Crdb cardless simbanking ni kimeo

BabaTina

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
429
574
Guys kuna ishu hapa imeniboa imebidi leo niisemee makavu laivu...hawa jamaa wa CRDB leo ni siku ya 5 system yao mbovu ya Cardless imeng'ang'ania Pesa yangu hewani..ilikuwa ni siku ya ijumaa last week nilipokuwa nahamisha kiasi fulani cha pesa kwenda Cardless then system yao ikasema request yangu haikufanikiwa nijaribu tena, ajabu ni kwamba nilijaribu mara mbili na kupata majibu yale yale ya kutokafanikiwa.!! few minutes later kucheki salio nikakuta jamaa wamekata salio kwenye akaunti yangu kwa ile transaction iliyogoma kufanyika.
Nikawapigia simu kuwauliza wale jamaa wa call center wakasema system inatatizo na hivyo pesa yangu ingerejeshwa kwenye akaunti ndani ya masaa 48...ajabu ni kwamba mpaka hivi sasa hiyo pesa hawajaresha na kila nikiwapigia simu wanaishia kusema "Pole mteja wetu kwa usumbufu suala linashughulikiwa" huu ni upuuzi pole yenu hainiletei chakula mezani...masuala yangu muhimu yamekwama ninyi mnaishia kunipa pole na kuniambia suala langu linashughulikiwa!??? mie sitaki siasa nataka pesa yangu niweke chakula mezani!! nyasi za chooni zisikauke...Pamb***...nyang'**...Serious itabidi mnilipe huu usumbufu.......mik**** ye*****u
 
Thanda yaani ni kinyaaa mtupu...nikipata changu pambafy zao nafunga na akaunti...huu ni umbuzi kabisa
 
ulitumwa kwenda kufungua account crdb?hayo ndio madhara ya kuiga technolojia za nje pasipo kujipanga
 
Duh, mie nimeogopa kukupa pole maana najua pole yangu haitokuletea chakula mezani

Inaweza kuniongezea hasira....natamani kuingia msituni nichape bakora hizi huduma za "pole suala lako linashughulikiwa"
 
ulitumwa kwenda kufungua account crdb?hayo ndio madhara ya kuiga technolojia za nje pasipo kujipanga

Sikutumwa! nilikuwa natafuta huduma ambayo itarahisisha shughuli zangu za kila siku ili at the end of the day niweke chakula mezani...kwani we kufungua akaunti mpaka utumwe...!!???
 
Sikutumwa! nilikuwa natafuta huduma ambayo itarahisisha shughuli zangu za kila siku ili at the end of the day niweke chakula mezani...kwani we kufungua akaunti mpaka utumwe...!!???
wafungulie kesi hao jamaa wakulipe,ugali uende kwa meza,la sivyo nyasi zitaota mpaka kwenye masink ya kunawia mikono
 
acha tu mie nilinuna muda mfupi uliopita sasa hivi nimeamua nipotezee tu crdb simbanking ni utitiri mtupu
 
Kero kama hizi ndio zilizomfanya yule mzee wa Sumbawanga kulipua benki ya NMB kwa radi, hii benki inanikera, natafuta benki ya kuhamia...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom