CP Simon Sirro Please take Note : Kushamiri kwa Mtukio ya Uhalifu Kata ya Goba

Mkusa

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
549
209
Kwako Commissioner Simon Sirro,

Siku za karibuni kumeshamiri matukio ya Wahalifu kuvamia Makazi ya watu katika kata ya Goba, watu wanaibiwa Mali zao, watu wanajeruhiwa na kuumizwa, Wanaume wanadhalilishwa mbele ya wake zao na wakati Mwingine mbele za watoto wao, watu wanapata usumbufu Mkubwa.
Halii hii imekuwa ikijitokeza katika kata ya Goba Wilaya ya Ubungo kana kwamba hawa wahalifu wana uhakika kabisa wa kutofanywa kitu.
Wana vamia almost kwa kutumia same style, Lat week wamevamia Nyumbani kwa Manajeshi Mmoja na kupora fedha na kumsababishia usumbufu Mkubwa kabisa.
Hawa Wahalifu wasipodhibitiwa hali itakuwa Mbaya sana.
Tumeona Wiki mbili zilizopoita Polisi wetu waki randa randa Mitaani kupasha Misuli moto kwa minajili ya kuongeza weledi na utayari wa kupambana na uhalifu.
Lakini kwa Wananchi wa kawaida tukiona bado tunanyanyaswa na wahalifu usiku Majumbani mwetu ilhali kila siku kwenye Luninga tunaona ASkari wetu wana Rehearsal na Silaha kali kwa kweli tunatatizika na kufadhaika sana.

Ushauri wangu:

1. Kamanda hebu waelekeze Askari wako kufanya fatiki yao ya Mazoezi kwa kuingia ndani ndani kwenye Mitaa ya watu ambako wahalifu ndio wanatunyanysa sana na sio kwenye Ma Barabara ambako si sehemu vutizi kwa wahalifu kufanya Matukio yao

2. Fatiki hiyo ifanyike Usiku , Mathalani kuanzia Saa nne usiku Mpaka saa tisa, Muda ambao wahalifu huepenedle kufanya uhalifu wao

3. Kuongeza Vituo vya Polisi kila Mtaa kwenye kila kata, prioirity iwe kwenye Mitaa ambayo iko Mbali na Vituo vikubwa vya Polisi, Kambi za Majeshi kama Magereza, JWTZ, Polisi etc

4. Kutazama upya ufanisi wa Polisi Call center iliyozinduliwa na Rais Mwezi uliopita, Binafsi nimeshawahi kupiga namba zao lakini sijawahi kupata Positive Response hata Mara moja

5. Kuangalia uwezekano wa Polisi pia kufanya kazi zinazofanywa na Makampuni binafsi ya Ulinzi, hii itakuwa ni source of income as well kwa jeshi la Polisi, wawe na Radio na Punic button kuwafungia watu majumbani mwao, same style kama makampuni binafsi ya ulinzi yanavyofanya

5. Ku engage makampuni binafsi ikibidi kuyasaidia pindi Matukio ya uhalifu yanaporipotiwa, imeonekana kwamba makampuni binafsi ya ulinzi response yao ni kubwa (Kwa sababu ya Biashara) sana hivyo wakiji integrate na Polisi itakuwa vyema sana pindi wakizidiwa na Wahalifu ili kupata Msaada zaidi.

Nakutakia kazi njema
 
Mods mnaeza Saidia kuiweka kwenye appropriate forum
 
Umeleta ukwelli mtupu kabisa na mapendekezo uliyotoa wayaangalie kwa kweli

Ila tutashughulika nayo tukimaliza kozi kwa RAS SIMBA
 
Poleni kwa hayo maswahibu. Kumwambia Sirro ni kupoteza muda tu ndugu yetu. Serikali hii, yaani Magufuli maana yeye ndiye kila wizara na kila taasisi, haitaki ulinzi shirikishi wakati polisi kiidadi na uwiano ni wachache. This is pure nonsense.
Kingine Sirro hawezi kufanya kitu mpaka aambiwe na mwanasiasa fulani. This is pure uselessness.
 
Goba kama wiki tatu zilizopita,kila siku Nlikuwa naisikia milio ya risasi usiku,mitaa ya njia panda pale karibu na bar,osterbay pale na kwa Moga,mpaka najiuliza hivi Goba hakuna Kituo cha polisi au mpaka Goba mwisho,polisi wasaidie watu wa Goba,kutokana na hali ya mazingira halisu ya Goba wezi wanavutiwa sana kuvamia,wanadhani Yale majumba yana pesa.
 
Mods mnaeza Saidia kuiweka kwenye appropriate forum
Tabia kuu ya uhalifu na wahalifu ni kuwa:-

Uhalifu na wahalifu ni zao la jamii. Kabla ya kutaka polisi wafike mtaani kwenu kufanya Doria(impossible soltn on my views) maana mitaa yenye wahalifu ni mingi sio goba pekee, ninyi kwenye mtaa waathirika wakuu mmechukua hatua gani?

Je, mnashiriki ulinzi wenu na wa mali zenu?
Je mna vikundi vya ulinzi vilivyoshiba vijana wazalendo wanaofanya doria?
Je, jamii ya watu wa goba, wamefedheheshwa na uhalifu huo kama ulivyofedheshwa wewe au wao wanaona ni kawaida?

Ndugu soltn iko mikononi mwenu wana goba. Naomba nikupe mifano.

Hapa nilipo, matatizo ya uhalifu yalikithiri huenda kuzidi goba. Mwenyekiti wa mtaa alichofanya, aliwatambua wezi, akashtaki Polisi. Hata hivyo nothing was done.

Akaja na mkakati wa kuihamasisha jamii. Tunalipa 1,000/- kila mwezi ili kuwalipa posho vijana sita wanaofanya doria kuanzia saa 22:00 mpaka asubuhi.

Kwa doria hiyo, mwanamtaa ambaye sasa ni kero, amekamatwa hivyo kesi zote zinazomhusu zinaendelea. Na tangu akamatwe hajapata dhamana. Atakuwa akimaliza kesi moja anaendele na nyingine.

Mtaaa kwa sasa ni shwari
 
Goba ni kama kapori flani hivi japo ni sehemu inayokuwa,mkuu karibu hapa goba luxury.
 
Kweli kabisa uhalifu udhibitiwe, waimarishe kile kituo wapewe magari na askari waongezwe! Mbona kwenye siasa wanaweza tena haraka na upesi sana? Waache kucheza na maisha ya wananchi! Wafanye upesi
 
Back
Top Bottom