Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,955
Hiyo bank ina slogan yao eti "the bank that listens" they should change to "the bank that LISTENED" hapo wala hawatakusikiliza ndg.Kama kuna CRDB bank employees ujumbe huu naomba muufikishe kwa mabosi wenu.
Network yenu haieleweki, wiki iliyopita network kwangu ilizingua ndani ya siku kama 3 hivi kila nikijaribu bilabila, ikatulia kwa siku kadhaa leo najaribu tena niweze kurekebisha maisha yangu network hamna.
Yaani hata kutazama salio mpaka niende bank zama hizi.
-Na ma ATM yenu yanasumbua sana hasa tarehe za mshahara.
-Makato makubwa kwa huduma ya kuhamisha fedha kwenda kwenye mitandao ya simu.
Mi yalinikuta hayo, nikaambiwa niandike barua, afu nisubiri ka wiki 2 ivi, afu ndo ilikua hela ya nauli nipo stendi.Wana jamvi mimi yamenikuta. Niko Kigoma ugenini, nikajifanya kutoa hela CRDB kwenda mpesa ili niitoe kilaini. yaliyonikuta ni balaa. Kwanza ilitoka halafu ikakataa kuja Mpesa, nikawasiliana nikaaambiwa ipo hewani na itarudi benki ndani ya saa 24. Sasa masaa 24 yamepita naambiwa nisubiri masaa mengine 24. Naomba ushauri jinsi ya kufungua madai maana hapa nimeshapata damage kubwa balaa. Tahadhari iwe kwako pia. Asante.
Nenda kwenye dawati la CRDB wanapohudumia wateja wakupe ufumbuzi
Mzee Shinyangaaa!!!! Hata mbinguni JF ipo?Dah mi ndo maana siweki hela Benki,