CRDB Salary Advance

Hiyo ni mikopo isiyo na tija.wangewaachia MPower
hawa acha wajifie njaa tu,maana hawatumii akili.Mimi waliishia elfu kumi,wakasitisha hawajawahi nikopesha tena wala sababu sijawahi ambiwa.

wanatuma sms haijafaulu,sjui nini?.
 

WAELEWEZE WAKUELEWE, JARIBU NAMNA YA KUBADILI TAREHE ZA KUCHUKUA MSHAHARA, THIS DOESN'T HELP A THING. HAIWASAIDII WAFANYA KAZI, LABDA DENI LINGEKUWA LAKAA MIEZI KAZAA.
 
Mfano mtu salary yake ni laki 8, je anaweza kukopa laki 9 ama.milioni? Au unakopa amaount unayolipwa..inakuwaje
 
Msemaji wa crdb. Asante
 
Mkuu...hakuna haja ya kusubmit salary sleep kwa badae?
Na mshahara ukichelewa itakuwaje, kuna waajiri wengine mpaka tar 15 ya mwezi mwingine. Pia kuna assurance gani kama mtu atapitishia mshahara hapo maana akiona anadaiwa anaweza kuongea na mwajiri alipwe kwa njia nyingine
 
Hakuna haja cha msingi uwe mtumishi wa serikalini na mshahara uwe unapitia CRDB..Unaruhusiwa kukopa mpka asilimia 50% ya take home yako ya mwez husika
Kwa hiyo ni wa serikali tu! Mbona makampuni binafsi ndio yenye wafanyakazi wengi na mishahara mikubwa na wwnapitisha mishahara hapo
 

Hiyo 5% ya riba ni kwa mwezi yaani 60% kwa mwaka? Hebu tupe maelezo ya kutosha maana hizi benki wanatukamua kotekote, mara service charge, maintanance fee nk.

Vv
 
Kama nikikopa tarehe 10 na mshahara wagu ukaingizwa 24; nikikatwa asimia 5 ni sawa na 120% kwa mwaka huu ni uonevu kwa wanyonge. CRDB kama mnataka kutenda haki; mngechaji kwa kutumia OVERDRAFT rates na kwa siku ambazo huyo mtumishi amechukua pesa zaidi ya salio lake.
 
Apa kwa mwezi lazima CRDB ikombe pesa za walimu wengi sana...jamaa wanabuni mbinu za kufilisi watu tu....heheheee big up sana , jamaa wameiva kwenye taaluma zao
 
Naomba kujua je ni lazima mtu ukope mwaka mzimaa?! Mbona umefanya assuption ya mwaka wakati ni mkopo ni wa mwez mmoja?! Sijaelewa hapo
 
Naomba kujua je ni lazima mtu ukope mwaka mzimaa?! Mbona umefanya assuption ya mwaka wakati ni mkopo ni wa mwez mmoja?! Sijaelewa hapo
Mkopo ni Wa mwezi mmoja tu sio kwa mwaka kwa mfano ukikopa 100,000/= mwezi huu. Unatakiwa kurejesha mwezi unaofuata kwa riba ya 5%ambayo kw jumula ni 105,000/=
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…