McCarthy
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 506
- 552
Salaamu wanajamvi?
Neema zoote kwa Baba Mungu/Allah.
Rejea kichwa cha mada hapo juu kama kinavyojieleza.
Kwamba, mimi ni kijana wa Kitanzania nikiwa kwenye 20's kiumri. Ninatafuta kazi ya kuajiriwa kwa dhumuni la kutoa huduma za kifedha kwenye duka la uwakala wa benki na/au makampuni ya simu mathalani "NMB Bank", "CRDB Bank", "Access Bank-Tanzania", "Vodacom M-Pesa", "Airtel Money," "Tigo Pesa" miongoni mwa mengine yenye vinasaba vya namna hiyo.
VIGEZO VYANGU NI:
1. Nina uzoefu wa hii kazi kwa miaka 7 na miezi takribani 9 yaani tangu mwezi Octoba, 2011 mpaka Juni, 2019 nikiwa nahudumia kama "NMB Wakala", "CRDB Wakala", "Access Bank -Tanzania Wakala", "Vodacom M-pesa Wakala", "Airtel Money Wakala", "Tigo Pesa Wakala", "Halopesa Wakala" pamoja na huduma zingine ndogo-ndogo ambazo ni mazalia ya hizo huduma kuu.
2. Nina elimu ya kutosha juu ya masuala haya ya biashara za uwakala wa mabenki na makampuni ya mawasiliano ya simu katika kufanya miamala ya kifedha. Hii ni kwa sababu nimehudhuria semina na makongamano mbalimbali yatolewayo na makampuni husika kwa nyakati tofautitofauti kwa mawakala wao juu ya ufanyaji biashara; yaani
a) mahitaji muhimu ya kuzingatia kama wakala wa mambo ya kifedha (mwakilishi wa benki/kampuni ya mwasiliano ya simu),
b) mahusiano baina ya mteja na wakala.(ukarimu mkubwa lakini kwa tahadhari kulingana na mteja anavyokuja)
c) masuala ya usalama wa ofisi kwa ujumla wake wakati wa kazi na umakini wa wakala juu masuala ya usalama awapo kazini.
d) mbinu za kuwa wakala bora kieneo na kujikusanyia wateja wengi na hata kutunukiwa vyeti vya huduma na uzalishaji bora.
e) masuala ya matapeli wa kimtandao ambao huwa wanapiga simu moja kwa moja na kujitambulisha kama watoa huduma kwa mawakala kutoka makao makuu na kumpa wakala maelekezo ambapo anaweza kujikuta anahamisha fedha (kama hana uzoefu); wateja matapeli wanaokuja ofisini kama wateja wa kawaida na mbinu zao (Nikiwa kazini nimepata visa vingi sana vya namna hii kwa ama kupigiwa simu na watu hao au wateja matapeli kuja kama wa kawaida ila kwa kuwa nilikuwa na uzoefu na elimu ya kutosha juu ya mambo hayo hawakufanikiwa)
f) makosa ya utakatishaji fedha na namna ya kuibaini na kudili na miamala ya namna hiyo. Kwa kufuata maelekezo ya benki au kampuni ya mawasiliano ya simu kwa kuzingatia sheria za nchi.
3. Najua mbinu mbalimbali za kufanya biashara hii kutokana na uzoefu wangu na mwajiri hatojutia. Mfano: anaweza kuwa na mtaji wa kawaida tu lakini akazalisha sana kama kuna wateja wengi eneo la biashara. Hii naweza kufanya kwa kubadilishana "float" au "cash" kupitia "super agents" wa makampuni husika au kuhamishia "float" benki na kupokea "cash" na kinyume chake(kama benki ipo jirani(hususani kwa maeneo ya mjini) Kwa kutumia "Agent's Till (second till)", etc.
4) Napenda kazi hii kwa dhati kwa sababu naijua vizuri.
Kama wewe ni ama mwajiri au vinginevyo, tukutane "inbox" kwa mawasiliano na maelezo zaidi.
Nawasilisha.