CRDB Is this stupidity or lack of caring?

CRDB Is this stupidity or lack of caring?

Niko katika mchakato wa kutafuta benki nyingine. Crdb wanafanya "business as usual". HAWAJALI KABISAAA!. Na hata ukitoa malalamiko ni buree HAWAJALI pia.
 
Kwa kifupi tu ni kwamba watumishi wengi wapya wanapata matatizo sana na haya mambo ya huduma kwa mtandao ila huwa hawataki kukiri kuwa haya mambo yanawapita pembeni. Wakati umefika sasa kwa wafanyakazi kujifunza zaidi haya mambo mapya ili kwenda na kasi ya CRDB kutoa huduma kisasa zaidi kwa kutumia miundombinu iliyojiwekea.Mara zote hadithi ni hizo hizo zinazofanana na ainisho la mtoa mada.Nimefungua akaunti katika benki hiyo kwa nia ya kufanya mambo mengi ya kibenki kupitia kwenye mtandao lakini ni wiki sasa zinakatika bila kuwa na taarifa zaidi ya tutakujulisha kwa sms au email.
 
Nilishajitoa CRDB siku mingi sana wamezidiwa na wateja na wanaringa sana

Mimi na ndugu zangu hatutaki kusikia hiyo bank wanadharau sana wateja wameshajiona Kama Ronaldo ama Messi
 
CRDB ni majanga matupu. Wanasikitisha sana.

Hiyo bank haiwafunishi wafanyakazi wao teknolojia mpya zinazokuja.

Hili swala la paypal ni kichomi, inasikitisha benki kubwa kama hiyo inajaza vilaza ambao hawajui hata paypal ni nini...

Nilifuatilia kuunganishwa na online purchase kwa miezi mitatu.

Eti branch nzima hawajui hata paypal ni nini..

Kubwa zaidi walivyokuwa wanachomoa hela zangu kama 550,000 bila maelezo yaliyonyooka.

Ndo nikaondoka huko mazima.

CRDB is too big to control, wana wafanyakazi vilaza sana..
 
Customer care wote CRDB watakuwa wameishia darasa la saba, maana huwa hawajielewi, unaweza ukamuuliza swali lenye mantiki kabisa, lakini yeye akakujibu kama roboti bila hata kutafakari kile anachokujibu kama kina logic au la, bogus.
 
CRDB ni majanga matupu. Wanasikitisha sana.

Hiyo bank haiwafunishi wafanyakazi wao teknolojia mpya zinazokuja.

Hili swala la paypal ni kichomi, inasikitisha benki kubwa kama hiyo inajaza vilaza ambao hawajui hata paypal ni nini...

Nilifuatilia kuunganishwa na online purchase kwa miezi mitatu.

Eti branch nzima hawajui hata paypal ni nini..

Kubwa zaidi walivyokuwa wanachomoa hela zangu kama 550,000 bila maelezo yaliyonyooka.

Ndo nikaondoka huko mazima.

CRDB is too big to control, wana wafanyakazi vilaza sana..
Mimi walinichomolea 3.5m, nilipowauliza wakaniambia eti ile siku nilipoenda kudraw yule teller akajisahau eti alipokuja mtu wa nyuma yangu akatoa kwenye akaunti yangu badala ya yake.., senseless..!
 
Mimi nilishafunga account CRDB. Mke wangu Ali insist tuwe na joint account but sikuwahi hata kwenda kuichukua card Yao. It is the bank of my last choice. Kiukweli wana huduma zinakera mpaka basi.

Msema kweli in mpenzi WA Mungu (in Magufuli's voice) mimi bank yangu ni Standard Chartered hawajawahi kuniangusha. Iwe miamala ya hapa au nikiwa nje ya nchi. I simply love them. Hata ungewapigia simu ukiwa nchi gani........the problem will be solved instantly.

CRDB Watu wenye dhamana wamekaa madarakani mda mrefu they have run out of ideas.

Ushauri wangu: funga account tafuta bank ambayo wataheshimu jasho lako. Kutafuta pesa shida hata kutumia?
 
Hivi hakuna CRDB people wanaopita humu? I can't believe this!

Halafu watu wanamlaumu Magufuli eti hela imepotea. Kwa approach Kama hii ya business as usual.....itapotea sana tuu.
 
leo nimefika tena kwenye branch yao nikaambiwa niandike barua ili card yangu ifunguliwe, swali langu ni kwanini ilifungwa? baada ya kuandika barua wakanipa form nijaze, nikawaambia nimeshajaza zaidi ya form tatu sasa na kila ninapokuja mnasema nijaze form. basi wakacheck kwenye mafail yao nakukuta form niliyojaza hapo nyuma na wakaambatanisha na barua yangu. wakaniambia watanipigia simu leo. ila cha ajabu kama kawaida yao ya kutoa promise za uongo kuwa watapiga simu au kutuma sms sijaona chochote mpaka mda huu, 7:31pm ( saa moja na nusu usiku ) Hivi hakuna customer support ya crdb humu ndani? au wao wapo vizuri sana kiasi kwamba hawataki kutatua matatizo ya wateja wao kupitia jamii forums?

Hamia Exim, achana na hao washajitosheleza
 
Haya yote ni shida ya sisi watanzania kutopenda kufanya kazi. Inakuaje mfanyakazi wa crdb kitengo cha huduma unashindwa kumsaidia mteja juu ya shida ambayo kila siku ndio kero unazoletewa kwenye meza yako?. Hatutaki kuvishughulisha vichwa vyetu, hatutaki kujifunza vitu vipya, hatuna mahaba na kazi tunazofanya tunachofikiria sisi ni kuhesabu tarehe za mwezi ili ufike mwisho wa mwezi tupate chochote kitu, inasikitisha na kuumiza sana tena sana. Unazungumza na mtoa huduma anavyoongea ni kama vile unampotezea muda, twende wapi? Tufanye nn ?. Watanzania wenzangu tupende sana kufanya kazi hii ni ibada kubwa mbele ya mungu.
 
Crdb kwa sasa wamelewa sifa ,, Ukija tawi la Mbezi ya kimara pale ndo utaochukia hii bank hadi basi.
Wame Installe ATM machine nne pale lakini kila siku yenye hela ni maoja au mbili na pengine ukute zote hazina kitu.
 
Hao jamaa niliwahama zamani sana, walishindwa ku-idhinisha card yangu ili niweze kufanya manunuzi online,, karibia nikose mke kwa sababu siku naenda ukweni jmosi flani hivi system ya bank ilikua down siku nzima na hela za mahari zilikua huko. Nikaona bora nifunge account tu kuliko kapata stress wakati hela ni zangu, nilihamia equity bank na sijuti mpaka kesho.
 
kadi yako haikuwa na tatizo lolote, inashangaza CRDB bado kuwa na matatizo kama hayo hadi leo, hamna tofauti na tigo, inaonyesha hao customer care ni wale wa low IQ, yani hawawezi tatua matatizo ya wateja kabisa.
Hali hiyo ilikuwa inanikuta zamani, ukifanya transaction, CRDB hawakati hela hapo hapo, sometimes itaweza chukua hata week 2 ndio wakaja kata, issue inakuja wanaweza block account yako, hela zote zikazuiliwa kutumika, sasa wanapokata hela yao wanasahau kuifungua account yako, ukikutana na customer care kimeo, haelewi tatizo ni nini, utaangaishwa kujaza ma form mengi na kuandika barua zisizo na mwanzo wala nyuma hadi uchoke.
 
Haya ndiyo yaliyonikuta kutoka CRDB bank, wasichukie ila wajaribu kuelewa kuwa tukiandika na kuanika mabaya tunayoyapata kutoka kwa Service Desk, Customer Care teams, Customer Service Reps ndio itakayopelekea wao kujirekebisha na kutoa huduma bora hapo baadae.

Matatizo kama haya huwa tunayapata kutoka yale makampuni yenye wateja wengi kuliko yale yenye wateja wachache.

Nimekuwa na tatizo na visa card yangu ya bank kwa mda mrefu, nilikuwa nashindwa kufanya manunuzi online, nashindwa ku-link card yangu na paypal na sio kama mimi ni mgeni katika hili. hivyo usije niambia process za kulink ni hizi na hizi.
Ok nielezee tu baada ya kushindwa kuitumia card yangu online nikapiga simu kwenye number ambazo zipo kwenye card yangu ( contact customer care ) kuelezea tatizo langu
nilijaribu kujielezea kwa umakini sana kuhusu tatizo langu na yeye akanijibu kuwa anachukua maelezo yangu na anayafikisha kwa idara inayohusika na nitajulishwa kwa
njia ya sms punde tatizo langu litakapotatuliwa. nikamwambia kama anaweza akanipa namba ya hiyo idara ili niwaelezee hili tatito, akanijibu kwa ufupi tu hapana na akakata simu.
nikapiga tena ikapolelewa na supervisor mwingine, ambae aliweza kutatua tatizo langu ndani ya dakika 3 tu, aliniambia subiri usikate simu na akaniweka on hold kidogo nafkiri labda
alikuwa anawasiliana na hiyo idara, alirudi online na kuchukua maelezo ya ziada na akaniambia account yangu haina hela hivyo niongeze halafu nijaribu kufanya manunuzi tena online pamoja na ku link card yangu na paypal.
Baada ya kuweka kiasi fulani cha hela mambo yakawa sawa na nililipia service ya dola xx na ikakubali na hapohapo nikapata sms ya muamala nilioufanya kutoka crdb bank.
Nikajaribu ku link card yangu na paypal nayo ikakubali. Baada ya siku nikapata tena muamala kutoka crdb ukionyesha kuwa nimefanya muamala na kama sitambui huo muamala nipige simu ili nieleweshwe, nikapiga simu na wakanieleza kuwa ule muamala nilioufanya
ndio umekamilishwa leo na wamenitumia hiyo sms kunijulisha na huo ndo mchanganuo katika Tsh, nikawaambia ok ila mbona muamala umekuja kwa mfumo wa USD na sio Tsh? wakasema hiyo ni Tsh na sio USD. basi nikawaelewa na kuwashukuru wakaniuliza kama nina swali lingine nikawaambia sina,
Cha kushangaza nilipotaka kufanya manunuzi mengine tena card yangu ikakataliwa kama ilivyokuwa awali, japo kulikuwa na balance kubwa tu ila ilikuwa inakataliwa, nikaongeza hela, hali ikawa hivyo hivyo,
safari hii nikaamua kwenda moja kwa moja kwenye tawi langu na kuijaribu card yangu kwenye ATM, napo ikagoma ikaleta ujumbe unaosomeka "sorry this transaction has declined", nikaingia ndani kwenye desk customer service, wakasema nijaze form halafu nilipie sh 5,900/= ili wa-reset password yangu, nikaambiwa baada ya hapo kilakitu kitakuwa sawa.
Baada ya kufanya hayo yote nikaambiwa nitapata sms kwenye simu halafu niingie kwenye ATM niweke password mpya nitakayotumiwa, sikupata sms wala nini na muda ukawa unazidi kwenda almost 2hrs, wakasema nijaribu hivyohivyo kwenye ATM na nikiulizwa password niweke 1234, nikafanya hivyo lakini bado nikawa napata ujumbe "sorry this transaction has declined".
Nikarudi tena ndani na yule alienihudumia mara ya kwanza akawa anamuhudumia mteja mwingine aliekuwa pembeni yake akaniuliza nikamwambia ujumbe ninaoupata kwenye ATM. akachukua card yangu na kuikagua kwenye computer yake na kunieleza kuwa card yangu imefungiwa hivyo lazima nijaze form ili waweze kuifungua,
nilifanya kama alivyonielekeza na akaniambia nimwone meneja ili aweze kuidhinisha, muda ukazidi kwenda na baada ya lisaa wakasema niende nirudi tena baada ya siku tatu.
Nilivyorudi tena baada ya siku tatu sikumkuta tena yuke meneja nikamkuta meneja mwingine, nikaanza kumwelewesha pale tulipoishia kabla ya yeye. achachukua card yangu na kuikagua tena kwenye pc yake, akasema card yangu imefungiwa walihisi ilitumika online pasipo idhini yangu tarehe zile ambazo mimi nilifanya muamala. nikamwambia ni mimi nilifanya huo muamala na kwanini waliifunga wakati sikulalamila?
kwa ushauri wake akasema nijaze form ili waweze kuifungua na wakachukua namba yangu ya simu ili wanijulishe. nikawauliza labda itachukua muda gani ili niweze kujua na nikiona siku zimepita niweze kuja tena, akaniambia we nenda tu tutakujulisha.
cha kunishangaza wiki mbili zimepita bila kupata sms kutoka kwao, nikaamua kwenda tena kwenye tawi langu na nikamkuta yule meneja wa mwanzo kabla ya huyu alieniambia nisubiri sms kutoka crdb. nikamkumbusha pale tulipoishia. akasema nijaze form ili nipate card mpya, safari hii nikawa mkali nikamwambia wiki mbili zilizopita nilikuja nikakukosa ila nilimkuta meneja mwingine nae akasema nijaze form nikajaza nikaambiwa nisubiri nitatumiwa sms kutoka crdb, lakini ni wiki mbili sasa sijapata sms kutoka crdb ndo nimeamua kuja tena
wewe unaniambia nijaze tena form nipate card mpya mbona kila nikija mnasema nijaze tu form hii ni safari ya tatu najaza form, na nikijaza kwaajili ya card mpya nayo nitaambiwa nisubiri tena wiki mbili, mbona siwaelewi? nikawauliza hivi ningekuwa na mamilioni kama Reginald Mengi ningekuwa nasumbuliwa hivi?
Nikawaambia Raisi anaposema watu hawafanyi kazi hajakosea, mshahara wako unatoka kwa wateja kama sisi, sasa mimi nikifunga account yangu na mwingine kwa maudhi kama haya akafunga, huoni kuwa mtapoteza wateja na hivyo kupelekea kwenu kutoona hela? halafu mtasema Magufuli kabana sana hakuna hela, kumbe ni ninyi hamtaki kufanya kazi.
Basi kwa maneno hayo akainua simu yake ya mezani na kuongea na idara inayohusiana na matatizo yangu na kisha kuniambia nisubiri kidogo. kwakuwa leo ilikuwa siku ya jmosi nikaona niwape muda, nikawaambia sina muda wa kusubiri naenda nitarudi jtatu na kama hawatakuwa na muafaka na card yangu basi nachukua fedha zangu zote nafunga account, nikaondoka.
Mi najua kuwa wako hovyo,ingawa sio mara zote.Tatizo ni kupeana kazi kwa kujuana,mtoto wa kaka,mjomba,jirani,rafiki nk.ila kubwa ni tabia ya kuoneana aibu,hakuna kuwajibishana pale kunapotokea mtu kakosea.Uzunguni wenzetu hawana hayo mambo.
 
Hamia Exim, achana na hao washajitosheleza
Hao majanga tupu mwezi wa 10 nlibank hela saa 6 halafu saa 9 nimerudi kudraw hela nilipie gari meneja ananiambia bank hakuna amount hiyo na hpo ilikua main branch,nkaona niende branch ya TFA nayo nkaambulia hela kidogo ilikua jmos ikabidi nisubiri mpka j3 ndio nidraw
 
Kununua chochote mtandaoni nanunua Visa ya Banc abc hapo hapo naweza fanya lolote
 
Mimi walinichomolea 3.5m, nilipowauliza wakaniambia eti ile siku nilipoenda kudraw yule teller akajisahau eti alipokuja mtu wa nyuma yangu akatoa kwenye akaunti yangu badala ya yake.., senseless..!
Sasa ulilipwa mkuu?
 
Back
Top Bottom