi za Sh 50, 100 na 200 ambazo kwa kawaida ni sarafu. Mhudumu amekataa kuzipokea kwa maelezo kwamba hawapokei "masimbi". Akamtaka kijana huyo azipeleke kwa makondakta wa daladala, azibadili ili wampe noti, au masimbi hayo ayapeleke BoT. Kukawa na vuta nikuvute, mwisho yule kijana akaondoka bila kuweza fedha kwenye akaunti.
Hoja: Hii ni sahihi kwa benki kukataa kupokea sarafu? Je, sarafu hazitambuliwi kama fedha halali hapa nchini? Naomba wadau tulijadili suala hili.
Nawasilisha.
Hoja: Hii ni sahihi kwa benki kukataa kupokea sarafu? Je, sarafu hazitambuliwi kama fedha halali hapa nchini? Naomba wadau tulijadili suala hili.
Nawasilisha.