Mkuu
Nguruvi3, kama wewe hauko maabara mwenyewe, basi usiwe na 100% ya ukweli kuwa wazi kisa ni Sayansi.
Sayansi inaweza geuzwa kuwa Siasa wakati wowote. Ni hitajio tu linapotokea.
Nilitamani sana kujua ni nini hasa kiko ndani ya hili janga corona. Kwanini mara zote limekuwa kama linacheza mchezo wa kupishana njia?
Chanjo kutozuia Maambukizi,
Kuongezeka kwa Aina, nk yaani kwa namna yoyote linataka tuamini kuwa HALIWEZEKANI.
Mkuu , ni namna gani unaitumia sayansi ndilo jambo la muhimu sana.
Sayansi inaweza kutumika katika siasa, uchumi, jamii , kigaidi, kijeshi n.k.
Ugunduzi wa atoms na electrons ulipelekea ugunduzi atomic Bomb iliyoua halaiki kule Nagasaki na Hiroshima
Sayansi imeleta ugunduzi wa mabomu. Kisayansi mabomu ni ''combustion'' na hvyo basi combustion zinazotumika katika ndege , Magari na mashine nyingine ni 'mabomu' katika ''calculated amount''
Ndivyo ilivyo kwa dawa za binadamu ambazo ni ''sumu'' lakini sayansi inatuwezesha kunywa na kupona
Kwahiyo ukinywa dawa ni sawa na kunywa sumu katika kiwango kinachokubalika
Ni sayansi inatuwezesha kupeleka chombo maili 300 kutoka duniani kuangalia sayari nyingine.
Lakini pia sayansi inatuwezesha kutekeleza uchumi, shughuli za kijeshi, kijamii na siasa ikiwemo
Hoja ni kuwa sayansi haina tatizo, kuna tatizo wakati wa kutumia sayansi na watumiaji wa sayansi.
Kama unaambiwa virus wanaambukiza halafu unaamini si virus ni vita ya uchumi ! tatizo si sayansi.
Kuhusu hoja ya chanjo, hili nalo tumelijadili sana. Kwamba kuna jamii ya virus ambayo utengenezaji wa chanjo yake una challenges. Moja ya virus hao ni HIV-AIDS kwasababu za kisayansi (ndefu kuzieleza)
Ukisikia kuna mutation basi wapo virus wanafanya mutations kwa kasi sana na kwa namna tofauti kiasi kwamba vaccines iliyogunduliwa leo inaweza isifanye kazi baada ya mwezi.
Inategemea aina virusi. Katika nchi za magharibi ''flu' inapita kila mwaka na chanjo za flu ni kila mwaka.
Si jambo geni.
Kwahiyo ni lazima kwanza uelewe vaccines zinafanyaje kazi, zina target wapi, zinakuwa za aina gani.
Je, ni live atenuated? Je, ni extracts za proteins ? n.k. n.k.
Katika hili ni kuelewa sayansi . Tatizo kubwa lipo kwa wapiga ramli na madogori kama wale wanaotengeneza Togwa bila kueleza inafanyaje kazi. Ni kuongozwa na hisia tu!
Hatuwezi kuwa peke yetu kwenye dunia hii ! tumeumiza watu wetu kwa ujuha wa changamoto za kupumua
Tumejificha nyuma ya ujinga tukiamini tumejificha.