CRDB Mobile na CRDB internet Bank sio salama kwa pesa zetu.

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
Jana nimepata meseji hii “ Dear customer, your estatement password for the month of September for the account ending with 83400 is 323240” na nikicheki ni kweli account number yangu inaishia na namba hizo lakini cha kushangaza sender inaonekana ni CRDB BANK wakati message centre ni +265299000110 ambayo inaonekana sio ya Tanzania. Kwa kusema hivo inaonekana kuna watu wameingilia mtandao wa Bank ya CRDB maana hii haiwezi kuwa kitu ya kaiwaida
 
technolojia itawaponza watu we subiri tu muone!!sijui e-statement,mobile banking n.k!
angalizo hizi benki zetu wasi introduce products ambazo zina risk kubwa ya kuwa hacked!
 
Acha ushamba wewe ulizaliwa wapi? Hiyo password nilitumiwa nilipoingia katika email yangu nilikuta ujumbe toka crdb bank. Wakati wa kufungua nikadaiwa password nikaweka hiyo niliyotumiwa kwenye......kitu hicho kikafunguka kumbe ni statement yangu. Nafikiri ninkwa ajili ya usalama wa statement yako mimi nilifanikiwa kuona
 
sasa ndugu yangu, usimsute mwenzio, mwambie vizuri.. mbona mm nimepata ujumbe lakini sijapata email!?
 
Acha ushamba wewe ulizaliwa wapi? Hiyo password nilitumiwa nilipoingia katika email yangu nilikuta ujumbe toka crdb bank. Wakati wa kufungua nikadaiwa password nikaweka hiyo niliyotumiwa kwenye......kitu hicho kikafunguka kumbe ni statement yangu. Nafikiri ninkwa ajili ya usalama wa statement yako mimi nilifanikiwa kuona

Ni kweli mie ni mshamba kutokea mkoa mpya wa Katavi eneo moja linaitwa Majimoto, lakini kitu ambacho mie sijakielewa ni kwa nini center number ni +265 ambayo inaonesha kuwa ni country code ya majirani zetu nchi ya Zambia? Angalia kwa makini meseji yoyote kama umetumiwa na mtu wa TZ center number ni +255. Anyway yawezekana mie ni mshamba kama unavaodai na mie nalikubali kwa kuwa niko huku Katavi lakini mimi kwa uelewa wangu mdogo nadhani hao ni hackers na hiyo estatement yao plus password sizitaki sidanganyiki
 
Acha ushamba wewe ulizaliwa wapi? Hiyo password nilitumiwa nilipoingia katika email yangu nilikuta ujumbe toka crdb bank. Wakati wa kufungua nikadaiwa password nikaweka hiyo niliyotumiwa kwenye......kitu hicho kikafunguka kumbe ni statement yangu. Nafikiri ninkwa ajili ya usalama wa statement yako mimi nilifanikiwa kuona
wajanja ndio waliwao
 
Siku zote kuna faida na hasara hata ukiweka katika kibubu, mfuko wa rambo ukachimbia, ukazichimbia handaki,uka weka kokote unakoona umeweka salama ipo siku utakwama tu!
Cha msingi kwa technologia tunayoenda nayo mahaka/wezi wa mtandao wataongeza ni wewe kuwa na tahadhari na kusoma vipeperushi mbalimbali ili ujielimishe usije ibiwa ukisubiri mtu asome kwa ajiliyako utakuja lipia gharama ya muda wake/utaibiwa.
Na uwe na akaunti katika benki tofauti ili moja iwe ya mobile na nyingine usitake huduma hiyo ili uweze kufuatilia kwaurahisi pesa zako na matumizi yake kwani Simbanking/Nmb mobile na nk ufuatiliaji wake ni mgumu na Hizi huduma ni nzuri zinarahisisha kazi zetu. Kwahiyo kuwa na akaunti mbili moja jiunge ila nyingine usijiunge na uliyojiunga isiwe na pesa nyingi sana ziwe ni za kuhudumia matatizo madogomadogo na isiyounganishwa weka pesa zako kwani ikitokea wizi ni rahisi kufahamu kilichofanyika na utarudishiwa kirahisi.
Mobile banking ni nzuri sana ila tumia kwa uangalifu maana pesa kupotea ni rahisi kwani unaweza kuchukua muda wowote na wakati wowote na popote pale na inaweza ukawa unaibiwa senti ndogo sana usijue au usione adhari kwa mapema.
Kuibiwa benki hutaweza kuzuia maana si wote wanaojua salio/masalio yao au riba wanayopata kwa miezi 3 au mwaka mzima cha msingi ni kupunguza uchotaji wa vijisenti vyako ambapo unaweza kuuliza salio hata mara 3 kwa siku hali kuna wengine hata hawajui salio lao na wengine masalio/salio lao ni kuna milioni ngapi na laki ngapi, makumi elfu hawajui hata kama wamechukua karatasi ya salio.

Nashauri waliojiunga watumie kwa uangalifu na si kuacha kutumia kwani matumizi ya huduma hiyo ni makubwa kuliko unavyodhani wewe na hayana weekend na hayana muda wa kazi wala wa sikukuu au siku ya mapumziko bali ni kutatua tatizo kwa urahisi na kutumia muda mchache
 
Back
Top Bottom