Mods mnaeza Saidia kuiweka kwenye appropriate forum
Tabia kuu ya uhalifu na wahalifu ni kuwa:-
Uhalifu na wahalifu ni zao la jamii. Kabla ya kutaka polisi wafike mtaani kwenu kufanya Doria(impossible soltn on my views) maana mitaa yenye wahalifu ni mingi sio goba pekee, ninyi kwenye mtaa waathirika wakuu mmechukua hatua gani?
Je, mnashiriki ulinzi wenu na wa mali zenu?
Je mna vikundi vya ulinzi vilivyoshiba vijana wazalendo wanaofanya doria?
Je, jamii ya watu wa goba, wamefedheheshwa na uhalifu huo kama ulivyofedheshwa wewe au wao wanaona ni kawaida?
Ndugu soltn iko mikononi mwenu wana goba. Naomba nikupe mifano.
Hapa nilipo, matatizo ya uhalifu yalikithiri huenda kuzidi goba. Mwenyekiti wa mtaa alichofanya, aliwatambua wezi, akashtaki Polisi. Hata hivyo nothing was done.
Akaja na mkakati wa kuihamasisha jamii. Tunalipa 1,000/- kila mwezi ili kuwalipa posho vijana sita wanaofanya doria kuanzia saa 22:00 mpaka asubuhi.
Kwa doria hiyo, mwanamtaa ambaye sasa ni kero, amekamatwa hivyo kesi zote zinazomhusu zinaendelea. Na tangu akamatwe hajapata dhamana. Atakuwa akimaliza kesi moja anaendele na nyingine.
Mtaaa kwa sasa ni shwari