COVID-19: Imechochea udhalilishaji wa kijinsia na ukatili majumbani?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42 kutoka Nigeria aitwaye Consolata (sio jina lake halisi) aliandika kwenye mtandao wa kijamii, “Kabla ya leo, kuwa mhanga wa ukatili majumbali ilikuwa kitu kilicho mbali sana na akili yangu, lakini leo ni jinamizi kwangu. Hofu na hisia ya kukosa matumaini zinanizidia. Nimechanganyikiwa kabisa!” Saa mbili baada ya kuandika ujumbe huo, mwanamke huyo alijirusha kutoka nyumba yake iliyo ghorofa ya 11 na kufariki.

Matukio kama hayo, ingawa si yote yanasababisha mauti, yametokea katika nchi nyingi duniani, hasa baada ya kutokea mlipuko wa virusi vya Corona. Hata kabla ya kutokea kwa janga hili, ukatili wa majumbani na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni vitu ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa sana.

Tatizo hili limeongezeka mara dufu baada ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona ambalo limesababisha wanawake na watoto kukaa muda wote na watesi wao, hawana sehemu ya kupata afueni, maana huenda kwenda shuleni, kazini ama kwenye shughuli mbalimbali kulikuwa kunawasaidia hata kupata ushauri kutoka kwa marafiki zao, na kuwapa muda kidogo wa kupumua. Lakini kutokana na marufuku ya kutoka nje, hawana pa kwenda wala wa kumkimbilia.

Katika mkoa wa Hubei nchini China, ambao ulikuwa kiini cha mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo, kesi za ukatili dhidi ya wanawake ziliongezeka kutoka 47 mwaka jana hadi kufikia 162 mwaka huu. Mara nyingi kesi hizi ziliporipotiwa katika vituo vya polisi, polisi hawakutilia maanani kesi hizo, na kuwaacha wanawake wakijilinda wenyewe wakati wa karantini.

Nchini Marekani, ambayo inaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaopiga simu katika Kituo cha Taifa cha Kushughulikia Ukatili Majumbani, wakilalamikia kufanyiwa ukatili na wenza wao, ikiwemo kutishia kuwafukuza majumbani na kuwaacha nje ambako watapata maambukizi. Mkurugenzi wa kituo hicho Katie Ray-Jones amesema, kuna baadhi wa waonezi hao wanakataa kuwapatia wenzi wao fedha au hata matibabu. Vitendo kama hivi vinawafanya wanawake kujihisi kuonewa, hawana thamani, na kufanya maisha yao kwa ujumla kuwa magumu sana.

Ukichunguza kwa makini, yote haya yanasababishwa na kulegea kwa taasisi ya malezi ya watoto. Wazazi na walezi tumesahau umuhimu wa malezi na makuzi ya watoto wetu. Athari hii ya ukatili majumbani, unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa watoto utaisha mara tu kila mtu mmoja mmoja atakapojifunza kuwa anao wajibu wa kujilinda na kuwalinda watu wote wanamzunguka, kusikilizana na kutatua mambo yanatowatatiza watoto kwa wakati.

Kama wazazi ama walezi, tunapaswa kufuatilia mienendo ya watoto wetu, tunapaswa kuwa na muda wa kukaa na kuongea nao kuhusu masuala yanayowasumbua, na tunapaswa kuwalinda watoto wetu wanapokuwa nyumbani na hata wanapokwenda kuatembelea marafiki zao.

Tunapaswa kufahamu kwamba, binadamu wote ni sawa, na haki za binadamu si kwa baadhi tu, bali ni kwa wote. Wanawake wana haki sawa na wanaume, unapompiga ama kumdhalilisha mwanamke au unapomfanyia ukatili mtoto sio kwamba unaonyesha jinsi ulivyo shupavu na mwenye mamlaka dhidi yake, bali unaweka wazi udhaifu wako katika jamii inayokuzunguka.
 
Much true.
Tanzania hatuna lockdown.tupo na Amani sana.ukatili upo na upo kila mkoa ,wilaya ,kata ,kijiji na kitongoji .hauwezi kuisha lakini matukio yakitokea ndio tutaona kwa taarifa ya Habari. Lakini upo mno katika kila jamanii.

Thanks for info.
 
Back
Top Bottom