COVID-19 na anguko la Shule za English Medium

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,106
27,085
Naliona anguko la shule za English Medium Tanzania.

Naona wazazi wengi wakiwatoa watoto wao kwenye shule za English Medium na kuwapeleka kwenye shule za kayumba.

Sababu? Sababu ni zile zile

1. Uhaba wa fedha: Wazazi wengi wataishiwa fedha na hivyo kushindwa kumudu gharama za kuwasomesha watoto wao kwenye shule za English Medium

2. Tukio la kustukiza la Corona limewafundisha watu wengi Somo moja kubwa Sana kwamba maisha yanaweza kubadilika wakati wowote na hivyo ni muhimu kuwa na akiba ya pesa na chakula cha kutosha wakati wote ili linapotokea tukio la dharula kama hili la Corona basi wasi hangaike.

Kwa hivyo basi Wazazi wengi wataanza kuona umuhimu wa kujiepusha na matumizi makubwa ya pesa yasiyo ya lazima.

Kutumia Milioni 5 Kwa mwaka kumsomesha mtoto kwenye shule ya kiingereza ili upate fahari ya kusifiwa mtaani kwenu unamsomesha mtoto wako kwenye shule ya mamilioni wakati ungeweza kumsomesha kwenye shule ya kayumba halafu ukamfanyia thoroughly and extensive academic management Kwa gharama kidogo ni.matumizi ya pesa yasiyo kuwa ya lazima.

Kulipa mamilioni kwenye English Medium ili Tu uone fahari mtoto wako aki kuiteni " Daddy and Mom" au akijua kutumia You Tube at age 3 ni matumizi mabaya ya fedha cause hivyo vitu hata watoto wa shule ya kayumba wanaweza kufanya.

Kama ni kuongea kiingereza hata Tid na Q chila wanaongea kiingereza Lakini hawakusoma English Medium.

Matter of fact TID who went to Kayumba speak better and fluent English than P. Funky Majani who went not only to an English Medium School but to an International School of Tanganyika.

So Watanzania wengi wataanza kuji budget now.

3. Kwa sababu ya conspiracy theories nyingi kuhusu Covid 19 kuna kundi kubwa Sana la Wazazi ambao wame subscribe into the theory . Na Kwa sababu ya hofu dhidi ya theories mbalimbali kuhusu Covid kama vile ID2020, 5G etc Wazazi wengi wamekata tamaa and they be like kama Mambo yenyewe ndio haya there is no hope for the future, kuwasomesha watoto English Medium ni kupoteza pesa Tu bure na kujistress.

4. Lipo kundi kubwa la Wazazi ambao lime subscribe kwenye nadharia kwamba tukio la covid 19 ni ishara ya kukaribia kurejea Kwa masiha. Rejea ishu ya Id2020 ilitabiriwa kwenye ufunuo. So they will be like hakuna umuhimu wa kutoa mamilioni shule za kiingereza wakati there is no hope for the future.

5. Lipo kundi la Wazazi ambao walikuwa wanawapeleka watoto wao shule za English Medium kwa sababu ya mkumbo huku wakiumia so watatumia tukio la covid 19 kama excuse ya kuwatoa watoto wao from St schools na kuwapeleka kayumba.

Wamiliki wa shule za English Medium jiandaeni kisaikolojia
 
Mimi nilichojifunza kwenye janga la covid 19 ni kuwa na uzazi wa mpango na kuiboresha familia yako. Chukulia mfano Magufuli aseme kuanzia leo watu wajifungie ndani mwezi wasitoke nje.

Je, wale waliozaa hovyohovyo wakaanza kurundikana wote ndani ya chumba na sebule nn kitatokea. Shule sio inshu maana zitafungua na maisha yataendelea. Inshu mrundikano + umasikini.
 
Sijawai kuona engineer au dokta aliyesoma hizo international zenu.. ama country bet student A level aliyesoma hizo english medium..

Hata best students wa vyuo vikuu kila mwaka ni zao la kayumba
Una uhakika na unachokisema? Unaweza ukaleta takwimu?
 
Nimesoma shule ya msingi kayumba
Nikasoma secondary kayumba
Nikasoma advance kayumba
Nimesoma na chuo kayumba

Tofauti niliyoiona katika interview kati ya tuliosoma kayumba na waliosoma English media.

Wanangu hawatasoma kayumba labda nishiwe kabisa uwezo wa kuwasomesha sitaki wanangu wakutane na shida kama nilizopitia Mimi baba yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wanaenda kusoma vyuo vya nje na kazi wanapatia hukohuko

Wale wa IST na shule zingine zinazotumia mitaala ya nje sawa... ila hawa wa daraja la kati kama tusiime, st marys etc.. tunakutana nao vyuo vikuu vya uma.. Wakiwa vilaza tu wanakimbizwa na sisi kayumba darasani..

UDSM wamejaa kibao tena sio kozi za coet wao wamejaa kozi za arts na social science na wanabuluzwa na kayumba.. narudia tena sijawai ona best student aliyeoma english medium chuo kikuu
 
Acheni kabisa kulinganisha kayumba na english medium. Mental development Activity zilizoko english medium ni kubwa sana kulinganisha na huko kayumba mnakosema.

Mtu anasema kasoma kayumba na bado kawa daktari au engeneer kwa udaktari gani ulio nao na ui engeneer wa kukariri

90% ya graduate wa kayumba wamekariri hata barua ya kazi mtu ana Google, wengi mnajifunzia kazi kazini, watu ni weupe sana, graduate wa sheria, uhasibu mchukie leo mpeleke ofisini mpe kazi uone

Haya ninyi madaktari wa kayumba mmesaidia nini nchi hata sasa kwenye mlipuko wa magonjwa mnakimbia wagonjwa.

Kwanza ulisikia lini aliesoma kayumba, kamaliza kidato cha nne akapata scholarship direct kwa credible college/university ulaya? Kayumba Uta Hustle weee mpk ufike level ya Masters ndio uanze kuomba tu vyuo nje lkn wanao mapiza feza na kunakofanana na huko kacheki uwezo wao huko na scholarship zinavowatembelea, na wengi wanafanya kazi hukohuko

Madaktari wa Tanzania hata Kenya haiwataki (kayumba)

Dumelang
 
Pengine CORONA sasa itasabababisha Shule nyingi za Kayumba ( Serikali ) zianze Kuthaminiwa na wale waliokuwa wakizipuuza.
 
Back
Top Bottom